Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 26 August 2012

Mswahili Wetu Leo;AIKAROSE MWASHA-Anaishi BELGIUM;NYOTA TUMAINI LETU!!!

NYOTA TUMAINI LETU





Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia:Kike
Miaka:12
Utaifa:TANZANIA
Mchezo: Taekwando 
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
MAKAZI: Leuven Belgium
MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA & DHAHABU


Kijana wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa  miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde Brussels Belgium tarehe  27 May 2012.
Sasa hivi anajiandaa na team yake kwenda Copenhagen kwenye  mashindano ya Wonderfull Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao.
Wito wake hasa kwa vijana wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA.
VIPAJI HUINUA TAIFA

"Swahili NA Waswahili" Tunakutakia kila la kheri.

3 comments:

www.nunuatokahollandwax.blogspot.com said...

Go AIKA , May u reach ur dream.waswahili tunasema, nyota njema huonekana asubuhi.

Yasinta Ngonyani said...

Kila la kheri hakuna kisichowezekana.

emuthree said...

Afadhali, angalau tunaweza kupata medali, na ww ndugu wa mimi kwanini usiwanie moja ya michezo, hata kuogelea sio mbaya, au kupigana miereka, ......