Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 15 October 2013

Mahojiano na wadau wa darasa la Kiswahili Washington DC‏

Photo Credits: Panafricanvisions.com
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.

Kama
tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania naKenya, na pia
yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi,
Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.

Ikizungumzwa na watu
wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee
ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na
inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani

Na matumizi
yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi
kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na
biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.

Kiswahili sasa
kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia
inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.

Kiswahili
ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na
hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya
waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha
darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.

Na leo,
wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV
(Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha
Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami
katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.

KARIBU UUNGANE NASI

Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Iddi Sandaly akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Bernadeta Kaiza ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Asha Nyang'anyi akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Twawapenda....Tukutane juma lijalo kwa kipindi kingine cha HUYU NA YULE tutakapohojiana na wadau wengine juu ya jambo jingine MUHIMU kwa jamii yetu

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

2 comments:

emu-three said...

Kiswahili chapendwa, lakini wenyewe asili nacho wanakibeza...utasikia mtu anasema `usilete uswahili wako hapa...' ni kutojiamini, ...kasumba ya utumwa imeziteka akili zetu.

Rachel Siwa said...

Asante Ndugu wa mimi@emu-three