Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 20 October 2014

Kutoka Sauti Ya Mwanamke;Mke wangu HAFANYI KAZI !!!



Mazungumzo kati ya Mume (M) na mwanasaikolojia (S)
S: Unafanya kazi gani Bw. Bandy?
M: Nafanya kazi kama mtunza fedha benki.
S: Mkeo je?
M: Mke wangu hafanyi kazi, yeye ni mama wa nyumbani tu.
S: Nani anaandaa chai wakati wa asubuhi?
M: Mke wangu anaandaa sababu hafanyi kazi.
S: Mkeo anaamka saa ngapi kuandaa chai?
M: Anaamka mida ya saa 11 asubuhi, anasafisha nyumba kwanza, halafu ndo anatengeneza chai.
S: Watoto wako wanaendaje shule?
M: Mke wangu anawapeleka shule sababu hafanyi kazi.
S: Baada ya kuwapeleka watoto shule, anafanya kazi gani?
M: Akiwaacha shule anaenda sokoni, halafu anaenda nyumbani kupika na kufua, kama unavyofahamu hafanyi kazi.
S: Ukirudi nyumbani jioni kutoka ofisini unafanya nini?
M: Huwa napumzika maana nakuwa nimechoshwa sana na kazi za siku nzima.
S: Wakati huo mkeo huwa anafanya nini?
M: Anakuwa anaandaa chakula cha jioni, anawalisha watoto, ananiandalia chakula, anaosha vyombo, anahakikisha nyumba ni safi halafu anawapeleka watoto kulala.
Kutokana na mazungumzo hayo hapo juu, nani kati ya hawa unadhani anafanya kazi nyingi zaidi?
---
Kazi za kila siku anazofanya mke kuanzia asubuhi hadi usiku sana zinaitwa ‘Mke wangu hafanyi kazi’??
Kuwa mama wa nyumbani hakuhitaji cheti wala cheo, lakini nafasi yake ni muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Ni vyema na busara kila mmoja akaheshimu nafasi ya mwenzie katika kuchangia mahitaji ya kila siku.

Share, Like, Comment, tuwasikie na marafiki zako.
Zaidi;https://www.facebook.com/SautiYaMwanamke?fref=nf

No comments: