Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 11 January 2013

Kisa cha Leo na Mswahili Emu-Three;Uchungu wa Mwana Aujuaye ni Mzazi:46!!!!!



‘Mama aliniambia kuwa siku aliyokutana na huyo mwanaume ambaye almuokoa ilikuwa kama pigo la pili katika maisha yake, maana hakutarajia kabisa kama itakuwa hivyo….’akaendelea kuongea huyo binti akisimulia kisa hiki.

*******

Turejee kidogo pale tulipoishia:

‘Haya sisi tunaondoka, tunashukuru sana kuwa mtoto amepatikana, na …safari ijayo tutakuja mimi na mume wangu,…’akasema malikia.

‘Na naomba mkija mje na huyo mwanaume aliyeniokoa….tafadhali mtafuteni popote alipo, …’akasema mama Maua.

‘Hilo usijali,..tutakuja naye….’akasema malikia huku akitabasamu,….na akafunua mdomo ili kumuelezea ukweli, ….

Lakini malikia alisita kumwambia ukweli je unafahamu ni kwanini, basi tuendelee na kisa hiki ili tujue ni kwanini malikia alisita kuelezea ukweli huo.

********

Wakati huo yule punda aliyempanda malikia akaanza kuondoka. Malikia aligeuka nyuma na kumwangalia yule mwanamke akiwa kasimama pale mlangoni huku akiwa kambeba mtoto wake, akatabasamu.

‘Mume wangu atafurahi sana kuwa hatimaye mtoto yupo mikononi mwa mama yake…’akasema na aliombea akifika huko kwao akute mambo yako shwari, ili safari ijayo warudi hapo pamoja, na kumtembea huyo mama, na ikiwezekana wamchuke wakaishi naye huko kwao msituni.

‘Lakini sheria hazimtaki…..’akasema na kuwaza

‘Sheria gani hizo za kubagua watu…kwani ana kosa gani, na kama ana kosa …hilo kosa hakulifanyia hapo, …hapana lazima hii hali iondolewe’akasema huku wakiendelea na safari ya kurudi kwao msituni. Na wakati wanaingia msituni, akakumbuka nyumbani kwao…..

‘Natamani sana nirudi niwaone ndugu zangu tena..lakinihaiwezekani, najua ipo siku nitarudi…’akasema huku machozi ya kimlenga lenga….

Wakati machozi yakimlenga , wakafika sehemu ambayo anaikumbuka sana, akasimamisha msafara, akaterema kwenye punda wake, na kuusogela ule mti. Akautizama na kuitafuta ile kamba ….huku akikumbuka tukio la siku ile….

Akakumbuka jinsi alivyomkimbia baba yake ….hebu turejee sehemu hiyo kidogo….....

Inaendelea ingia;

Ni Mswahili;Emu-Three na Diary Yangu[Yake!!]

                           

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

No comments: