Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 16 January 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;1Samueli22...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu katika yote..

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi

Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mfalme wa Amani, Mungu mwenye nguvu,Mungu wa walio hai,
Mungu mwenye huruma,Baba wa Upendo,Baba wa Yatima..
Mume wa Wajane,Mponyaji,wewe ukisema ndiyo hakuna wakupinga
hakuna jambo gumu lolote mbele zako lisilo wezekana,Jehovah Jireh,Jehovah Rapha,Jehovah Raah,Jehovah Shammah,Jehovah Shalom,
Emanueli-Mungu pamoja nasi...!!


Wastahili sifa, ee Mungu, huko Siyoni, watu watakutimizia wewe ahadi zao, maana wewe wajibu sala zetu. Binadamu wote watakujia wewe. Tunapolemewa na makosa yetu, wewe mwenyewe watusamehe. Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu, waishi katika maskani yako. Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako; mema ya hekalu lako takatifu. Kwa matendo yako makuu watuitikia na kutuokoa, ewe Mungu wa wokovu wetu; wewe ndiwe tumaini la viumbe vyote, duniani kote na mbali baharini. Kwa nguvu yako uliisimika milima mahali pake. Wewe una nguvu mno! Watuliza mshindo wa bahari na wa mawimbi yake, wakomesha ghasia za watu. Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako. Wasababisha furaha kila mahali, toka mashariki hata magharibi. Wewe waitunza nchi kwa kuinyeshea mvua, waijalia rutuba na kuistawisha; mto wako umejaa maji tele, waifanikisha nchi na kuipatia mavuno. Hivi ndivyo uitengenezavyo nchi: Mashamba wayanyeshea mvua kwa wingi, na kuyalowanisha kwa maji; ardhi wailainisha kwa manyunyu, na kuibariki mimea ichipue. Wautunukia mwaka wote mema yako, kila ulipopitia pamejaa fanaka. Mbuga za majani zimejaa mifugo, milima nayo imejaa furaha. Malisho yamejaa kondoo, mabonde yamefunikwa kwa ngano. Kila kitu kinashangilia kwa furaha.


Tazama jana imepita Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine..
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Yahweh tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh tunaomba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Yahweh tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,kwakupigwa kwake sisi tumepona..

Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba utupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji/utendaji
Mungu wetu nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Yahweh tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Yahweh tukawe salama moyoni,Mungu Baba ukatupe macho ya rohoni
Jehovah ukatupe na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh ukatamalaki na kutuatami,Baba wa Mbinguni ukatubariki tuingiapo/tutokapo na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Mungu Baba tunaomba ukavitakase  na ukavifunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo,Mfalme wa amani tunaomba ukatuongoze popote tupitapo
Yahweh na ikajulikane kama upo Baba wa Mbinguni..
Jehovah tunaomba utupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Ukatufanye barua njema Mungu Baba nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..



Enyi watu wote duniani mshangilieni Mungu! Imbeni juu ya utukufu wa jina lake, mtoleeni sifa tukufu! Mwambieni Mungu: “Matendo yako ni ya ajabu mno! Nguvu zako ni kubwa mno hata maadui zako wanajikunyata kwa hofu. Dunia yote inakuabudu; watu wote wanakuimbia sifa!” Njoni mkaone mambo aliyotenda Mungu; ametenda mambo ya kutisha kati ya watu: Aligeuza bahari kuwa nchi kavu, watu wakapita humo kwa miguu; hapo nasi tukashangilia kwa sababu yake. Anatawala milele kwa nguvu yake kuu; macho yake huchungulia mataifa yote. Mwasi yeyote asithubutu kumpinga. Msifuni Mungu wetu, enyi mataifa yote; tangazeni sifa zake zipate kusikika. Yeye ametujalia maisha, wala hakutuacha tuanguke. Umetupima, ee Mungu, umetujaribu kama madini motoni. Umetuacha tunaswe wavuni; umetubebesha taabu nzito. Umewaacha watu watukanyage; tumepitia motoni na majini . Lakini sasa umetuleta kwenye usalama. Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, nilizotamka na kukuahidi mimi mwenyewe nilipokuwa taabuni. Nitakutolea sadaka za kuteketezwa nononono, tambiko za kuteketezwa za kondoo madume; nitatoa sadaka za ng'ombe na mbuzi. Enyi mnaomcha Mungu, njoni nyote mkasikilize, nami nitawasimulieni aliyonitendea. Mimi nilimlilia msaada kwa sauti, sifa zake nikazitamka. Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza. Lakini kweli Mungu amenisikiliza; naam, amesikiliza maneno ya sala yangu. Asifiwe Mungu, maana hakuikataa sala yangu, wala kuondoa fadhili zake kwangu.


Asante Mungu wetu kwa uponyaji wako kwa wapendwa wetu
Asante Mungu Baba wa baraka zako na matendo yako makuu
uliyotutendea,Mungu wetu  umeonekana kwenye maisha ya watoto wako
Yahweh unastahili sifa,Unastahili kuabudiwa,Unastahi kuhimidiwa
Mungu wetu sifa na Utukufu tunakurudishia wewe..!!

Yahweh tunaomba ukaonekane kwenye shida/tabu za wengine wanaopitia magumu/majaribu,Jehovah tunaomba ukawaponye na kuwatendea sawasawa na mapenzi yako..
Mungu wetu ukawape neemaya kujiombea na kufuata njia zako
Yahweh Nuru yako ikaangaze katika maisha yao..
Amani ya Kristo Yesu ikawe nao siku zote za maisha yao..
Kwakuwa ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!

Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwa nami
Mungu mwenye nguvu na baraka aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake,Amani ya Bwana Yesu iwe nayi Daima..
Nawapenda.


