Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 1 January 2013

Afya na Jamii; na MSwahili John Haule-Panda maua yafukuzayo Mbu!


Panda maua yafukuzayo Mbu!

Msimu wa mvua unakuja. Hauji kimya kimya. Ni lazima unakuja na maambukizi makubwa ya malaria yatokanayo na madimbwi yanayozalisha mbu kwa wingi zaidi na mbaya sana mbu jike wa anofelesi huzaliwa wengi pia. Mbu hawa ndio vinara wa kuwaambukiza watu malaria na habari mbaya zaidi nilizonazo mkononi nikuwa wanawake hasa wajawazito ndio waathirika wakuu wa maambukizi ya ugonjwa huu kwa vile huzalisha hewa ya karboni nyingi kuliko wanaume na hivyo kuwavutia mbu hawa ambao wanaambukiza malaria kuwafuata na kuwadunga. Hii ndio siri ya foleni ndefu za akina mama na watoto mahospitalini.
Mbu hawa wapoje?
·        Wana rangi ya kahawia. Akitua katika mwili wako hutega tumbo lake kubwa juu kwa nyuzi 45 na kuleta miguu yake ya nyuma kuwa stendi za kubeba uzito wa damu atakayo kudunga!
·        Huweza kunusa binadamu alipo toka umbali wa mita 50!

Ni kawaida ya msimu wa mvua kuja na hali ya joto inayowavutia watu wengi kutoka nje na kupunga upepo usiku ambao ndio muda muafaka mbu hao kundunga na kuambukiza watu malaria kwa mujibu wa wataalamu. Rumours Africa tumetafiti namna bora ya kuwafukuza mbu toka katika maeneo yote ya nyumba yako, ofisi, hoteli, shule, hospitali, kiwanda na sehemu zingine za kazi ambazo watu hukaa usiku hasa mabaa yanayokesha ambayo pia ni wazalishaji wakubwa wa wagonjwa wa malaria.

Maua yafukuzayo Mbu?
Njia hiyo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizotugharimu mno kuokoa maisha ya watanzania ni kupanda maua yenye harufu na rangi zinazofukuza mbu kama vile rosemary, cintronella, mchaichai n.k.
Tulitafiti pia ni jinsi gani watanzania watazipata mbegu hizi za maua kwa urahisi lakini tukagundua kuwa ni sehemu chache sana wanazoishi watu wenye uelewa hasa wazungu ndio hupanda maua haya bila kuwaambia wengine  na kuwaacha watanzania wengine wapande maua kama urembo tu badala ya dawa na vyakula, na hivyo kujikuta wakipata wakati mgumu kupambana na malaria.

Kwa sasa bado tunafanya mpango wa kutafuta wadau wa kuwekeza kuanzisha bustani ya maua hayo ili tupate mbegu kusaidia watu lakini kwa mwenye haraka zake kujikinga na malaria ni gharama kidogo maana itabidi kusafiri mpaka Peramiho Mission au Uwemba Mission ambako nimeyaona kwa macho mashamba yanayozalisha maua yakiwemo hayo na kusafirishwa ulaya. Pengine labda niliwahi sikia tu kuwa hata Arusha pia kuna mashamba ya maua pia lakini upatikanaji wake kwa kweli siujui.

Maua haya hatimaye yatasambaa. Kila mtu nahisi angependa kupanda maua yenye maana halisi katika maisha na hasa kumlinda yeye, familia, wafanyakazi na wateja pia. Hivyo yeyote ambaye amevutiwa na habari hii na angependa kushiriki kwa namna yoyote kuwekeza katika fursa hii muhimu na adimu kwa taifa letu basi angewasiliana na rumoursafrica kupitia simu namba 0768215956 au email rumoursafrica@gmail.com.

Ujumbe huu unaweza kuwa muhimu kwako, lakini unaweza kuwa muhimu kwa wengine pia hivyo ningekuomba msomaji wangu uufikishe ujumbe huu kwa wapendwa wako ukisisitiza umuhimu wa kujikinga na malaria.

Asanteni kwa kunisoma.

John Haule ni mpelelezi binafsi (Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com


         "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

1 comment:

Anonymous said...

Tutapanda maua ya saa nne yanachanua nayo dawa ya mbu?