Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 27 September 2015

Muwe na Jumapili Njema;Burudani-2015 Ambassadors of Christ Choir-Siku zakilio zimepita,Nimekupata Yesu,kesheni kaombeni,Yanatisha sana na ....(New video 2015)

Wapendwa;Muendelee vyema na jumapili hii,
Amani,Busara,Hekima,Heshima na Utu vikatawale siku zote!!


(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yoh 6:1-14)
13Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini. 14Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.
15Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.” 16Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni nyinyi chakula.” 17Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.” 18Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.” 19Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Neno La Leo;Mathayo14;1-36

Kifo cha Yohane Mbatizaji
(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9
)
Yesu anawapa chakula watu zaidi ya elfu tano
(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yoh 6:1-14)

Yesu anatembea juu ya maji
(Marko 6:45-52; Yoh 6:15-21)
Yesu anaponya wagonjwa kule Genesareti
(Marko 6:53-56)
Bible Society of Tanzania



















Shukrani;Rwanda Tube
"Swahili na Waswahili"Mbarikiwe sana.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Namshukuru Mwenyezi Mungu jumapili yangu ilikuwa njema na yenye upendo...Natumaini hata ww ilikuwa hivyo!!

Rachel Siwa said...

Ilikuwa njema Kadala wa mimi Asante