Shauli anawaua makuhani

1Daudi aliondoka huko akakimbilia kwenye pango karibu na mji wa Adulamu. Kaka zake na ndugu zake wengine waliposikia kwamba alikuwa hapo, wote walikwenda kuungana naye. 2Watu wote waliokandamizwa au waliokuwa na madeni, au wale ambao hawakuridhika walijumuika na Daudi. Jumla yao ilikuwa watu kama 400, naye akawa kiongozi wao.
3Kutoka huko, Daudi alikwenda mpaka huko Mizpa nchini Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, “Nakuomba, baba yangu na mama yangu wakae hapa22:3 wakae: Makala ya Kiebrania: Watoke. kwako mpaka nijue Mungu atanifanyia nini.” 4Basi, Daudi aliwaacha wazazi wake wakae na mfalme wa Moabu; nao wakakaa kwake muda wote ambao Daudi alikuwa ngomeni. 5Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae hapa ngomeni, ondoka mara moja uende katika nchi ya Yuda.” Basi, Daudi akaondoka, akaenda kwenye msitu wa Herethi.
6Siku moja, Shauli alikuwa Gibea, amekaa chini ya mkwaju, mlimani, huku akiwa na mkuki wake mkononi na watumishi wake walikuwa wamesimama kandokando yake. Basi akaambiwa kwamba Daudi na watu wake wameonekana. 7Naye Shauli akawaambia watumishi wake, “Sasa nyinyi watu wa kabila la Benyamini nisikilizeni, je, mnadhani huyu Daudi mwana wa Yese atampa kila mmoja wenu mashamba na mashamba ya mizabibu? Au je, mnadhani atamfamya kila mmoja wenu kamanda wa maelfu au kamanda wa mamia ya majeshi? 8Kwa nini nyinyi nyote mmekula njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayeniambia habari hii, wakati mwanangu afanyapo mapatano na mtoto wa Yese. Tena, kwa nini hakuna hata mmoja kati yenu anayesikitika au kunieleza kuwa mwanangu mwenyewe anamchochea mtumishi wangu dhidi yangu akinivizia kama ilivyo leo hii?” 9Ndipo Doegi, Mwedomu, ambaye alikuwa amesimama karibu na watumishi wa Shauli akasema, “Nilimwona mwana wa Yese akija Nobu kwa kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu. 10Ahimeleki alimwombea Daudi kwa Mwenyezi-Mungu, akampa chakula na upanga wa yule Mfilisti Goliathi.”
11Mfalme Shauli akaagiza kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu, pamoja na watu wote wa jamaa ya baba yake ambao walikuwa makuhani huko Nobu waitwe. Wote wakamwendea mfalme Shauli. 12Shauli akasema, “Sasa sikiliza wewe mwana wa Ahitubu.” Ahimeleki akamjibu, “Naam, bwana.” 13Shauli akamwambia, “Kwa nini wewe na Daudi mwana wa Yese, mmekula njama dhidi yangu? Kwa nini ulimpatia mikate na upanga, halafu ukamwombea kwa Mungu? Kwa sababu hiyo, leo ameniasi na ananivizia.”
14Ahimeleki akamjibu, “Kati ya watumishi wako, Daudi ndiye ofisa wa kuaminika kuliko wote. Yeye ni mkwe wako wewe mfalme mwenyewe, kapteni wa22:14 kapteni wa: Makala ya Kiebrania: Amegeuka ili. kikosi chako cha ulinzi na anaheshimika kuliko wote nyumbani mwako. 15Leo, sio mara ya kwanza kumwomba Mungu shauri kwa ajili yake.22:15 leo … yake au je, sasa nimefanya uovu leo kwa kumwomba Mungu shauri kwa ajili yake? Sivyo hata kidogo. Mfalme, usinishuku mimi wala mtu yeyote katika jamaa ya baba yangu juu ya njama hizo. Mimi mtumishi wako, sijui lolote, liwe kubwa au dogo juu ya jambo hilo.”
16Lakini mfalme Shauli akamwambia, “Ahimeleki, hakika utauawa, wewe na jamaa yote ya baba yako.” 17Shauli akawaambia walinzi waliokuwa wamesimama kandokando yake, “Geukeni na kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu, maana wao wanapatana na Daudi; walijua kuwa ametukimbia wala hawakuniarifu.” Lakini walinzi hao hawakuinua mikono yao ili kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu. 18Kwa hiyo, mfalme Shauli akamwambia Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Doegi, Mwedomu, akaenda na kuwaua makuhani wote. Siku hiyo, Doegi aliua makuhani themanini na watano ambao huvaa vizibao vya kikuhani vya kitani. 19Kisha aliwaua kwa makali ya upanga wakazi wote wa Nobu, mji wa makuhani, wanaume na wanawake, watoto wadogo na wanyonyao, ng'ombe, punda na kondoo. 20Lakini Abiathari, mmoja wa watoto wa kiume wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, aliponyoka akakimbilia kwa Daudi. 21Abiathari alimweleza Daudi kuwa Shauli amewaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu. 22Naye Daudi akamwambia Abiathari, “Nilijua wazi siku ile nilipomwona Doegi Mwedomu, kuwa atamwambia Shauli. Hivyo, mimi nimesababisha22:22 nimesababisha: Makala ya Kiebrania: Nimegeuka. vifo vya watu wa jamaa ya baba yako. 23Wewe, kaa pamoja nami, wala usiogope. Maana, anayetafuta kuyaangamiza maisha yangu anatafuta hata yako pia. Ukiwa pamoja nami, uko salama kabisa.”


1Samweli22;1-23

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: