Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Balozi. Show all posts
Showing posts with label Balozi. Show all posts

Thursday 3 September 2015

DIASPORA YA MONTGOMERY COUNTY YAMUAGA BALOZI AMINA SALUM ALI




 Bwn. Daniel Korona akisherehesha hafla futi ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Kulia ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa Montgomery County's African Affairs Advisory Group na African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabazo nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa kabisa katika historia ya AU na yeye  kama Balozi kuwezesha Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia Umoja huo.


Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum Ali


Balozi Amina Salum Ali akitoa shukurani zake ambapo leo anaondoka kurudi Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani kazi aliyoifanya tangia 2006.
 Wahudhuriaji 
 Wageni waalikwa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Thursday 6 August 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AONDOKA RASMI MAREKANI KURUDI TANZANIA.


 Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.




                               Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.

 Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.

 Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.

               Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa  pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.

                        Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika hatua za mwisho za usajili.

                           Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika

Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.

Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.

 Kwa pamoja tunasema Safari Njema na Ubarikiwe Sana Balozi Mulamula daima tutakukumbuka.

                    PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

Tuesday 4 August 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATINGA NDANI YA STUDIO YA KILIMANJARO


 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik

 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa