Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 10 January 2012

Wazazi /Walezi wa sasa na Malezi!!!!!!




                        watoto kutusaidia jikoni.

kusafisha vyumba vyao.

kusaidia kusafisha na sehemu nyinngine
Wabaki na Furaha/Amani.
Ni matumaini yangu wote wazima,
Haya wapendwa,Wazazi/walezi wenzangu,vipi watoto kufanya/kusaidia kazi za nyumbani,
Hii imekaaje/wewe unaonaje?kazi kama kusafisha vyumba,kuosha vyombo,kuaanda vyakula na kazi nyingine nyingi,Jee wewe unafikiri ni Umri gani uliosahihi kwa mtoto kuanza  kumfundisha kazi ndogondogo?naje huu ni Unyanyasaji au ni malezi ya kawaida? naje Kuna kazi za watoto wa kiume na wakike?kama ndiyo jee sisi wenye watoto wa jinsia moja je?Unafikiri watoto wote wanapenda kazi? je kama hataki?.
Mimi binafsi kazi nyingine sikuwa nazipenda kufanya nilipokuwa mtoto,lakini mama alikuwa ananilazimisha, jee alikuwa ananikosea au ndiyo malezi?Jee wewe unapenda/ulipenda kazi zote ufanyazo/ulizokuwa unafanya?.
Mwana Umleavyo ndivyo akuavyo au.......

Karibuni sana Waungwana katika kusaidiana Kimawazo,Kujadili na Kuelekezana kwa Upendo!!












6 comments:

Anonymous said...

Watoto wote ni sawa jamani hakuna cha kazi za wakiume wala za wakike, maana kama maisha yenyewe ni kwenye nnchi hizi za ugenini sasa itakuwaje ikiwa wakiume hafundishwi kupika atapikiwa na nani au hata huyo wa kike asipo fundishwa na kukazaniwa baadae aibu ni ya wazazi/walezi wako ndugu zetu wengi tu wakikukaribisha kwao unaona haya maana mama kupika hajui au sijui ndiyo malezi kazoea uchoyo basi unakuta mwanaume anahangaika kukarimu wageni mwanamke katulia,tufundishe watoto wetu kazi na maanadili mema na tukemee kabisa tabia ya uchoyo ina aibisha sana ndugu zangu

Mija Shija Sayi said...

Lalalalaaa.. Nakwambia Rachel hujitaki!! Wenye watoto wao wakikuona unampa kisu jikoni umwekwisha.. Yaani nchi hizi mtoto wako lakini huna mamlaka naye..duh!
Wataanza kwa kuangalia kazi zote hizi mtoto peke yake...siku mbili utasikia hodi ya soshoweka.

Nikirudi kwa swali lako mtoto wa miaka saba hadi nane unaweza kuanza kumfundisha kazi kidogo kidogo kwa afrika lakini. Kwa Ulaya ni afadhali usubiri hadi 18 kama unataka kuishi na wanao...

Nimeipenda hii mada mama T.

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana wapendwa kwa maoni/Ushauri,haya tuendelee,ma'Mkubwa nimekusoma,Ubarikiwe! duhh nchi hizi bwana yaani 18 kwazamani si ndoa jamani,mtu bado hajua kazi za ndani,haya mambo ndiyo asiyetaka kaka NYABINGI.

emuthree said...

Mtoto asipofanya kazi ataijuaje? Ni vyema kumjengea mazingira ambayo hata akibakia peke yake anaweza kuwajibika bila wasiwasi.
Kuna watoto ambao mpaka anafika sekondari hawezi hata kufua nguo yake mwenyewe kazoeshwa kila kitu anafanya mfanyakazi wa nyumbani. Ya mungu ni mengi, huenda mtu ukashuka huko ulipo hadi kufikia sehemu ambayo hujimudu, au ndio hivyoo umerudisha namba, huyo mtoto unatagemea atishije, ndio atafikia kusimangwa kuwa alikuwa akidekezwa.
Ushauri wangu, tujaribu kuwajengea watoto uzoefu wa kila kazi,ili aje baadaye kukushukuru.
Ndugu yangu tupo pamoja

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza kabisa napenda kusema nimefurahi sana kuwa da`Rachel umeitoa mada hii.
Pili napenda kukubaliana na asiye na jina hapo juu ni kweli kabisa hakuna kazi za watoto wa kiume wala wa kike.
Tatu nasikitika sana haya malezi ya ughaibuni kweli jamani mtoto hata kufanya usafi wa chumba chake anashindwa au niseme kuosha vyombo, kujiandalia chakula cha asubuhi, kuchemcha tambi asiweze. Eti mpaka mtoto awe mkubwa miaka 18 je atapohama nyumbani na kwenda sehemu nyingine mama ataenda kumpimkia na kumfanyia hizo shughuli nyingine?..Hakika hili swala kwa sisi tuliolelewa maisha ya kiafrika ina kuwa ngumu sana ..sijui nicheke au nilie? kweli hata kukunja nguo zake hii ashindwe. naona niache hapa nisije nikaharibu maana nina mihasira kwelikweli hapa....

Rachel Siwa said...

Wapendwa ahsanteni sana kwa Ushauri/mawazo na kuelimishana, kwani mimi,wewe,yule.huyu na wale wooote tumejifunza kitu hapa,@da'Yasinta pole na mihasira hivi haya mambo/Sheria zipo U.K. Tuu au??? na Vipi nyie watu mlioolewa/kuoa na mataifa mengine jee mkiwafundisha watoto kazi hizi wao,yaani mzazi mwenzio anaafiki/kukubaliana nawe?Tafadhali jamani mtujuzee..