Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 6 November 2011

Trehe:5/11 NI SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU.


Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.



Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.


Habari hii nimetumiwa na Kabipingaz Blog
Asante sana.

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Asante sana, Mdogo Wangu, kwa kutuletea habari hii kuhusu Mama huyu.

Inaelekea huyu Mtanzania alikuwa na akili zaajabu sana na itakuwa kashfa na aibu kwa vizazi vijao kama hatuweki mtandaoni zaidi ya haya machache tunayeyasoma kuhusu Bibi Titi Mohammed.


Zaidi niseme kwamba, mimi nikiwa mbali na Tanzania nimeisoma habari hii kwa masikitiko na kiu la kujua zaidi:


1. Hivi huyu mama alitendewa haki katika kesi yake, kwa maoni ya Watanzania raia wa kawaida na siyo wahusika wa ngazi za juu katika serikali na siasa?

2. Nyuma ya pazia la kesi yake kulitokea nini iliesababisha watu waliyejenga uhuru waTanzania kama Bibi Titi Mohammed wajihusishe na majaribio ya kuangusha serikali yao?


3. Alikuwa ni mama wa aina gani nje ya masuala ya siasa?


4. Alikuwa na watoto na ndugu wa karibu zaidi ya mumewe? Nao waliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari kuhusu tabia yake? Kama ndio hivyo, nini zaidi tunaoweza kuambiwa kuhusu Bibi Titi Mohammed?



***************


Rest In Peace, Dear Lady! You Made Africa A Better Place For Me And All Other Africans.