Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 21 June 2016

Hotuba ya Maalim Seif Shariff Hamad + maswali na majibu....Washington DC


Photo Credits: Swahilivilla Blog
June 18, 2016, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Maalim
Seif Sharif HamaD alifanya mkutano kuzungumza na waTanzania waishio nje
ya nchi kupitia wale waishio jijini Washington DC.

Hii ilikuwa sehemu ya shughuli zake alipokuwa katika ziara yake ya siku 14 nchini Marekani na Canada.

Ameeleza
mengi kuhusu uchaguzi wa Zanziba, kilichotokea, kilivyotokea na namna
wanavyotafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa, kikatiba na kisheria
uliopo nchini Zanzibar

Karibu umsikilize

Baada ta hapo, wahudhuriaji walipata nafasi ya kuuliza maswali
Karibu uwasikilize

Mahojiano na Makala Jasper kuhusu Tuzo ya National Geographic Society for Leadership



Makala Jasper ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI).

Juni 16, 2016, alitunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, akiwa ni mshindi miongoni ma washiriki 30 kutoka barani Afrika.

Tuzo hiyo imetokana na kazi anayofanya pamoja na wananchi katika Vijiji mbalimbali mkoani Lindi.
MCDI huwezesha wanakijiji kutumia rasilimali za misitu kujenga uchumi na kutunza mazingira.

Katika miradi inayofanyika chini ya MCDI, wananchi wameweza kujiendeleza na kujenga shule, hospitali, kununua chakula cha dharura na kutoa misaada kwa vijiji vingine.

Tuzo ya National Geographic Society/Buffet Award ni ya pili kupokelewa na Bw. Jasper.

Ya kwanza ilikuwa Whitley Fund for Nature Award aliyopokea nchini Uingiereza tarehe 27 Aprili, 2016.

Karibu umsikilize

Sunday 19 June 2016

Jumapili iendelee vyema Na Happy Father's Day;Burudani-Sarah K-Liseme,Nasema Asante Na Ambassadors Of Christ Choir - Moyoni Mwangu,Nimekupata Yesu,




Wapendwa/Waungwana;Natumaini Jumapi ilikuwa/inaendelea vyema,
Mungu azidi kuwalinda na kuwabariki kila iitwapo leo,msipungukiwe na Amani ya moyo,
Upendo,Furaha na Upendo....

"Happy Father's Day" kwa BABA yangu mpendwa Ulale kwa Amani[R.I.P]
Kwa BABA wa watoto wangu na wa BABA wote wanaojua makujukumu yao kama baba
Mungu azidi kuwapa Hekima,Busara,Upendo na utunzaji/Ulezi mwema...

Mungu akawabariki na kuwajaalia wananume wote wanaohitaji watoto
Mungu awape sawa sawa na amapenzi yake....
 Ameeen....










Neno La Leo;waefeso 3:14-21

Upendo wa Kristo
14Kwa sababu hiyo, nampigia magoti Baba, 15aliye asili ya jamaa zote duniani na mbinguni. 16Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalieni kwa uwezo wa Roho wake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu, 17naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Namwomba mpate kuwa na mzizi na msingi katika mapendo 18kusudi muweze kufahamu pamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendo wa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu, kwa kimo na kina. 19Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.
20Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria;21kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina.

Biblia Habari Njema














"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe wote.

Tuesday 14 June 2016

Msemaji wa serikali azungumza na Diaspora.......Jukwaa Langu Juni 13 2016


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga
Photo Credits: Wavuti.com
Katika kipindi hiki, tumezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga ambaye ameeleza kuhusu nafasi na wajibu wa serikali kwa waTanzania waishio Diaspora.
Pia amegusia wajibu wa waTanzania hao kwa nchi yao na kujibu maswali mbalimbali
Karibu


Sunday 12 June 2016

Nawatakia Jumapili iliyo njema;Burudani-William Yilima-Yesu Nitie NguvuNimalize Salama,Ee MUNGU,Uko Wapi,Subiri Muujiza Wako,UmulunguMwinza....



Habari za Jumapili wapendwa/wangwana..
nawatakia jumapili yenye baraka tele...




Neno La Leo;Ufunuo 2:1-29
Ujumbe kwa Efeso







Ujumbe kwa Smurna






Ujumbe kwa Pergamumu








Ujumbe kwa Thuatira





































"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 7 June 2016

Mahojiano na Chef Issa Kapande toka Sweden


Chef Issa ma ma-Chef
 wa timu ya Stockholm, Sweden, waliposhiriki na kushika nafasi ya
kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la
Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  
Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg.
Chef Issa Kapande ni mpishi maarufu na mmiliki wa mgahawa mkubwa unaotoa
huduma za chakula cha Kitanzania nchini Sweden, unaojulikana kama
Tanzania Restaurant
Alikuwa mkarimu sana kujiunga na Mubelwa Bandio kuzungumzia safari yake katika fani ya upishi na mpaka alipofikia.
Karibu ujiunge nasi kusikiliza