Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 6 November 2011

ALFEO SILUNGWE AKIITANGAZA TANZANIA KATIKA MOJA YA PRESENTATION ZAKE INDIA.




Alfeo Silungwe Mtanzania anaye piga Nondo ya Masters of Statistic ndani ya Nchi ya India akiwa anafanya presentation katika moja ya kozi anayo isomea chuoni hapo.





                                                   Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
                          Asante sana.
                                  


Trehe:5/11 NI SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU.


Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.



Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.


Habari hii nimetumiwa na Kabipingaz Blog
Asante sana.

Saturday 5 November 2011

Nawatakia Eid Njema Wapendwa!!!!!

                   Eid yenye FURAHA.
                        Eid yenye UPENDO.
    Eid yenye AMANI. da'Sabrina Kiwinga anatuwakilisha Swahili na Waswahili.

Muwe na Eid njema yenye Furaha,Upendo na Amani !kwa watu wote.
Tupate kusameheana na Tushirikianae vyema siku zote.




Nakumbuka nyumbani Eid kama hii, vyakula vilikuwa vinatembea tuu,vya Nyumba hii vinaliwa na Nyumba nyingine, Nyumba za Waislam kupelekea hata wasio waislam au kula nao pamoja.na Ikiwa Christmas nayo vivo hivyo,kulikuwa hakuna cha Udini wala nini wote Mnafurahi pamoja, kuoga na kuvaa nguo nzuri[za Sikukuu].
Sijui huu Upendo kama upo.Mungu atubariki na kutupa upendo wa Kweli.


EID NJEMA KWA WOTEEEE.






HATARI ILIYO MBELE KWA WAMACHINGA WANAOONGEZEKA KWA KASI KATIKA MATAA YA UBUNGO SERIKALI MNAIONA?

Trafiki Polisi akiongoza magari katika junction kubwa ya Ubungo, maarufu kama Ubungo Mataa.

Fuso ikiwa imeingia katika moja ya mtaro mkubwa ulioko bara bara ya Ubungo karibu na Ubungo mataa.

Kwa kipindi kirefu sasa eneo la Ubungo karibu na Mataa ya kuongozea magari yanayo ingia Jijini au yale yanayotoka pande mbili, mengine yakitokea Mwenge na mengine yakitoke Buguruni na kwenda sehemu mbali mbali za jiji limevamiwa na wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Nimejaribu kulifuatilia kwa kipindi kirefu ili kuweza kujiridhisha kujua kama wamepewa ruhusa na nani kufanya biashara katika eneo lisilo rasmi, nilijaribu kuongea na wamachinga wachache; wa kwanza anaitwa Salum Ramadhan anauza taa za kichina katika eneo hilo, yeye alidai hawajaruhusiwa na mtu kufanya biashara hapo ila ni kutokana na ugumu wa maisha ndio umewapelekea kufanya biashara katika eneo hilo na wa pili naye Ndg. Deogratius Shirima akasema maneno hayo hayo ambayo hayapishani maana na huyu wa kwanza.

Sikuishia hapo nikataka kujua je kuna mtu yeyote ambaye anakuja kukusanya japo ushuru kutoka kwao? nao kwa pamoja wakasema kuna mtu huwa anakuja kukusanya ushuru lakini wao hawana uhakika kama ni kutoka Serikali za mitaa au la! nikawauliza swali jingine, huyu jamaa ambaye ameweka jenereta hapa na kuwapa huduma ya Umeme mnamlipa Sh. ngapi? wakasema kila taa 1 ni Sh. 1000/- nikapenda nijue sasa swali langu la msingi, wanajua HATARI iliyo mbele yao kutokana na kufanya biashara kando kando ya bara bara kubwa kama hii ambayo inapitisha magari mengi na hasa mengine yanakuwa yako kwenye mwendo wa kasi! wakasema wanaifahamu ila hawana jinsi wataenda wapi na maisha yenyewe ni magumu!
Kwa kweli nilitoka bila kuwa na jibu sahihi nini hatma yao kama gafla gari likitoka kwenye bara bara na kuwavama. 
Tatizo hili naamini serikali wanaliona ila wanalifumbia macho na pindi ajali itakapo tokea ndio wanafumbua macho na kujua sehemu sio halali, ni vema serikali ikalichukulia hatua mapema kabla halija tokea la kutokea. Tumekua tukiona sehemu mbali mbali ajali zinatokea na kuua watu wengi ambao wapo kando kando ya bara bara kwa hiyo ni vema Serikali ikachukua tahadhari mapema.

             Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
Asante sana.

Tuesday 1 November 2011

Mimba Inavituko au Kujiendekeza????

Wapendwa!!Umeshawahi kukutana na Baadhi ya Wanawake wenye Mimba za Vituko?
Wengine hawapendi kuoga,Kuchana/kusuka Nywele, yaani hawajipendiiii,Wengine wanakula Sabuni,Udongo na Vingi visivyolika na Watu wa kawaida, Wengine Visirani,Jeuri,Matusi,Kususa[Kuzila],Kudeka na ....,Wengine hawalali/Kulala sana,Wavivu,Hawapendi watu hata WAUME ZAO!!.
Wengine wao wanapeta tuu/hawana tatizo, hawana tofauti za Mjamzito na akiwa kawaida, tofauti ni Tumbo tuu Limejazika/kuwa kubwa, wanajiremba /kuwa wasafiiii mpaka wanapo JIFUNGUA!!!


Jee Sababu ni Mimba au Kiejendekeza?
Wewe Mpendwa msomaji ulishapata Mimba ya hivyo au kuwa karibu na Mtu mwenye Mimba ya VITUKO?
Nasikia Wababa wengine wanakimbia nyumba zao kwa sababu ya Mimba za Vituko, au nao Wanatafuta Sababu ya kuondokea tuu? Sasa  wewe uliyempa Mimba unakimbia jee nani amkimbilie/kumsaidia?


KARIBUNI SANA WAUNGWANA KWA MAONI/USHAURI WENU!!!!!





Monday 31 October 2011

COVENTRY NA EID PARTY!!!!!!!!


EID PARTY EID PARTY EID PARTY COVENTRY, U.K.!!!
KARIBUNI SANA WASWAHILI WOTE KATIKA KUSHEHEREKEA EID!!
Party hii ni ya kina MAMA na  WATOTO tuu.


Tarehe  12.11. Itakuwa jumamosi,Itaanza saa 9:00 Mchana [3:00.pm],Mpaka saa 3:00 za Usiku[9:00.pm].

Mahali ni; Moat House Leisure and Neighbourhood Centre,
                  Winston  Avenue,Coventry,Cv2 1EA.

Tiketi zimesha anza kuuzwa!!Wahi Tiketi yako Mapema!!
Bei £5 kwa Mtu mmoja.Watoto chini ya mwaka mmoja wataingia Bure!!Chakula Bure!!Kinywaji 50p.
Pia kutakuwa na michezo  ya Watoto,kama Bouncy Castle na Mingine Mingiiii!!

Kwa Maelezo zaidi na manunuzi ya Tiketi
Wasiliana na;Bi ZAYANA Kwa namba 07889257308.

UKIPATA UJUMBE HUU WAJULISHE NA WENGINE.
KARIBUNI SANA!!!!!!.

Friday 28 October 2011

Mama mkwe Kuvunja Nyumba/Ndoa,ni Mapenzi kwa Mwanawe?Kwani ni Yeye Mama!!

 Wapendwa, hivi kwa nini MAMA MKWE/WAKWE;Hasa  Mama wa MUME.Mara nyingi wanapenda kuiingilia nyumba/Ndoa za watoto wao, Mpaka wengine kufanikiwa kuvunja/kuharibu Mahusiano/Ndoa hizo.Je wanataka mke wanaompenda wao/ kukuchaguli wao au Mapenzi tuu ya Mtoto wake tangu mdogo mpaka Akioa ndiyo yanamfanya aone/waone WIVU?Na JE nini kifanyike ili hali hiyo isitokee?.

Mimi Rachel nasema;Kina mama wakwe watarajiwa na mliokuwa na wakwe tayari,Jamani Taratibu waacheni watoto wajinafasi,Bali pale watakapotaka Ushauri au inapobidi.
Haya nawe Mpenzi Msomaji unalipi la kuongezea au Ushauri,Maoni gani kwa mama Wakwe wa Aina hii?

Karibuni sana Wababa,Wamama,Wanawake na Wanaume,mliokuwa ndani ya ndoa na mliokuwa bado!!!!!!!.

PATA NA BURUDANI YA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAKA; MRISHO MPOTO!.