Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 27 October 2013

Nawatakia J'Pili yenye Baraka;Burudani-Kijitonyama Choir,Ndani Ya Safina,Hakuna Kama Wewe!!!

Nimatumaini yangu J'Pili hii inaendelea vyema.. Iwe Yenye Neema,Baraka,Upendo na Amani....

BWANA akamwambia Nuhu,Ingia wewe na Jamaa yako yote katika Safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki... 
Neno La Leo;Mwanzo:7:1-24


Ndani Ya Safina aahhh....ndani ya Safiiina aa humo ndani ya Safina oooohh kuna upendo mwingiiii..........Mhhhh..Wanyakyusa kwa Waheheeee..Wasambaa kwa wadigoooo..Njoni wote Tuingieee...






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana

Saturday 26 October 2013

chaguo La Mswahili Leo;Mrisho Mpoto!!!!

Waungwana ni wakati mwingine tena wa "Chaguo La Mswahili"Leo chaguo limeangukia kwa kaka Mrisho Mpoto[HOME BOY]Mpoto kama ukimsikiliza juu juu..huwezi kumuelewa kabisa na ukashangaa huyu naye anaimba nini?Lakini ukitulia na kumsikiliza maneno anayotumia utakubaliana nami..Maneno yake ni Vichocheo,Mafunzo,Maisha Na Jamii inayotuzunguka...
Mhhh..mimi Mpoto ananikosha/nibamba/Kupenda kazi zake,,,Vipi wewe mwenzangu?


Iyeeehhh Mjomba Iyeehh...!!..Bora kujenga darajaaaa...!!
Mjomba hapa Nyumbani Tuna hadithi  na misemo mingi kujihakiki,Maana lake mtu halimtapishi Lakini kukumbatia maji kama jiwe ni ujingaaa...
Twende Sote sasa....








"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Msiba wa Martha Shani DC


Katika kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA wiki hii... Kutoka nchini Marekani, tuanze na habari za msiba ulioikumba jamii ya waTanzania waishio maeneo ya Washington DC.

Marehemu Martha Shani

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).a


Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 26, 2013 





*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Wednesday 23 October 2013

Tuesday 22 October 2013

MAENDELEO YA MSIBA WA BI MARTHA SHANI WASHINGTON DMV


                                          Marehemu Martha Shani[1976-2013]
Marehemu Bi Martha akiwa na mumewe Alex Pamoja na watoto wao Jose naChris 
                                         
                                   
NDUGU YETU ALEX KASSUWI BADO ANAHITAJI MSAADA WETU WA HALI NA MALI ILI KUWEZESHA KUSAFIRISHA MWILI WA MPENDWA MKE WAKE ALIYEFARIKI GHAFLA SIKU YA JUMAMOSI OCT 19, 2013.

KUTOA NI MOYO NA CHOCHOTE UTAKACHOWEZA KITASAIDIA NA HATIMAE KUWEZESHA SAFARI HII NDEFU YA KUMPELEKA MAREHEMU KATIKA MAPUMZIKO KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE TANZANIA

GHARAMA ZA MSIBA KUSAFIRISHA MAREHEMU NA FAMILIA YAKE NI $19,500

FEDHA ZILIZOPATIKANA HADI SASA NI $4,300
ZILIZOBAKI $ 15,200

TAFADHALI TUMA RAMBI RAMBI ZAKO KUPITIA ACCOUNT IFUATAYO :-
# 446030759150 BANK OF AMERICA,MD
ROUTING # 052001633
MAJINA KWENYE ACCOUNT NI ALEX KASSUWI & FAITH ISINGO

CHEKI ZINAWEZWA ANDIKWA KWA ALEX KASSUWI AU FAITH ISINGO.

PIA UNAWEZA KUTOA RAMBIRAMBI ZAKO KWA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU AMBAKO NDIKO MSIBA UPO
ADDRESS NI

482 ARWELL CT
FREDERICK, MD,21703

AU WAWEZA WASILIANA NA MMOJA YA WANAKAMATI HAPO CHINI NA KUMUELEKEZA UPO WAPI ILI AWEZE KUKUSANYA MCHANGO WAKO

Tino Malinda -240-565-7133
Dickson Mkama - 301-661-6207
Mariam Mtunguja - 240-422-1852
Quizella Ntagazwa - 240-602-5011
MV Mtunguja- 240-593-0575
Victor Marwa - 240-515-6436
Faith Isingo - 240-705-1055
Julius Manase-240-393-8445

UKISOMA UJUMBE HUU TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZIO, MZIGO HUU NI WETU SOTE NA KWA PAMOJA TUNAWEZA

HAKUNA KIDOGO PALIPO NA NIA. NA HAKUNA KIKUBWA PALIPO NA UMOJA.

Sunday 20 October 2013

Tumalizie J'Pili hii Vyema;Burudani- The Whispers Band-Nina Baba yangu asiyeshindwa kamwe na Nyingine!!!

Wapendwa muendelee na J'Pili kwa Amani,Furaha na Bidii....
Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

Neno La Leo;Mithali:22:29 na Muhubiri:9:10






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

TAHADHARI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI; Sasa wanatumia mitandao ya Internet ya Kuomba ajira, TAFADHALI soma taarifa hii usije ukalizwa.



Kuna UTAPELI mpya umeingia Nchini, kuna watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo za kazi huzitangaza kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa.

Matukio yenyewe yanakuwaje: Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai  wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho.

Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.

Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli.

KUWA MAKINI EWE MTANZANIA

IMETOLEWA NA:
MDAU MPENDA HAKI