Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 7 July 2012

EXTRA BONGO WAFUNIKA MBAYA KATIKA UZINDUZI WA UKUMBI WAO MPYA NEW WHITE HOUSE A.K.A BONGO RESORT KIMARA KOROGWE NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.!!!


Rais wa bendi ya Extra Bongo Ally Choki akiimba mbele ya wapenzi na washabiki wa bendi yake ndani ya ukumbi wao mpya New White House aka Bongo Resort Kimara Korogwe jana.

Rogert Hegga Katapila akiimba mbele ya washabiki wao katika ukumbi wao mpya uliopo Kimara Korogwe Dar es salaam.
Ally Choki na Henry

Mnenguaji mahiri wa Extra bongo akiwapagawisha washabiki wao ndani ya Kimara Korogwe.

Wakata nyonga wa kiume wa Extra Bongo wakiwakimbiza washabiki wao ndani ya ukumbi wao mpya Bongo Resort Kimara Korogwe.

 la Extra Bongo Banza Stone A.K.A Makaveli, Generale akipagawisha wapenzi wao ndani ya White Inn Kimara Korogwe.Jembe

Mwanamuziki wa BAIKOKO akiimba mbele ya washabiki wa Extra Bongo ndani ya Kimara Korogwe.

Tunda Man naye hakuwa nyuma katika kuwaburudisha mashabiki wa Extra Bongo.

Mwanamuzi wa Kizazi kipya Bongo Fleva Sheta akiwakimbiza washabiki wake ndani ya ukumbi mpya wa Extra Bongo katika uzinduzi wa ukumbi huo.

Extra Bongo jana walizindua ukumbi wao mpya New White House a.k.a Bongo resort uliopo kimara Korogwe. Uzinduzi huo ulisindikizwa na kundi la bendi ya taarabu Coast modern Taarab chini ya omary tego na Maua Tego, Tunda Man, Cheta na kundi maarufu la BAIKOKO ambalo linapiga muziki wenye maadhi ya utamaduni wa makabila ya watu kutoka Mkoa wa Tanga.

Friday 6 July 2012

MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE!!!!!


ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutakuwa na maonyesho yatakayoenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile Kisukari, moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi.
Mbali na huduma hizo, malengo makubwa ya hospitali katika kuadhimisha miaka 100, ni kupambana na changamoto zilizopo wilayani na nchini kwa ujumla katika kutoa huduma bora za afya.
Baadhi ya changamoto hizo ni upungufu wa wataala wa kada mbalimbali na uchakavu wa miundo mbinu.
Kupitia sherehe hizi, hospitali ina mpango wa kuanzisha chuo cha taaluma za afya na tiba wilayani Karagwe mapema mwakani.
Chuo hicho kitatoa wataalam katika fani za Uuuguzi, Uganga, wataalam wa Maabara na Maafisa afya.
Ш Faida za Chuo hiki:
o Kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam Mkoani Kagera na nchini kwa ujumla.
o Kusaidia vijana wanaomaliza elimu ya sekondari kupata elimu ya taaluma kwa gharama nafuu, zingatia mkoa hauna chuo cha waganga, ni gharama kubwa kwa wazazi kupeleka watoto wao nje ya mkoa kusomea taaluma hio.
o Chuo kitatoa nafasi nzuri kwa watumishi waliopo kazini kuweza kujiendeleza wakingali katika mazingira ya familia zao hivo kupunguza gharama na usumbufu wa kusomea nje.
o Chuo kitasaidia kuongeza ajira hivo kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.
Katika kufanikisha malengo hayo, jumla ya shilingi 1.8 billion zinahitajika. Ikiwa ni kwa ajili ya uendeshaji wa maadhimisho (utoaji wa huduma bure kwa wiki ya maadhimisho), ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa chuo.
Kwa niaba ya menejiment ya hospitali, nakuomba ewe mpenda maendeleo uchangie kufanikisha malengo haya kwa maendeleo ya sekta ya afya.
Wote watakao changia wataorodheshwa katika kitabu maalum cha kumbukumbu.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu kwa Mganga Mkuu: 0762 751 335 / 0712 916 800 / 0787 785 969
Shukrani
Dr. Andrew Cesari
Mganga Mkuu
Nyakahanga Hospital

Thursday 5 July 2012

FFU kupeleka hewani "Bongo Tambarare" na "Supu ya mawe"!!!!!!!!!




    WaTanzania  Kusherekea Saba Saba na CD " BONGO TAMBARARE"
                         Ya Ngoma Africa Band
  
     Nyimbo za "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" Kutinga Redioni


Wakati tunapoelekea katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba,
watanzania tunafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo
mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya
muziki wa dansi  Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani,
CD hiyonyimbo tatu  "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari"
Inasemekana imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio
duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa,hili watanzania wenye
Bongo Tambarare yao wapate raha ya muziki.
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii,
kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na  wake kiongozi wa bendi hiyo
kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo
afande Chris-B.
Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa 
kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Wednesday 4 July 2012

Wanawake na Urembo-Kunyoa Nyusi -Burudani Kipepeo!!!!!!



Waungwana Leo tuangalie Unyoaji Nyusi, Sikuhizi hata Waume wananyoa Nyusi.
Jee wewe  Unapenda kunyoa nyusi?
 Ungependa Mkeo/Mumeo,Mpenzi wako Anyoe Nyusi?


Jee unatumia njia gani?Jee unapenda kutoa zote au unapunguza tuu?


