Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label kumbukumbu. Show all posts
Showing posts with label kumbukumbu. Show all posts

Saturday 5 September 2015

Reggae Time ya Pride FM......Justin Kalikawe




Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.

Kwangu
ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa
kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.

Nakumbuka
ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu.
Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times
Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini
Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).

Na nakumbuka tulipanga
kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu
namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika
KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. Ni
katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii
kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine
Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi.
Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate
naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.

Bahati
mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na
aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwisho
wa ushiriki wake katika mkakati huo.

Lakini wakati anafariki,
nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa
zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki
mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.

Lakini….

Justin Kalikawe ni nani?

Saturday 23 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Miaka 50 tangu kuuawa kwa Rais John F Kennedy‏



 

Ijumaa wiki hii,
Marekani imeadhimisha nusu karne tangu kuuawa kwa Rais wa 35 wa taifa
hilo, John F Kennedy aliyeuawa Novemba 22, 1963 alipokuwa akisafiri kwenye gari la wazi jijini Dallas

Rais John F Kennedy akiwa katika gari la wazi muda mchache kabla hajauawa kwa risasi. Pembeni yake ni mkewe na mbele yake ni aliyekuwa Gavana wa Texas John Bowden Connally, Jr.ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo
Kwa wiki nzima, kumekuwa na shughuli mbalimbali kukumbuka tukio hili lililoshitua wengi nchini humo. Mambo mengi yametendeka. Vitabu vipya vimeandikwa na watu wamezungumzia kuuawa kwa Rais huyo pamoja na ufuasi alioacha kwenye uongozi mpaka sasa. Na kama ilivyotegemewa, Kengele ziligongwa, maua yaliwekwa kwenye kaburi, bendera zilipepea nusu mlingoti na nyimbo mbalimbali ziliimbwa

Rais Barak Obama, aliadhimisha kumbukumbu
hizo Jumatano wiki hii kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais
Kennedy na pia kutoa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali akiwemo Rais
mstaafu Bill Clinton, mwanahabari maarufu Oprah Winfrey na wengine 14.

Rais Barack Obama (wa pili kulia) akiwa na mkewe Michelle, Rais mstaafu Bill Clinton (wa tatu kulia) na mkewe Hillary Clinton wakitoa heshima mbele ya kaburi la JFK jumatano wiki hii.


Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 23, 2013




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Tuesday 15 May 2012

Siku kama ya Leo da'Masika na Bw'Jamal,Waliungana na Kuwa Mke na Mume. Burudani: Nitadumu nae!!!!

                                  Nakuvisha/kuvalisha Pete[Pingu] hii..............
                                     Bwana Jamal James Umekubali..............
                                  Mke mkeo kaka J .J
                               Mama Masika katikati, Hongera mama.
                    Mwenyewe da'Masika, Raha jipe Mwenyewe!!!
                                  Mwenye Bw'J.J.Mwakitalu.
                           Shughuli Watu na Watu Walikuwepo.
BIBI na BWANA MWAKITALU.
Na Wamejaaliwa kupata Watoto Wawili
.
Tunawatakia kila lililo jema katika Maisha yenu,Mungu azidi kuwabariki na Ndoa hii Idumu!!!!

Kama una lolote unataka kushiriki nasi, tuma kupitia Email.rasca@hotmail.co.uk
                         Pamoja sana Waungwana.

Sunday 6 November 2011

Trehe:5/11 NI SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU.


Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.



Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.


Habari hii nimetumiwa na Kabipingaz Blog
Asante sana.