Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 15 January 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;1Samueli21...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona..
Si kwa nguvu zetu,wala si kwa ujuzi wetu,si kwamba sisi tumetenda mema sana,si kwa uwezo wetu wala si kwa akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
ni kwa neema/rehema zako Mungu ni kwa mapenzi yako Baba wa Mbinguni..!
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Mungu wetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na tukiwa tayari kwa majukumu yetu..

Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe ee Jehovah,Uabudiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu,Neema yako yatutosha Mungu wetu..!!

Mapigano na ugomvi wote kati yenu vinatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu. Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana kupata vitu, lakini hamvipati; hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu. Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu. Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: “Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa.” Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu.” Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni. Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki! Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa. Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.



Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu Baba..
Yahweh tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote,Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na nguvu  za mpinga Kristo zishindwe katika jina lililo kuu jina la Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo..
Mungu wetu tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..


Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu. Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?

Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Mungu wetu tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji na utendaji Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale kwenye nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Mungu wetu tunaomba Baraka zako Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki,Mungu wetu tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Yahweh ukavibariki na kuvitakasa kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia..
Mungu wetu ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Yahweh tukanene yaliyo yako,Mungu Baba ukaonekane popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni..
Jehovah ukatufanye chombo chema Yahweh tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..


Basi, sasa sikilizeni nyinyi mnaosema: “Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata faida.” Nyinyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Nyinyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena. Mngalipaswa kusema: “Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile.” Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.

Yahweh tunaomba ukawaponye wagonjwa Mungu wetu ukawape uvumilivu/nguvu,imani wanaowaguza,Yahweh tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wenye shida/tabu...
Mungu wetu tunaomba ukawavushe salama wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Baba wa Mbinguni tunaomba ukawalishe wenye njaa,Mungu wetu tunaomba ukawaokoe na kuwaweka huru waliokatika vifungo vya yule mwovu,Mungu wetu tazama walio magerezani pasipo na hatia Yahweh tunaomba ukawatendee na haki ikatendeke..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawe tumaini kwa waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka..
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe na wakaomba/kutubu,Mungu wetu ukaonekane katika maisha yao wote wanaokutafuta na kukuomba kwa bidii na imani..
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapezni yako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwa kuwa nami
Mungu wetu aendelee kuwabariki na msipungukiwe katika mahitaji yenu
Baba wa Mbinguni akawape kama inavyompendeza yeye..
Nawapenda.




Daudi anamkimbia Shauli

1Daudi alikwenda kwa kuhani Ahimeleki huko Nobu. Ahimeleki akatoka kumlaki huku akiwa anatetemeka, akamwuliza, “Kwa nini umekuja hapa peke yako?” 2Daudi akamjibu, “Niko hapa kutokana na amri ya mfalme. Aliniambia nisimweleze mtu yeyote juu ya kile ambacho amenituma. Nimeagana na watu wangu kwamba tukutane mahali fulani. 3Je, una kitu chochote? Nakuomba mikate mitano au chochote kilichoko.” 4Kuhani Ahimeleki akamwambia, “Hapa sina mkate wa kawaida. Ninayo tu ile mikate mitakatifu. Mnaweza kupewa mikate hiyo ikiwa watu wako hawajalala na wanawake hivi karibuni.” 5Daudi akamwambia, “Kwa hakika, daima ninapokwenda kwa ajili ya shughuli maalumu, wanawake wamekuwa mbali nasi! Ikiwa miili ya vijana wangu ni mitakatifu tuwapo kwenye shughuli za kawaida, je, si zaidi katika shughuli hii maalumu?” 6Hivyo kuhani Ahimeleki akampa mikate mitakatifu, kwani hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya kuwekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ikabadilishwa na mikate mipya kutoka mekoni.
7Basi kulikuwa hapo siku hiyo mtumishi mmoja wa Shauli ambaye alikuwa amezuiliwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mtumishi huyo aliitwa Doegi, Mwedomu, msimamizi wa wachungaji wa Shauli.
8Basi, Daudi akamwambia Ahimeleki, “Je, una upanga au mkuki ambao unaweza kunipatia? Kwa kuwa shughuli za mfalme zilinilazimu niondoke haraka, nami niliondoka bila upanga wangu wala silaha nyingine yoyote.”
9Ahimeleki akamjibu, “Ninao ule upanga wa Mfilisti Goliathi uliyemuua kwenye bonde la Ela; uko nyuma ya kizibao cha kuhani umefungwa katika kitambaa. Ikiwa unataka kuuchukua huo basi, uchukue kwani hakuna upanga mwingine hapa.” Daudi akamwambia, “Hakuna upanga mwingine kama huo; nakuomba unipe.”
10Siku hiyo, Daudi alimkimbia Shauli, akaenda kwa mfalme Akishi wa Gathi. 11Watumishi wa mfalme wakamwambia Akishi, “Huyu si Daudi, mfalme wa nchi ya Israeli? Je, si huyu ambaye walikuwa wakiimbiana juu yake katika ngoma, wakisema, ‘Shauli ameua maelfu yake na Daudi ameua makumi elfu yake?’”
12Maneno hayo Daudi hakuweza kuyasahau, akaanza kumwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 13Hivyo, akabadilisha tabia yake, akijifanya mwendawazimu, akawa anakwaruzakwaruza kwenye malango ya mji,21:13 mji: Au ikulu. na mate yake akayaacha yatiririke kwenye ndevu zake.
14Akishi akawaambia watumishi wake, “Mnajua kuwa mtu huyu ni mwendawazimu; kwa nini mmemleta kwangu? 15Je, nawahitaji wendawazimu zaidi? Kwa nini mnaniletea mwendawazimu aje kunisumbua na vitendo vya wendawazimu? Je, mtu huyu ataingia nyumbani kwangu?”


1Samweli21;1-15
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: