Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Utapeli. Show all posts
Showing posts with label Utapeli. Show all posts

Sunday 20 October 2013

TAHADHARI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI; Sasa wanatumia mitandao ya Internet ya Kuomba ajira, TAFADHALI soma taarifa hii usije ukalizwa.



Kuna UTAPELI mpya umeingia Nchini, kuna watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo za kazi huzitangaza kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa.

Matukio yenyewe yanakuwaje: Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai  wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho.

Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.

Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli.

KUWA MAKINI EWE MTANZANIA

IMETOLEWA NA:
MDAU MPENDA HAKI

Thursday 27 October 2011

ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI.






KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.
MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.

HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.

WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.
  
  Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog

Asante sana.