Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 11 January 2013

Afya na Jamii;Na Mswahili John Haule- Nyama tamu, Inaua!


Historia yake:
Kwa miaka mingi sana nyama imekuwa chakula cha asili kabisa katika nchi yetu. Nyama imekuwa ikiliwa na inaendelea kuliwa na vyakula vya wanga, na hapo ndipo nyama ilikutana na jina jipya la kitoweo. Lakini pia nyama hailiwi tu kwa staili hiyo, nyama pia ilijikuta ikipata jina lingine kwenye mabaa na vilabu vya pombe iliposhushiwa na mafunda ya pombe na kuitwa asusa.
Nyama ni tamu sana. Kuna uhakika wa kitaalamu kabisa unasema nyama ikipikwa au kuchomwa basi utamu na mahitaji yake kiafya mwilini huongezeka mara dufu. Lakini nyama ukiikuta mezani itakutatiza sana kujua hii ni ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, au sungura. Vilevile inawezekana pia hata hisia zako zikawa tena mbali na ukweli maana nyama ipo pia ya porini kama vile pofu, nyati, mbuni, swala, digidigi na wengineo wengi tu, hivyo kuuliza kabla ya kula nyama ni muhimu sana hasa kwa wale wenye miiko na baadhi ya vyakula na waislamu ambao baadhi ya nyama kwao zimeharamishwa. Ila mimi nawaongezea jicho la tatu ndugu zangu hao kuwa IMEHARAMISHWA tu lakini HAIKUKATAZWA kuila kama hutakuwa na jazba kunielewa utagundua hivyo. Na mimi nafikiri leo naziharamisha nyama za aina zote hapa kwa ushahidi wa madhara ya kiafya na kiroho pia.
Mungu pia hapendi nyama:
Kama mtakumbuka mliosoma Biblia, Wajukuu wa Mungu Kaini na Abeli walijikuta siku moja wakimtolea babu yao sadaka. Kaini akiwa kama mfugaji alichinja akamletea Mungu nyama. Mungu alikataa na sadaka yake haikuteketea! Lakini Abeli akiwa kama mkulima yeye alileta mazao ya shamba lake. Mungu alipokea! Ikawa Kaini akamwuua nduguye Abeli na kizazi cha wafugaji kikajimegea dhambi ile mpaka leo.
Nyama inajenga matabaka:
Enzi zetu za kujisomea hapa nchini kila nyumba ilikuwa na “Book Shelf” Leo zipo wapi? Sisi tulisoma kitabu kilichoitwa UPUMBAVU WA MWAFRIKA na ndani kulikuwa na hadithi nyingi tamu ikiwemo “Uchu wa Mzee Mikidadi” ambayo tulipoisoma tulielewa kuwa nyama ina nguvu ya kuwagawa watu kimatabaka kwa uchu tu wa wenye madaraka, ukiachilia mbali madhara makubwa zaidi ya kiafya.
Uharamu wa nyama umeifanya jamii iwatenge wanyonge na kuwakweza wenye nguvu na mamlaka katika kila Nyanja ya maisha. Angalia, Katika vitoweo vyote nchini na duniani hakuna ambacho ni ghali kama nyama. Wanakula wenye pesa tu. Wapo akina mama wa kambo walioripotiwa kuwalisha nyama watoto wao na kuwalisha maharage wale watoto wa kambo. Katika jamii yoyote wenye mamlaka na nguvu ndio wanao faidi nyama huku wengine wakiambulia mchuzi na mifupa. Ukiandaa sherehe usipoleta nyama watu watakuwa hawakuelewi kabisa toka miguuni hadi utosini. Nyumba Fulani Fulani nyama hupakuliwa na mama. Mboga za aina nyingine ni ruksa yeyote kujipakulia. Wengine wameripotiwa kuwahesabia finyango za nyama wake zao. Wapo pia wanawake waliopewa nyama kilo moja wapike ikafika mezani robo kilo tu, lakini watu watakuambia wapo wanaume wanaokula kilo ya nyama wakiwa baa na huku mke na watoto wanalalia uji. Huku utasikia mtoto kachomwa mikono kisa eti kadokoa nyama, na mikasa kadha wa kadha inayotutahadharisha kuwa nyama itatutoa roho!
Nyama inaua:
Lakini umeona jinsi tulivyoiangalia nyama kwa historian a taswira tu bila kuiangalia madhara yake kiafya ambayo ni lukuki kiasi hayaorodhesheki hapa leo. Nyama inatakiwa iliwe kwa dharura tu na sio kama mlo kamili kwa kuwa nyama ina rekodi ya kuua walaji wake kimya kimya bila wao kujijua kama wanateketea. Mfano watu mia waliokula nyama kilo moja kila mtu kwa siku, watu 30 walikufa baada ya miaka kumi na kuwaacha wengine taabani kwa magonjwa ya moyo kama kisukari, BP, kupooza, ganzi n.k. Si hayo tu, bali magonjwa ya ini, figo na mapafu yalisababisha vifo pia.
