Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Saturday, 5 May 2012

SHIME TUSHIRIKIANE KUMSAIDIA MWENZETU;WIMBO,TANZANIA ALL STAR- MBONI YANGU.


Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake. Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.
Wimbo huu unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu umerekodiwa kuhamasisha na kumchangia Sajuki. Kutoa ni moyo bado hujachelewa. Unaweza kutuma mchango wako kupitia AKIBA BANK A/C # 050000003047 A/C ni ya mke wake Sajuki, Wastara Juma au unaweza kutuma kupitia M PESA 0762189592.

Mimi na wewe tunahitajika katika hili.

Habari zaidi na Picha,utazipata. http://www.jestina-george.com

Sajuki na Mke wake Wastara.
Sajuki alivyokuwa na Alivyo sasa.


Pole sana utapona tuu.

Pamoja waungwana.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kweli kutoa ni moyo!! bahati mbaya sijaweza kusikiliza huo wimbo kwani ni peusi tu sijui ni usamba wangu au?

Rachel siwa Isaac said...

Jaribu tena dada Yasinta,Wimbo unaujumbe mzuri sana.

Yasinta Ngonyani said...

Nimeweza ni kweli ni ujumbe mzuri sana na halafu umeshakaa kichwani mwangu nauimba utafikiri ndo niliutunga...Ahsante