Hivi Watu wa Zamani nao walinyoa Nyusi?
Kunyoa Nyusi kunaweza kusababisha madhara yoyote kiafya?


Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana!!!

Monday 2 July 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Mapishi ya Cold Vegetable Soup - Recipe of (Swahili)!!!!!!


Waungwana "JIKONI LEO" Pata video mpya kutoka "TUPIKE PAMOJA" Wanakuletea mambo ya Supu!!
Supu si Nyama tuu, Ungana nao kupitia www.tupikepamoja.com pia unaweza kuungana nao You tube.
Mhhh Tamu sana!!!!!!!!
 Unaswali au Maoni? Usisite kuongea nao ,Usife nalo....hahahaaha "Pamoja sana Swahili NA Waswahili"

Sunday 1 July 2012

J'Pili ya leo, Tujifunze kupitia kaka Mubelwa na Mch.F.Shideko !!!!!!!!



Kaka Mubelwa Bandio[Mzee wa Changamoto]

Sijawahi kuhusika na mwisho wa maisha ya mwanadamu kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Kaka Domitian Rutakyamirwa. Na katika kuhusika huku, (tangu kuugua mpaka harakati zilizofuata baada ya kifo chake) nimegundua na kujifunza mengi kuhusu mtu, utu na watu. Ni kwa kupitia maisha ya mwisho ya Kaka Domi, nimeweza kujiakisi na kuakisi mengi yanayoendelea katika maisha yetu wanadamu na kuweka bayana “ndivyo-sivyo” ya maisha yetu.
Binafsi nimeshuhudia maisha yangu yakikaribia kifo tena cha ghafla katika matukio tofauti na bado sikuona ama kujifunza nililojifunza sasa.
Nakumbuka kauli ya mwisho niliyoisikia ikitoka kinywani mwa Kaka Domi ni ile ya kutubu aliyoongozwa na Mchungaji akiwa wodini.
Katika matukio yote niliyokumbana nayo, na ambayo wenzangu baadhi walipoteza maisha, hakuna kati yao aliyepata nafasi ya kutubu na kumuomba Mungu kama alivyofanya Kaka yangu huyu.
Na kama alivyohubiri Mchungaji kwenye ibada ya mazishi, mambo makuu matatu aliyosisitiza ni kuwa
1: Hatujui tutaondoka lini.
2: Hatujui tutaondokea wapi.
3: Hatujui tutaondoka vipi
Domitian, aliyekuwa Kaka, rafiki, Mume, mzazi na mlezi kwa wengi aliishi maisha ambayo yamekuja kudhihirika katika wakati wa uhitaji wake.
ASANTENI NYOTE
Maisha ya Domi yamedhihirisha UMOJA unaotamaniwa na waTanzania hasa wa Washington DC na vitongoji vyake ambao kwa namna moja ama nyingine unakwamishwa na mambo mbalimbali, lakini pale inapotokea tofauti zetu zikawekwa kando kwa ajili ya

 mtu aliyekuwa nasi sote licha ya tofauti zetu, tunaona matunda ya umoja. UMATI unaojitolea kufanikisha jambo kwa namna ya kipekee sana.

Inaendelea.ingia http://changamotoyetu.blogspot.co.uk
                             Marehemu;Domitian Rutakyamirwa; Ulale kwa Amani.[Rafiki wa kaka Mubelwa]

Mahubiri ya Mch. Ferdinand Shideko kwenye ibada ya kumuaga Ndg Domitian Rutakyamirwa iliyofanyika Jumatano June 27, 2012 kwenye kanisa la
The Way Of The Cross Gospel Ministries (at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 2074

U.S.A

Wapendwa; muwe na j'Pili yenye Amani,Baraka,Pendo na Umoja.

Samehe Usamehewe,Mungu atusaidie katika Msamaha!!!!!

            "Swahili NA Waswahili" Nimesamehe na Nawapenda Wooote!!!!!!!

ENGINEER DEUSDEDIT MALULU NA DORIS KASAKA WAMEREMETA KATIKA NDOA YAO TAKATIFU ILIYOFUNGWA JANA.!!!!!


Engineer Deusdedit Malulu akiwa na mke wake kipenzi Doris Joseph Malulu, kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa Takatifu jana katika kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara.

Engineer Deusdedit Malulu akimvisha pete ya ndoa mke wake mpenzi Doris Kasaka aliyefunga nae ndoa takatifu jana.


Familia ya Mzee Njelu Kasaka wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto wao wapendwa Doris Kasaka Malulu na Engineer Deusdedit Malulu waliofunga ndoa takatifu jana jioni.

Maharusi kwa nyuso za furaha wakipiga picha na Mtoto wao.



Engineer Deusdedit Malulu na Mkewe Doris wakikata Keki kwa pamoja kuonyesha kuonyesha ishara ya umoja na mapendo.
Meza kuu ya Familia ya Engineer Deusdedit Malulu

Meza kuu ya Wazazi wa Doris Kasaka.


Engineer Deusdedit Malulu na Doris Kasaka walifunga ndoa takatifu katika kanisa la Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara jana Tarehe 30/06/2012 na baadae kwenye Sherehe ya nguvu iliyofanyka katika ukumbi wa Luxery Mbezi Mwisho.

Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Shirika la ugavi wa Umeme (TANESCO) Makao Makuu na Bi Harusi ni mwajiriwa wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ZANTEL Dar es salaam.


Swahili na Waswahili Tunawatakia Maisha mema yenye Furaha,Amani na Baraka.