Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 25 February 2015

Maisha;Ndoa Na Wanandoa-Majuto ni Mjukuu.!!!!!


Kijana Joseph ambaye sasa ni
marehemu,enzi za uhai wake
alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla
ya kuoa.
Baada ya kuoa miaka mitano ya
kwanza akabahatika kuwa na watoto
mapacha wa kike na wa kiume na
mke wake aliishi kwa furaha
akifurahia baraka ambazo Mungu
aliwapa familia ile.
Mke hakuwa na kazi na mme akaona
ni vyema amsaidie kwa kumsajilia
kampuni na mama yule akawa na
kampuni ya mitindo na ikafana sana
na kupata umaarufu katika eneo lile.
Miaka michache baadae baadae mme
akapatwa na matatizo kazini na
kusimamishwa kazi na kwa kuwa
alikuwa daktari basi na leseni yake
ya udaktari ikafungiwa na
hakutakiwa kufanya kazi yoyote.
Mpango huo ulisukwa na wenzake
pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana
kwa utendaji wa kazi zake na
kupinga vitendo vya rushwa.
Maisha yakazidi kuwa mabaya pale
nyumbani kwani miaka ilivyosogea
hakupata tena wala kuliona lile
penzi la mkewe, kwani mke akawa ni
mtu wa kumchukia mmewe mara
mme akihitaji fedha apewe kwa
masimango na mbaya zaidi hata
watoto wakaanza kufundishwa na
mama yao kumchukia baba yao.
Hali ile ilimpa mzee yule wakati
mgumu na ikafikia kipindi akaanza
kudhohofika mwili kwa mawazo
ingawa akajitahidi sana
kutoyaonesha hayo machoni pa
watu na majirani.
Baada ya muda akapatwa na homa
na akawa akijiuguza lakini baada ya
muda akashauriwa aende akapimwe
na kugundulika kuwa alikuwa na
tatizo katika moyo wake
lililosababishwa na msongamano wa
mawazo.
Akamfuata mkewe ofisini kwake na
kumwambia anatatizo la moyo na
ilihitajika apate msaada wa fedha
kiasi cha laki tano (500,000) ili
afanyiwe upasuaji wa haraka na
kujiokoa katika hali hiyo hatarishi
kwa maisha yake.
Mke alimjibu, " Sidhani kama nina
hela ya kuchezea kwa kukupa
mwanaume usiye na faida kwa
familia yako... yaani mpaka chupi
nikununulie mimi?Wanaume
wenzako wanafanya kazi na sio kama
wewe ulivyo sasa"
Baba alinyanyuka na kuufuata
mlango bila ya kusema neno machozi
yakimtoka na akikumbuka jinsi
alivyoijenga familia yake kwa upendo
na amani akiwapa mahitaji yote na
jinsi alivyotumia mpaka tone lake la
mwisho la fedha, muda na hata
jasho kuinyanyua biashara ya mkewe
ambayo ni kwa ajili ya familia.
Akawasha gari na kuondoka kuelekea
nyumbani akiwa na mawazo huku
akiona jinsi mtu umpendaye
anayoweza kubadilika kiasi cha
kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa
huna kazi na kumfananisha na wale
wote.
Huku nyuma mke akaingiwa na roho
ya ubinadamu na na kujilaumu kwa
kauli ile na kuanza kuumia kisha
akajaribu kumpigia simu mzee ikawa
haipokelewi na kumka kuliwasha gari
na kuanza kumfuata mzee
Kilomita chache mbele akaona kuna
mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki
gari na kuuliza kuna nini?
wakamwambia kuna ajali ya gari
kuna mzee alikuwa anataka kuingia
upande wa kushoto bila kuona kama
kuna gari.
Kusogea pale hakuamini kuona mwili
wa mme wake ukiwa umefunikwa
alianza kutokwa na machozi kabla
ya kuingia kwenye gari na kuona
kuna kadi nzuri ikiwa kwenye
bahasha akaifungua na kuisoma.
Kilio kikubwa kilimtoka baada ya
kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni
siku za kuzaliwa ya baba huyo na
hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye
mzee kununua kadi iliyoandkiwa "
NAKUSHUKURU MUNGU KWA
KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA
PAMOJA NA CHANGAMOTO
NINAZOZIPITIA NAAMINI KUNA SOMO
WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI.
UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH
DAY TO ME"
Mama yule aliomboleza na mpaka
sasa anazidi kuomboleza na hana
amani tena hata faida ya ile
biashara haioni tena na hajui nani
atamsamehe.
Je, unapitia mapito gani sasa katika
mahusiano yako?
Je, unayamudu vipi matatizo ya
mahusiano yako?
Je, unafikiria nini kama siku ukiamka
na kuona wewe ndio chanzo cha
kifo, kilema au chanzo msongamano
wa mawazo kwa mwenza wako
kutokana na tabia zako za ubinafsi?
Ndugu una kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa kukupa
mwenza huyo na kuamini kuwa
katika kila mnalolipitia ni jaribu la
kuwafanya muwe na sababu ya
kuonyeshana upendo vyema zaidi ya
ule wa mwanzo;
Nimeumia sana mpaka nimefikiria
sana mahusiano yangu na watu
wanaonizunguka,
kupitia stori hii nimepata somo la
upendo na uvumilivu na kuzishinda
stress za dunia.

"Nimetumiwa na Rafiki nami nikaona ni vyema tusome wote"
 "Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

1 comment:

mumyhery said...


Duh inasikitisha LoL111