Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 26 February 2011

Zilipendwa!!!!!!!!

Haya wapendwa vipi mitindo ya zamani  bado inamvuto?.Je wewe  unaikubali, unaweza kuirudia au itabaki kwenye kumbukumbu!!! karibuni sana  waungwana!!!!!!

Monday 21 February 2011

Wanaume na Majukumu!!!!!!!!

Wanaume wanaokaa vijiweni(maskani), wanaocheza bao siku nzima, wanao shinda vilabuni,wapambe na wengine.Je niukosefu wa kazi,mitaji,ubunifu,uvivu,kuchagua kazi au kukimbia Majukumu yao?Wewe msomaji  unamawazo/ushauri gani?.Tuungane pamoja katika kujifunza karibu sana!!!!!!!

Monday 14 February 2011

Watoto na Uhuru!!!!!!!!

Wazazi /Walezi wenzangu.Wewe una  mawazo  gani  kwa watoto chini ya miaka 15,kupewa uhuru wa kusheherekea  siku zao za kuzaliwa na rafiki zao nje ya nyumbani,tena bila ya usimamizi wetu?.Je ndiyo maendeleo,kuwapatia nafasi wajimwage au?Nasubiri mawazo yako ili tujifunze na kuelimishana katika malezi ya watoto wetu, karibuni sana!!!!!!!!!!!!!

Wednesday 9 February 2011

Wanawake na Mitindo!!!!!!!!!!!!!!!!



Haya wapendwa!Mitindo hii wewe unaionaje au ndiyo kwenda na wakati?.
Je mitindo inatakiwa iendane na sehemu usika? Yaani kama kwenye, Harusi,sokoni,bar na kwingineko.
Wewe unamawazo gani na Mitindo ya kina mama//dada? Tuhabarishane  wapendwa!!!!!!!!

Friday 4 February 2011

Jikoni leo ni Makande!!!!!!!!!!!!


Leo ni mwendo wa Makande wapendwa .Wengine wanayaita Pure sijui wewe  unayaitaje!!!! Jee wewe vipi  unayapenda ?na unapenda kushushia na nini chai,juisi,maziwa,maji au?karibuni !!!!.

Sunday 30 January 2011

Wanawake na majukumu!

Wanawake wa zamani na waleo nani wanamajukumu mazito?.Tulinganishe wa vijijini wa leo na wa zamani,
Pia wa mjini  wa leo na wa zamani. Wa mjini  wa leo wana  wafanyakazi wa ndani,mitandao,Elimu na ujuzi mwingi tu,Pia wa vijijini wa leo wana mashine za kusaga  na huduma nyingine. Je wewe mwenzangu unamtazamo gani?

Tuesday 25 January 2011

Wanaume na mitindo!!!!!!!!!


Kumekuwa na mitindo mingi ya wanaume kama,kusuka,kunyoa kipara,kuweka rasta,kuvaa hereni na mingine mingi!jee mitindo hii inaendana na umri wa mtu?