Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 24 July 2016

Muendelee na Jumapili nyema;Burudani-Bado Sijafika,Kina Cha Upendo Wako,Twaokolewa kwa Neema - Kijitonyama choir



Wapendwa/Waungwa natumaini Jumapili inaendelea vyema..
Basi muendelee kuwa na Amani,Furaha,Baraka na msipungukiwe na
kila lililojema Mungu awe nanyi daima.






Kuumbwa ulimwengu
1Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. 2Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. 4Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,5mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
   



    Neno La Leo;Mwanzo 1:1-31



6Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” 7Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo. 8Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.





9Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. 10Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.







11Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. 12Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.
14Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka, 15na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo. 16Basi, Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17Mungu akaiweka mianga hiyo angani iiangazie dunia, 18ipate kutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya nne.


20Mungu akasema, “Maji na yatoe makundi ya viumbe hai na ndege waruke angani.” 21Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema.22Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni, muongezeke, muyajaze maji ya bahari; nao ndege waongezeke katika nchi.” 23Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tano.



24Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo. 25Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema.
26Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” 27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. 28Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”


29Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. 30Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo. 31Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita.


Biblia Habari Njema


"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday 17 July 2016

Natumai Jumapili inaishia vyema;Burudani,Bwana Wa Majeshi na Nimesogea.by Paul S.Mwangosina -Sandra-Neema birthday, Shukrani na utukufu kwa Mungu wetu...


Wapendwa/Waungwana natumaini mlikuwa/mnaendelea vyema na Jumapili hii..
Mungu aendelee kuwatunza na kuwalinda, Kiroho na kimwili,Muingiapo na mtokapo,Vilaji na vinywaji, Msipungukiwe na Amani ya moyo,Baraka na Furaha kila iitwapo leo...

Kwetu kuanzia ijumaa mpaka leo tulikuwa na wakati mzuri sana,
15/7 kila mwaka tunaungana na binti yetu mpendwa kwa kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
Ni zawadi iliyo njema  kwetu kutoka kwa Mungu,Tunamshukuru sana Mungu kwa baraka hii
kwenye maisha yetu,"Sandra-Neema" alikuwa baraka tangu alipofika mikononi mwetu na anaendelea kuwa baraka kwetu,Miaka 18 ni mingi na kwa wengine ni dada mkubwa lakini kwetu sisis wazazi kila siku utakuwa mtoto kwetu.

Mungu aendelee kukulinda,kukuongoza katika masomo na maisha yako yote yawe mikononi mwake
kila hatua unayopitia umtangulize Mungu iwe mchana iwe usiku,liwe giza iwe Nuru,kunena na kutenda,Uzidi kukuwa kiroho na kimwili, Uendelee kuwa baraka kwetu kama wazazi, walezi, ndugu,Jamaa , marafiki na jamii pia.Mungu azidi kukuinua katika yote yaliyo mema.

Shukrani;Viongozi wetu katika imani,washarika wenzetu na wote tunaomba pamoja
bila kuchoka katika yote.Mungu aendelee kuwabariki sana kwa kuwa pamoja nasi.
Shukrani;kwa Ndugu,Jamaa,marafiki zetu wote kwa Zawadi na  mchongo wenu kwenye makuzi ya binti yetu na yote,
tunaamini mtoto hulelewa na wengi si wazazi tuu,Mungu awabariki sana na tunawathamini mno.

Ngoja niishie hapa kwa leo Mungu yu mwema sana na tunauona mkono wa Bwana.

"Happy birthday da'Sandra-Neema".



1Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uhai maangavu kama kioo, yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo. 2Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa. 3Hapana kitu chochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo.
Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katika mji huo, na watumishi wake watamwabudu. 4Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao. 5Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.



Neno La Leo;Ufunuo 22: 1-21


Kuja kwa Yesu
6Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
7“Sikiliza! Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki.”
8Mimi Yohane, niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuona, nikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliyenionesha mambo hayo, nikataka kumwabudu. 9Lakini yeye akaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”10Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia. 11Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu.”
12  “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. 13Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.”
14Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.15Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.
16“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
17Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.

Hatima
18Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki.19Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki. 20Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: “Kweli naja upesi.”
Amina. Njoo Bwana Yesu!
21Nawatakieni nyote neema ya Bwana Yesu. Amina.

Biblia Habari Njema 


"Swahili Na Waswahili"Muwe na wakati Mwema.

Sunday 10 July 2016

Jumapili iendelee vyema;Burudani-Glory Come Down,My God is Awesome,BreakEvery Chain





                  Wapendwa /Waungwana nawatakia jumapili njema
                   yenye,Afya Njema,Amani,Upendo,Kweli,Uvumilivu,

                   Hekima,Busara,Tumaini,Furaha,Upolekiasi.
               
                   Mungu aendelee kuwabariki.  




Neno La Leo;Mwanzo 37:4-36



Yosefu na ndugu zake
1Yakobo aliendelea kukaa katika nchi ya Kanaani, alimoishi baba yake kama mgeni. 2Hizi ndizo habari za ukoo wa Yakobo.
Yosefu, akiwa kijana wa umri wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake, wana wa Bilha na Zilpa, wake za baba yake. Yosefu akawa anamjulisha baba yake juu ya tabia mbaya za ndugu zake.
3Israeli alimpenda Yosefu kuliko watoto wake wote kwa sababu alikuwa amezaliwa wakati wa uzee wake. Alimshonea Yosefu kanzu ndefu. 4Lakini ndugu zake walipoona kwamba baba yao alimpenda Yosefu kuliko wao, wakamchukia hata hawakuzungumza naye kwa amani.


Ndoto za Yosefu
5Usiku mmoja, Yosefu aliota ndoto, lakini alipowasimulia ndugu zake, wao wakazidi kumchukia. 6Aliwaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: 7Niliota kuwa sote tulikuwa shambani tukifunga miganda na ghafla mganda wangu ukainuka na kusimama wima. Miganda yenu ikakusanyika kuuzunguka na kuuinamia mganda wangu.” 8Ndugu zake wakamwuliza, “Je, unataka kutuambia kwamba utatutawala? Au utakuwa na mamlaka juu yetu?” Basi, wakazidi kumchukia kwa sababu ya ndoto na maneno yake.
9Kisha Yosefu akaota ndoto nyingine, akawasimulia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine; nimeona jua, mwezi na nyota kumi na moja vinaniinamia.” 10Lakini alipomsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake alimkemea akisema, “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Je, itatulazimu mimi, mama yako na ndugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?” 11Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akawa analifikiria jambo hilo.



Yosefu anauzwa
12Siku moja, ndugu zake Yosefu walikwenda kuchunga wanyama wa baba yao karibu na Shekemu. 13Basi, Israeli akamwambia Yosefu, “Unajua ndugu zako wanachunga wanyama kule Shekemu. Kwa hiyo nataka nikutume kwao.” Yosefu akajibu, “Niko tayari.” 14Baba yake akamwambia, “Nenda ukawaangalie ndugu zako na wanyama kama wako salama, kisha uniletee habari.” Basi, Yakobo akamtuma Yosefu kutoka bonde la Hebroni. Yosefu alipokaribia Shekemu 15mtu mmoja akamkuta akitangatanga mbugani, akamwuliza, “Unatafuta nini?” 16Yosefu akamjibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Tafadhali, niambie mahali wanakochunga wanyama.” 17Yule mtu akamwambia, “Bila shaka wamekwisha ondoka, kwa sababu niliwasikia wakisema kwamba wanakwenda Dothani.” Basi, Yosefu akawafuata ndugu zake, akawakuta huko Dothani. 18Ndugu zake walipomwona akiwa mbali na kabla hajafika karibu, wakafanya mpango wa kumuua. 19Waliambiana, “Tazameni! Yule mwota ndoto anakuja. 20Haya, tumuue na kumtupa ndani ya shimo mojawapo. Baadaye tutasema kwamba ameuawa na mnyama wa porini. Halafu tutaona hizo ndoto zake zitakuwaje.” 21Lakini Reubeni aliposikia maneno hayo, akataka kumwokoa mikononi mwao; basi akawaambia ndugu zake, “Tafadhali, tusimuue. 22Msimwage damu. Ila mtumbukizeni katika shimo hili hapa mbugani, lakini msimdhuru.” Alisema hivyo kusudi aweze kumwokoa Yosefu mikononi mwao, na baadaye amrudishe kwa baba yake. 23Yosefu alipowafikia ndugu zake, wao wakamvua kanzu yake. 24Kisha wakamshika na kumtupa shimoni. Lakini shimo hilo halikuwa na maji.
25Walipoketi kula, wakaona msafara wa Waishmaeli wakisafiri kutoka Gileadi kwenda Misri. Ngamia wao walikuwa wamebeba ubani, zeri na manemane. 26Hapo Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutapata faida gani tukimuua ndugu yetu na kuficha mauaji yake? 27Afadhali tumwuze kwa hawa Waishmaeli, lakini tusiguse maisha yake, kwani yeye ni ndugu yetu; yeye ni damu moja nasi.” Ndugu zake wakakubaliana naye.28Wafanyabiashara Wamidiani walipofika mahali hapo, hao ndugu wakamtoa Yosefu katika shimo, wakamwuza kwa Waishmaeli kwa bei ya vipande ishirini vya fedha; nao wakamchukua Yosefu hadi Misri.
29Basi, Reubeni aliporudi kwenye lile shimo, na asimwone Yosefu tena, akazirarua nguo zake kwa huzuni, 30akawaendea ndugu zake, akawaambia, “Kijana hayupo nami niende wapi?” 31Basi, wakachinja mbuzi, wakaichukua kanzu ya Yosefu na kuichovya katika damu ya huyo mbuzi. 32Kisha wakampelekea baba yao ile kanzu, wakamwambia, “Tumeiokota kanzu hii. Hebu iangalie kama ni ya mwanao, au siyo.”33Baba yao akaitambua hiyo kanzu, akasema, “Ndiyo hasa! Bila shaka mnyama wa porini amemshambulia na kumla. Hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande.” 34Hapo Yakobo akayararua mavazi yake kwa huzuni, akavaa vazi la gunia kiunoni. Akamlilia mwanawe kwa muda wa siku nyingi. 35Watoto wake wa kiume na wa kike wakamjia ili kumfariji, lakini akakataa kufarijiwa, akisema, “Niacheni; nitaendelea kuomboleza kwa ajili ya mwanangu, mpaka nitakaposhuka kuzimu alipo.” Ndivyo baba yake alivyomlilia.
36Wakati huo, kule Misri, wale Wamidiani walimwuza Yosefu kwa mtu aitwaye Potifa, mmoja wa maofisa wa Farao, ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi.Biblia Habari Njema



"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.