Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 21 May 2012

Jikoni Leo. Mswahili; da'Sophi na Tupike Pamoja!!! Angalia Video!!!!
Karibuni "tupikepamoja.com"


Habari utakazo zipata katika tovuti hii ni picha za video na maelezo ya kina kuhusu namna ya kupika mapishi na vyakula vizuri vya kimataifa muhimu zaidi ni rahisi kupika.
Tovuti hii ni kwa ajili ya watu wanaopenda kupika, kujaribu vyakula vipya na ladha mpya ili kuwashangaza rafiki na familia zao kwa ladha hizo. Maelekezo ya mapishi utakayopata hapa ni kwa ajili ya meza kuu ingawa wakati mwingine tunashirikiana nawe katika vinywaji na viburudisho (deserts & sweets).
kwa kuanzia ni matumaini yetu utafurahia kupika kama sisi.
Pia usisahau kututumia maoni yako, maswali na ujumbe tuweze kuboresha na kutimiza mahitaji yako, Asante kwa ushirikiano wako
Furahia chakula chako!

Kujua zaidi Mtembelee.www.tupikepamoja.com
Haya Waungwana Mambo hayo kazi kwenu na "Tupike Pamoja"

Hongera da'Sophi kazi nzuri.

3 comments:

ray njau said...

Kupika?
Kaazi saaaaaaana!!
Kula ni raha saaaaaana.
Jumatatu njema kwa wadau wote.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante!! tutafuatilia kwani kila wakati ni vizuri kujifunza mapishi mapya.

Rachel siwa Isaac said...

Pamoja kaka Ray na da'Yasinta.Mwaka huu tutajua kupika vingi tuu!!!