Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 19 April 2014

Shukrani/Asanteni Wote na MUNGU awabariki Sana!!!!


Salaam Waungwana;

Tunamshukuru MUNGU mwenyeezi kwa yote.
Tunamshukuru MUNGU kwa maisha ya Mama/Bibi yetu mpendwa Khadija Mgaya Chuma[bibi Mwalimu].
Tunamshukuru MUNGU kwa kufanikisha vyema,Mazishi ya Mpendwa wetu.
Bi Khadija alifariki usiku wa Jumanne na Kuzikwa siku Alhamisi katika Makaburi ya Ilala Mchikichini.Dar.
Mama Kiwinga na Familia yake,Wanawashukuru sana Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani na Wote walioshiriki kwa Michango,Muda,Upendo,Faraja, Sala/Dua na Mengineyo.
MUNGU azidi kuwabariki na kuwaongezea kila lililo jema kwenu.

Wenu Mama Kiwinga
Wa Ilala Sharifu/Shamba.

Asante Sana.


"Swahili Na Waswahili" Tunawashukuru wote katika yote.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole kwa msiba wa bibi yetu Khadija. Naamini Mwenyezi Mungu amewapa nguvu kwa kipindi hiki kigumu. Amina

emu-three said...

Poleni sana , yote ni mapenzi ya mwenyezimungu

Rachel Siwa said...

Asante sana da'Yasinta,MUNGU yu.mwema na tunamshukuru katika yote.

Rachel Siwa said...

Asante sana ndugu wa mimi@emu-three kwa yote.