Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Ubatizo. Show all posts
Showing posts with label Ubatizo. Show all posts

Tuesday 7 August 2012

Ubatizo wa da'Charmaine Mungai;Ulifanyika St .Patrick Church Coventry!!!!!!!!

                    da'Farajika [mama mtoto] na da'Charmaine.
             wazazi wa mtoto na wazazi wa kiroho,Mtoto abatizwa!!!!
       Wazazi  na Charmaine Akishangaa duh jamani sinita unguaaa. 
Baba, Mama na Mwana
Wapendwa walioungana na Familia kwenye ibada ya Ubatizo
Zawadi ya Rosary kutoka kwa ma'Mkubwa Stellah
                             Ma'mkubwa Stellah na Charmaine
Da'Tecla[mama wa Ubatizo] da'Farajika[mama mazazi] na Binti yao.MUNGU Awabariki saaaana.
mama na baba wa Ubatizo na Familia ya Mungai
Familia
Kaka Richad na kaka Isaac, watoto kwa mbalii nao walikuwepo
da'Joyce,da'Farajika,da'Stellah ,da'Tecla na mtoto wao!!

Shangazi, da'Tracey,da'Farajika.


Mamazzzz Pamoja sana.
mama totoo na baba totoo na shangazi walikuwepo!!
                                dada Rose na da'Farajika Mbarikiwe sana!!!!
            dada Rose mwenyeweeee, yeye alikuwa anashughulika na misosi[Chakula] Mmmm tulishiba mamaaa,Asante sana.




  Mmmm hizi zinatosha, Jamani mweehh Shughuli za Waswahili kama una Diet usisogee!!!Mmmm Tamu saaana.

Waungwana J'Pili ya tarehe 05/08/12.Familia ya Mungai na da'FarajikaWalimbatiza mtoto wao Charmaine Mungai.

Ubatizo ulifanyika St.Patrick Catholic Church.Coventry U.K.
Baada ya hapo waliungana na Wageni wao Nyumbani kwao kwa Chakula cha Mchana.

Wazazi hao wa Charmaine Wanawashukuru sana Baba na Mama wa Ubatizo. Ndugu, Jamaa, Marafiki woote kwa kuungana nao kwenye siku hii muhimu ya mtoto wao.
Hawana cha kuwalipa bali Wanawaombea kila lililo jema.

Nasi; "Swahili NA Waswahli" Tunamtakia maisha mema na baraka mtoto Charmaine na Wazazi pia.
                                          "Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Friday 30 September 2011

Ubatizo wa da'Arianna,Uliofanyika Tanzania!!!!!!

                             Da'Arianna na mapozzzz.
                    Siku zote uwe Nuruni.
        Shangazi akiwa sambamba na mtoto wake,Hatimaye Arianna anabatizwa.
                          Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina!!
                    Mama Arianna kama anaota vile.
                         Familia pande zote 2, walikuwepo.
                       Familia sambamba na Mpendwa wao.


                 Mashangazi wa Arianna, wapo Makini.
                           Mjomba na Shangazi wakifurahi.
              Nakuaminia  MAHOZA hapo huhitaji msaada.
                 Kula mama mimi penda sana wewe Rafiki yangu.
                      Kula kwa niaba ya baba, mimi penda sana wewe ba'Mdogo.


             Asante sana mama kwa kunisababishia haya , baba yako inakuja hukohuko.
             Arianna mwanangu tumemaliza ehh, Ndiyo mama, yaani nilikuwa naogopa.


Arianna;  Ali BATIZWA katika kanisa la KIANGLIKANI  MAGOMENI,DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.
Baadae walielekea kwenye Sherehe ya kumpongeza kwa UBATIZO na Kufika kwake TZ.


Ujumbe kutoka kwa Wazazi wa Arianna;Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jambo hili na mengi mema aliyotutendea.Pia Tunawashukuru sana Wazazi wetu,Ndugu,Jamaa na Marafiki wote,kwa yote.
Mungu awabariki sana sana.


   :Swahili na Waswahili inakutakia maisha mema da'Arianna na Hongera sana,
    na pole sana huku kucheza kama Bongo sahau, lakini Mchanga unauzwa hata Tesco mwanangu.