Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Saturday, 18 August 2012

MASHUJAA MUSICA NA RATIBA YAO YA SIKUKUU YA IDD EL FITR!!!!!


Martin Sospeter Luhangisa, Meneja wa Mashujaa Bendi
BAADA ya kukamilisha ziara ya kutambulisha wanamuziki wake wapya wa Mashujaa Band, sasa ni zamu ya kuwapa burudani wapenzi wa bendi hiyo kwa siku ya Idd Mosi na Idd Pili.
Meneja wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd mosi watakuwa Msasani kwenye ukumbi wa Emirates.
Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd pili watakuwa Mjini Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Bendi hiyo ambayo hivi sasa ipo hivi chini ya Rais wake Chalz Baba, itatoa burudani hiyo kwa ajili ya kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa nyimbo zao na Bendi yao kwa ujumla.
Alisema, pia kwa wale wanaoisikia Bendi ya Mashujaa kwenye vyombo vya Habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo laivu katika Sherehe za Eid El Fitri.
"Kama tulivyowapagawisha wakazi wa Songea na Mbeya wiki iliyopita, sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mtwara," alisema Sospeter.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Nawatakieni mafanikio mema....