Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 28 February 2012

Jikoni Leo -Bamia,Kwanini Wanaume wengi Hawali?Burudani- Nshomile!!!!!

Bamia za kukaanga na mafuta,Hapo naongeza na nyanya.

Mimi hupenda na Ugali.Bamia za Kuchemsha[Mrenda]
Waungwana hivi ni kwanini mboga hii ya Bamia Wanaume wengi Hawali/Hawaipendi? Jee wewe Unapenda Bamia na Unapikaje?Wengine wanatia na nyanyachungu,Kwenye Samaki Wakavu na....Jee Unaweza kula Bamia na Ugali wa Muhogo? Karibuni sana!!!!

8 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Mie nala bamia. Tena saana tu. Naipenda.
Na burudani...... naburudika.
Si "nshomile"? Hahahaaaaa

Yasinta Ngonyani said...

Ndio na ugali wa muhogo inakubali yaani umenitamanisha wewe kama kawaida yako...ugali na bamia na hii burudani weweeeeeeeeeeee...haya haya. Nilikuwa sijajua kama wanaume hawapendi ngoja tusubiri maelezo

Goodman Manyanya Phiri said...

Kwa lugha ya mama-mzazi huku Bondeni, (Kiswati/Siswati/Swazi nao wako wengi Swaziland karibu na Msumbiji), bamia tunaita "mandanda" au "ligusha".IMANI POTOFU


Wanaume wengi hata hapa hua hawali (shibe?).


Si unajua imani potofu za mswahili?

Niliwahi kusikia hapa Pretoria kwamba eti "magoti ya dume yanadhoofika ukila bamia".

Mimi nawaambia "Hiyo ni LUBRICANT nzuri kwa magoiti kulainishwa... KULENI,JAMAANI!"

Lakini hawataki! Watakukonyezea jicho tu ukiwakaribisha bamia; na ukiwalazimisha watafyonya... shauri yako, Dada Yangu Mwanablogu!SAYANSI YATUAMBIAJE JUU YA MSWAHILI, DAMU YAKE, NA HAMU YAKE?Sababu ingine labda ni ya kisayansi. Maana yake utakuwa unaelewa kwamba, kuliko Wazungu, Waswahili wanayo Damu Grupu "O" ambao tunaambiwa inapendelea kula nyama, kuliko Damu Grupu "A" (ambayo kwa wastani Wazungu wameitawala NA KUPENDELEA MBOGA ZA MAJANI).

Sasa mwanababa mswahili (ukimtofautisha na mwanamama "aliechacha" mwenye kumtegemea baba wa nyumbani kupata vishilingi) akiwa na pesa zake kumtosha, na Damu Grupu "O" kumtuma, lahasha hawezi akala bamia/mandanda! Wala hatapendelea mboga yoyote ile ya majani!!!

Lakwake ni moja tu: "Nyama iko wapi, Mama-mtoto?! Mbona hukupika nyama leo?"

Kama rafiki yangu, Mzee wa Changamoto, nami binafsi napenda bamia sana. Hata sasa hivi naandika kwa kumezea mate! Nakulaumu kwa kunivutia namna hii! Siku moja teknolojia itatuwezesha kutumiana bamia mtandaoni!!!!!


Cheka Kidogo!

SIMON KITURURU said...

Mimi Bamia haipandi ila sikujua wanaume wengi hawaipendi!:-( Na kwa bahati mbaya UJI wa aina yoyote ile , MAZIWA na Ugali wa muhogo haupandi pia!:-(

EDNA said...

yam yam! napenda sana bamia mimi huwa nachanganya na mboga yoyote ya majani,ila sijawahi kula na ugali wa mhogo.

Anonymous said...

mwe bamia bamia jamani umenitamanisha mie, yaani mi nalipenda bamia usiseme ukilipata hata lakuchemsha tu na ugali mweupe hapa mpaka na kumbua unga wa ugali wa kwetu kihesa mweupeeeeeeeeeeeee du kwa bamia acha bana,pole wasio lipenda

emu-three said...

Huenda ni kutokana na ilivyo wengine wanahisi utalegea kama ilivyolegea, ni imani tu, ...Tupo pamoja ndugu wa mimi

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Mie nakulaga ati!

Phiri!!!!