Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 30 July 2012

GERRY TEGETE, NGASA WASHEREHEKEA UBINGWA PAMOJA NDANI YA WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE.!!!!!!


Mwanamuziki nguli wa Bendi ya Mashujaa Musica Chaz Baba akiimba kwa furaha kubwa ndani ya Ukumbi wa White House Kimara Korogwe usiku wa kuamkia leo.

Kutoka kulia Chaz Baba, Mrisho Ngasa Mchezaji wa Azam na Gerry Tegete Mchezaji wa Yanga wakiwa ndani ya viunga vya White House Kimara Korogwe jana baada ya kutoka kwenye Mechi kali baina ya timu zao, ya kombe la Kagame ambayo Yanga waliibuka mabingwa kwa mabao 2 kwa bila.

Kulia Gerry Tegete akishoo luv na Mchezaji mwenzake Mrisho Ngassa anayechezea club ya Azam.

Rapa maarufu wa Bendi ya Mashujaa Fagasoni akiimba ndani ya ukumbi wa White house Kimara Korogwe.


Mpiga tumba namba moja Afrika mashariki MCD akiwakimbiza washabiki wao ndani ya White house Kimara.

Mrisho Ngassa na Chaz Baba wakifurahia kwa pamoja Ushindi waYanga, Mrisho ngassa ni Mshambuliaji mahiri wa Club ya Azam.

Tegete, Henry na kulia Mrisho Ngassa ndani ya White House Kimara.

 kulikulikuwa na mechi ya fainali ya kombe la Kagame kati ya Yanga afrikani na Azam FC ndani ya uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliibuka mabingwa

Ngassa na Tegete kwa kuonyesha mpira sio ugomvi walisherehekea pamoja ushindi wa Yanga baada ya mechi katika viwanja vya White House Kimara korogwe wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatumbuiza

1 comment:

Giancarlo said...

Felice inizio settimana a te...ciao