Unapokula nyama unaongeza lehemu na mafuta yabisi mwilini ambayo hupenya na kuingia katika mishipa ya damu na kuganda katika kuta zake. Kadiri mgando unavyoongezeka ndivyo njia ya damu inavyopungua na mwisho kuziba kabisa! Sumu hizo zinapoanza kuganda mgonjwa ataanza kuhisi matatizo na akipimwa atakuta mapigo ya moyo yamefeli yaani BP. Kadiri atakavyoendelea kula nyama na kuziba mishipa basi siku moja damu itapita kwa shida sana na ataanza kusikia ganzi sehemu zote zisizopata damu. Mwisho mishipa ikiziba kabisa ndio huwa tunaita mtu amepooza. Maana hakuna damu inayoenda huko tena! Dawa za wagonjwa hawa ni kitunguu swaumu na mafuta ya Sardine toka Ueskimo tu. Kitunguu swaumu niliwahi kukiongelea na nafikiri walionisikia wanaelewa cha kufanya. Ila haya mafuta ya Sardine toka Ueskimo nitayaongelea siku nyingine.
Nyama inadhuru kisaikolojia pia:
Watu wa jamii za wafugaji na walaji wakubwa wa nyama kwa ujumla ni wakorofi sana. Ni waoga na wanaweza wakakudhuru bila kuwa na sababu za kutosha. Hawa jamaa wanaamini kuwa kama huna silaha basi wewe si mwanaume. Hii imetokana na kujilundikia kiasi kikubwa cha lehemu na sumu nyingine toka katika ulaji wa nyama uliokithiri. Hupenda kulala wakiweka silaha kwenye mto ili wajiridhishe kuwa wanalala salama. Kama ni hohehahe ataweka sime hata kisu tu, wakati mwenye pesa ataweka bastola kabisa. Cha kukuchekesha msomaji wangu leo ni kuwa watu hao nchini tumewapa “kibali baridi” cha kutembea na silaha popote! Kama huamini toka wewe na jambia lako mkononi kama utafika popote kabla polisi na watu wa usalama hawajakukamata. Utakamatwa kwa sababu si sheria kutembea na silaha hadharani wote tunalijua hili, lakini hawa ndugu zetu asili yetu imewakubali watembee hata na mikuki na hatuwaulizi kulikoni.
Ikaja pia staili mpya ya kuwaajiri kazi za ulinzi baadhi ya wala nyama hawa. Wenye akili zetu tulibaki midomo wazi tukiamini staili hii itakufa siku si nyingi baada ya wanaowaajiri kukutana na hasara ya kuibiwa kila kukicha. Na kweli leo hii wamesahaulika… Mtu mwenye kiasi kikubwa cha lehemu mwilini ni mwoga, hajiamini, na vitu kama hivyo kwa kuwa damu haitembei ipasavyo. Sasa mtu mwoga atalindaje wakati yeye mwenyewe hajiamini na anatembea na silaha lundo! Yatakuwa maajabu sana.
Madhara ziada ya nyama:
Lakini madhara ya nyama bado hayaishi kama nilivyodokeza hapo awali. Kuna hili ambalo sitaliacha. Ng’ombe, mbuzi, kondoo na mifugo mingine huwa wanakula chochote kitamu kwao wanachokiona ardhini sote tunajua. Lakini tumeshuhudia wanyama hao wakila nailoni, misumari, nywele bandia, na sumu nyingine nyingi tu tunazozalisha binadamu. Sumu hizi tunakutana nazo tunapokula nyama na hakika zinatudhuru vilivyo. Haya, Wanyama hao hao huwa tunawapeleka josho kuua wadudu mwilini. Sumu ya zile dawa ni lazima ukutane nazo ukila nyama. Unalijua hilo? Wachilia mbali sumu hizo, wanyama hupewa dawa wanapopatwa na maradhi tena dawa kali (antibiotics) ambazo utazila na nyama na hatari yake ni kukujengea usugu dhidi ya dawa za kibinadamu pale utakapougua. Ni hatari sana.
Kwa mila na desturi zetu watanzania tuna nunua nyama pale buchani. Utakuta gogo moja limevilia damu na ndilo linalotumika kukatakata nyama. Pale utajiuliza kwanza usalama wa nyama juu ya lile gogo upoje maana hujui ni mti gani, una kamikali gani, zinaua au ni salama na maswali mengine lukuki. Lakini ukimwuliza muuza nyama hatakupa jibu lolote la kukuridhisha pale. Hajui. Upo mtaa Fulani wanaume walikuwa wafanyakazi wa reli ambao walikuwa wakila nyama kwa wingi kuliko wake na watoto wao. Leo hii mtaa hauna baba wote wamefariki. Kwa niaba ya watanzania wote naishauri wizara ya afya kupitia mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kufunga misumeno ya kukatia nyama katika mabucha ya nyama maana ndio utaratibu duniani kote na ndio ustaarabu. Vinginevyo kuna watu wanakufa kimya kimya.
Bado tu nyama inaonekana ina maambukizi dhidi ya maradhi zaidi kuliko mboga za majani, matunda na nafaka. Nyama hubeba wadudu wanaojulikana na wasiojulikana kila unapoila kuja kukuambukiza maradhi ya aina mbalimbali.
