Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 28 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 12...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Ni asubuhi nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kuanza majukumu yetu..
Utukuzwe Mungu wetu,Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho..
Alfa na Omega,Mponyaji wetu,Mlinzi wetu,kimbilio letu,Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye huruma,Mungu mwenye kusamehe,Mungu mwenye
kubariki,Mungu akisema ndiyo nani aseme siyo?

Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize? Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua.

Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu...!!

Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,
kwakujua/kutojua Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea...
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote,Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na za mpinga Kristo zishindwe katika jina lipitalo majina yote jina  la Bwana wetu Yesu Kristo..
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba utupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendaji nasi tukatende
sawasawa na mapezni yako..
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Jehovah
nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni ukatupe 
sawasawa na mapenzi yako..

Mfalme wa Amani tunayakabidhi maisha yetu mikononi mwako
Yahweh tunaomba ukabariki na kutuongoza katika nyumba/ndoa zetu
Mungu wetu amani ikatawele na kila mmoja afuate majukumu yake..
Baba wa Mbinguni ukasimamishe na kuziponya Nyumba/ndoa zote zilizokuwa kwenye shida,kutoelewana na kuelekea kuvunjika/zilizovunjika..
Mungu wetu tunaomba ukawaguse wanandoa na ukawape neema ya kujirekebisha,kujua wapi walipokosea,kuomba na kufuata misingi ya ndoa,ukawape neema ya kusamehena na kuchukuliana...

Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ngambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake. Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, “Je, ni halali mume kumpa mkewe talaka?” Yesu akawajibu, “Mose aliwapa maagizo gani?” Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.” Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo. Naye akawaambia, “Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe. Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini.”

Baba wa Mbinguni tunawaweka watoto wetu mikononi mwako Mungu wetu ukawalinde na ukawasimamie katika maisha yao,wakawe na hofu nawe Mungu wetu,wakafuate njia zako amri na sheria zako,ukawalinde katika ujana wao/makuzi yao,wakakue kimwili,kiakili,kimo na kiroho,ukawaokoe na tamaa za dunia hii na wasiionee haya imani yao na wasimamie Neno lako.

Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa. Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia humo.” Kisha akawapokea watoto hao, akawawekea mikono, akawabariki.

Tazama wazazi/walezi wetu Mungu ukawabariki na kuwalinda kimwili na kiroho,ukawatunze katika imani,ukawape amani ya moyo na wakamalizie
wakati wao kwakufuata amri na sheria zako,wakasimamie Neno lako
na kufuata njia zako...
Baba wa Mbinguni ukabariki familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu,Baba ukatulinde sisi na vyote
tunavyovimiliki,Yahweh tuka nene yaliyo yako,tukapate kutambua/kujitambua,Baba ukatamalaki na kutuatamia,Yahweh Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu..
Tukawe barua njema na tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..



Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?” Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Unazijua amri: ‘Usizini, Usiue, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.’” Naye akamjibu, “Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.” Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.” Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi. Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!” Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu! Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, “Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?” Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana.” Petro akamwambia, “Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!” Yesu akasema, “Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa: Nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uhai wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,Baba tunaomba ukawaponye wagonjwa,Yahweh ukawape chakula wenye njaa,Mungu wetu
ukawafungue wote waliokatika vifungo vya yule mwovu,Jehovah ukawasamehe wote waliokwenda kinyume nawe,Baba ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako nazo ziwaweke huru..
Baba tunaomba Amani yako,uponyaji na ulinzi wako na ukawatendee
sawasawa na mapenzi yako..
Ee Baba tunaomba usikie na upokee sala/maombi yetu..


Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” Yesu akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” Wakamjibu, “Uturuhusu kuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.” Yesu akawaambia, “Hamjui mnaomba nini! Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa, au kubatizwa kama nitakavyobatizwa?” Wakamjibu, “Tunaweza.” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli, na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa. Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa.” Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane. Hivyo, Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao. Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkubwa kati yenu, sharti awe mtumishi wenu. Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote. Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa waungwana kwakuwa nami
Baba wa upendo,amani na awe nayi daima..
Nawapenda.


Mzozo kati ya Yeftha na kabila la Efraimu

1Watu wa kabila la Efraimu walikusanyika, wakavuka mto Yordani wakafika huko Zafoni. Kisha wakamwambia Yeftha, “Kwa nini hukutuita tuende pamoja nawe kupigana na Waamoni? Sasa tutaichoma nyumba yako nawe mwenyewe ndani yake.”
2Yeftha akawaambia, “Mimi pamoja na watu wangu tulikuwa na uadui mkubwa na Waamoni. Niliwaombeni mnisaidie lakini hamkuja kuniokoa. 3Nilipoona kwamba hamkuja kuniokoa, nilikwenda, roho mkononi, kupigana na Waamoni, naye Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwangu. Kwa nini sasa mnakuja kupigana na mimi?”
4Basi, Yeftha akakusanya watu wote wa Gileadi, akapigana na watu wa Efraimu. Watu wa Gileadi wakawashinda watu wa Efraimu. Hawa Waefraimu ndio hao waliokuwa wamesema: “Nyinyi watu wa Gileadi ni wakimbizi wa kabila la Efraimu mliotoka katika kabila la Efraimu mkaenda kwa kabila la Manase.” 5Kisha watu wakavishika vivuko vya mto Yordani ili kuiziba njia ya watu wa Efraimu. Kila mara alipotokea mkimbizi akaomba kupita huko, watu wa Gileadi walimwuliza, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Na kama alijibu, “La,” 6walimwambia: “Haya tamka neno ‘Shibolethi’” lakini yeye hutamka “Sibolethi,” kwa sababu hakuweza kulitamka sawasawa. Hapo, walimkamata, wakamuua huko kwenye vivuko vya mto Yordani. Watu 42,000 wa Efraimu walipoteza maisha yao wakati huo. 7Yeftha alikuwa mwamuzi katika Israeli kwa miaka sita. Kisha akafariki, akazikwa huko Gileadi katika mji wake.12:7 katika mji wake: Kadiri ya makala ya kale ya Kigiriki; makala ya Kiebrania: Katika miji ya Gileadi.

Ibzani, Eloni, na Abdoni

8Baada ya Yeftha, Ibzani kutoka Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. 9Yeye alikuwa na watoto wa kiume thelathini na wa kike thelathini. Nao binti zake thelathini aliwaoza nje ya ukoo wake, na wana aliwaoza wasichana thelathini kutoka nje ya ukoo wake. Ibzani alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka saba. 10Akafariki, akazikwa mjini Bethlehemu.
11Baada ya Ibzani, Eloni wa kabila la Zebuluni, akawa mwamuzi wa Israeli kwa miaka kumi. 12Naye akafariki, akazikwa mjini Aiyaloni katika nchi ya kabila la Zebuluni.
13Baada ya Eloni, Abdoni mwana wa Hileli kutoka Pirathoni akawa mwamuzi wa Israeli. 14Yeye alikuwa na watoto wa kiume arubaini na wajukuu thelathini ambao walipanda punda sabini. Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka minane. 15Kisha Abdoni akafariki, akazikwa mjini Pirathoni katika nchi ya kabila la Efraimu kwenye eneo la milima ya Waamaleki.


Waamuzi 12;1-15

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: