Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 27 March 2012

Jikoni Leo-Ni kwa Mama Mwakitalu!!!Pata na Burudani ya Ngoma!!!!![Mwanamke jiko au Mwaume Jiko?]



Da'Masika/mama Mwakitalu
Mboga za Majani Mchanganyiko,Majani ya Kunde na Majani ya Maboga
Mchuzi wa Samaki Umeungwa/wekwa Nazi na nyanyachungu

Maandaziiiiii na hapo chini ni Mahindi ya Kuchemsha.

Haya Waungwa,vipi wewe unapenda kupika?au Unapika kwasababu ni lazima upike na ule?Kwenye kazi za Nyumbani kila mmoja kuna kazi anapenda kuifanya, Na kuna baadhi ya Kazi hatuzipendi,Lakini tunafanya kwa sababu ni lazima zifanywe,Na utasikia duuh yule kaka/dada au Mama/Baba anajua Kupika sana,Hivi kujua kupika ni Chakula kiive au?
Kwani Utamu/Radha ya chakula wewe unaweza kupendezwa nacho na mwingine asipendezwe nacho.
Jee Kazi/Ujuzi wa Kupika ni kwa Wanawake tuu?Kwani mara nyingi utasikia Mwanamke jiko na si Mwanaume Jiko,Hasa kwa Maisha ya Leo,
 kwa Maisha ya Zamani wengi wao Mama/Dada kazi yao kubwa ni Upishi na Baba wengi ndiyo walikuwa wanafanya Kazi hasa Mijini, Kwa Vijijini Woote BABA na MAMA Wanaenda shambani lakini Kupika ni MAMA.Jee Leo Tunaweza Thubutu kusema MWANAUME JIKO? AU TUTAKUA TUMEWADHALILISHA?Kwani wapo Wanakarangiza haswaaaa kutushinda au Hamjakutana nao?.


Karibuni Waumgwana kwa Mawazo na Kuelimisha na Kwa upendo.

5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Wanaume pia wanajua sana kupika ila wanapenda kufanya kazi hii kama KAZI ya kuwaingizia kipato na sio wajibu nyumbani.

Wanaume wana mambo!!.....

Yasinta Ngonyani said...

Wewe bwana yaani huachi kutamanisha.....haya mimi kuna kitu kimoja kilikuwa kinanikera sana kuhusu mapishi..ni hivi wanasema wanawake na jiko lakini ukienda mahotelini wapishi wakubwa ni wanaume ..Je ndo kusema wao wanapika vizuri zaidi kulika wanawake? na kama hivyo kwanini wasipike na nyumbani pia? maaana utakuta kupika hotelini sawa lakini nyumbani hapana. Hapa kwa mimi ni tata kiduchu....

emu-three said...

Oooh ndugu wa mimi wanipa njaa nami hapa nimefunga mkanda,maana maish aya sasa ni kufunga, vinginevyo....mmh, kufa hatufi lakini cha moto tunakiona!

sam mbogo said...

Doh! bisikuti yangu,mbona masufuria yamekaa kibongo bongo!? safi sana.msosi wa nguvu, naona samaki wa kweli. kuhusu kupika wanaume tunapika,hasa kama mimi napika. kuna vituvingi vinavyo changia wanaume hasa nyumbani bongo kutokupika nahata kama wanajuwa. mazingira ya bongo nimagumu kiasi fulani mwanaumekupinda mgogngo kupika. mfano ,kwamjini kuna swala la maji,viungo siyo wote wanakuwanavyo mojakwamoja ndani,inabidi mtu atumwe,sasa hiyo kwa wababa ina kuwa ngumu kidogo. majiko ya kuchangia unakuta jiko niwanawake watupu hii nayo inakuwa shida kidogo. ukunaji wa nazi inakuwa ngumu njemba kuazima kibao nakukaachini kukuna nazi hilinalo kwa ndume ya kibongo inakuwangumu,nk.vilevilemaisha tunayo ishi bongo siya mtu mmoja ni familia kubwa,hivyo swala la dada wa kazi nalo lina changia,kwa wale wenye uwezo.wale wenye pesa zao nyingi tu ndo usiseme hatawakezao hawapiki kabisa kazi yao nikusimamia chakula kuona kama kimeiva .ukiangalia kijijini huko ndo usiseme mwanaumekupika,unaweza tungiwa nawimbo.ila kunabaadhi ya wanaume kwa ujeuri wao pale kijijini hupika nainajulikana hivyo,kwamba huyo nimtu wa hivyoyaani inachukuliwa kama tabia.lakina nina hakika huko tuendako wataongezeka wapikaji wakiume hasa mjumbani.huku ulaya tuishiko mfano mimi napika sana kiasi nikama vile ndo mpishi mkuu wa nyumbani kwangu,ila wakati mwingine huwa najiuliza kwanini napika,naoshavyombo? jibu linakuja hakuna aliye andikiwa kupika kupika ni kwa wote inategemea na nafasi.ila wanawake/wakezetu wajanja akisha juwa wewe kupika hakukupigi chenga wanakatabia ka kujisahau!!. kaka s.

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana Waungwana kwa maoni yenu,@da Mija na Da'Yasinta kweli wana mambo kama sikunyingine wangekuwa wanapika hata kidogo na nyumbani.

oohh ndugu wa mimi pole sana maisha kwa sasa kila sehemu ndugu yangu.

@Bisikuti yangu chebwana Sam,masufuria ni kweli bongo,duh Asante sana kwani nimekupata/tumekupata vilivvyo, hilo la kujkisahau lipo sana tuu wala sibishi.