Nile ua nisile nyama?
Lakini, nyama bado ina utetezi wa kutosha kuwa na faida za kiafya. Msomaji wangu ona nyama jinsi ilivyo shetani maana haieleweki kama tule, au tusile. Nyama hasa nyekundu ni muhimu sana kwa afya yako lakini, inakubidi ule kidogo sana kama finyango tatu tu kwa wiki, hiyo ni kitaalamu. Ukiifanya mlo rasmi utakufa! Cha ajabu wakati vyakula vingine vikipikwa hupoteza ladha na uthamani wake, kwa nyama mambo ni tofauti kabisa maana ikipikwa, ikichomwa, ikikaangwa ikiokwa nk ladha huwa tamu ajabu na uthamani wake mwilini huongezeka mara dufu. Ukila nyama unajipatia madini ya chuma, zinki, na protini kwa wingi mno.
Wengi wa wagonjwa walioshindwa vitandani wanahitaji sana chuma, zinki na protini kuamka na kupona haraka. Chuma humsaidia mtu kuwa na kinga dhidi ya maradhi sasa kama hukupata virutubisho vya madini hayo basi unaweza kufa hapo kitandani kwa kuwa hukula nyama mpaka chuma imeisha mwilini, hivyo usubiri ugonjwa utakaofuata Anemia na baadaye kaburini. Mgonjwa huyu utamjua kwa dalili hizi: Kapoteza uzito, ngozi imemkauka, mapigo yake ya moyo yanaenda mbio au taratibu sana, Hana pumzi, kifua kinambana, kizunguzungu, hakumbuki tena kitu, kichwa kinamuuma lakini sio malaria, miguu na mikono imekufa ganzi nk.
Usipokula nyama pia tumesema utakosa madini ya zinki. Zinki pia ni kiboko kukupa kinga ya mwili upambane na maradhi sasa kama hamna lazima maradhi yakulaze kitandani. Wanandugu mpeni virutubisho vya zinki kabla hamjampoteza ndugu yenu. Mkitaka kumjua kuwa anahitaji zinki angalieni yafuatayo: Mgonjwa hana utulivu na usiku hapati usingizi, kama ana vidonda haviponi, ana vidoadoa au alama ya nusu mwezi katika kucha zake vidoleni, anakosa nguvu nk. Ukiona dalili hizo hebu wahi umpe virutubisho vya zinki apone vinginevyo mtamkosa.
Lakini pia usipokula nyama unajikosesha protini. Protini ikipungua mwilini utaona mgonjwa anapata tabu kupona vidonda, analalamika viganja vinawaka moto, analalamika miguu inamuuma na muda mwingine atasema tumbo pia linamuuma mara kwa mara, hana nguvu, anashambuliwa na maradhi ya ngozi na wengine hukonda vibaya.
NATIVA ni suluhu:
Hapa Tanzania kuna virutubisho vya kurejesha afya ya mgonjwa huyo haraka na salama. Makampuni mengi yapo kiushindani katika biashara hiyo kila mtu akikushauri kutumia zake. Mimi kwa uzoefu wa maradhi haya nakuelekeza msomaji wangu tumia virutubisho vya kampuni ya NATIVA toka Afrika Kusini kama unatafuta suluhu ya uhakika na haraka kwa mgonjwa wako. Nativa wapo mji mzima na ukihitaji dawa nipigie tu simu nitakusaidia kuzipata.
Wapo wakulima ambao si wafugaji nap engine kupata nyama si kitu rahisi. Kizazi cha Abeli yaani Wakulima wao madini ya chuma, zinki na protini wamejaziwa kwenye mazao yao hivyo utavipata vitu hivi ukila mboga za majani, karanga na jamii yote ya njugu, maharage na jamii zake, matunda kwa wingi nk. Hivyo hakuna sababu ya kungoja upungukiwe na madini hayo mwilini.
Kula nyama msomaji wangu. Lakini usiigeuze kuwa mlo rasmi, kula kama waislamu walivyoambiwa katika msaafu kuwa nguruwe ni haramu aliwe kwa dharura tu. Lakini mimi leo nakuambia wewe kula nyama yoyote kwa dharura tu. Kama Mungu alimkatalia mjukuu wake Kaini sadaka ya nyama aliyomtolea jiulize nyama ina nini?
Bwana pori mmoja alisema hivi: Baba anayekula nyama kwa wingi anajijengea uhayawani wa ndege na wanyama wanaowala wenzao (predetors) msituni. Na ndio maana huwa baba wa aina hii huzinyanyasa familia zao…
Kama umekula nyama kwa muda mrefu na unajihisi dalili zilizopo hapo juu tafadhali tuwasiliane nikusaidie. Kama una mgonjwa wa kisukari, kupooza, presha zote, kupungua na kuzidi uzito pamoja na dalili za maradhi kwa kukosa madini kama nilivyoorodhesha hapo awali basi usisite kunitafuta ili nikupe dawa za uhakika upone.
Asanteni sana kwa kunisoma na mungu awabariki sana.

            "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.  

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nimerudi Kachiki nikitengamaa nitasema zaidi..nimeipenda picha yako hapo juu:-)

Rachel Siwa said...

Wawo wawooooo "Kadala" Tunashukuru kwa kurudi salama!!!!Sande bhehhh..

Nilikumithiiii...ukisha pumzika na ukiwa nyumbani nitumie sms!! nikupigie tulongane......

Wasalimie woote hapo Nyumbani na msimalize hizo thawadiiii

Anonymous said...

nashukuru sana kwa ujumbe wako mzuri sana ulotuandikia hapa kuhusu madhara ya nyama.

Ila kwa ufahamu wangu mdogo wa biblia nadhani hapo umechanganya kdogo ebu karudie tena kusoma kipengele kile cha Kaini na Abeli, sadaka ya Abeli ilikua ya nyama na ya Kaini ilikua ya mazao, kwa kumbkmbu zangu Kaini altoa masalia ya mazao yake lkn Abeli alitoa uzao wa kwanza wa wanyama wake tena alitafuta walionona sana na sadaka yake ilikubaliwa moja kwa moja lkn ya Kaini ilikataliwa sababu alitoa kwa kinyongo na dharau.......

ni kweli nyama ina madhara kama ulivotueleza lkn kwa hapo kwny bible naomba urudie tena pls ni ktk kukumbushana tu.

Asante sana na kazi njema