Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 26 October 2014

Wapendwa muendelee na Jumapili Vyema;Burudani-Pole wana Congo Uamusho,Wasiwasi mjini, Choir CBCA Bugabo/ Bukavu, RD-CONGO,



Wapendwa;Nawatakia Jumapili Njema yenye ,Amani,Busara,Hekima na Kupendana Kindugu..
Neno La Leo;Warumi:13:1-14

Kupendana kindugu
8Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.9Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” 10Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria.
11Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.12Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga.13Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. 14Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.



"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

No comments: