Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 1 November 2011

Mimba Inavituko au Kujiendekeza????

Wapendwa!!Umeshawahi kukutana na Baadhi ya Wanawake wenye Mimba za Vituko?
Wengine hawapendi kuoga,Kuchana/kusuka Nywele, yaani hawajipendiiii,Wengine wanakula Sabuni,Udongo na Vingi visivyolika na Watu wa kawaida, Wengine Visirani,Jeuri,Matusi,Kususa[Kuzila],Kudeka na ....,Wengine hawalali/Kulala sana,Wavivu,Hawapendi watu hata WAUME ZAO!!.
Wengine wao wanapeta tuu/hawana tatizo, hawana tofauti za Mjamzito na akiwa kawaida, tofauti ni Tumbo tuu Limejazika/kuwa kubwa, wanajiremba /kuwa wasafiiii mpaka wanapo JIFUNGUA!!!


Jee Sababu ni Mimba au Kiejendekeza?
Wewe Mpendwa msomaji ulishapata Mimba ya hivyo au kuwa karibu na Mtu mwenye Mimba ya VITUKO?
Nasikia Wababa wengine wanakimbia nyumba zao kwa sababu ya Mimba za Vituko, au nao Wanatafuta Sababu ya kuondokea tuu? Sasa  wewe uliyempa Mimba unakimbia jee nani amkimbilie/kumsaidia?


KARIBUNI SANA WAUNGWANA KWA MAONI/USHAURI WENU!!!!!





9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Rachel asante kwa kuliandika hili. Mie binafsi kusema kweli hayakunipata haya. Mimi sidhani kama ni kujiendekeza kwa vile wakisha jifungua wanakuwa kawaida tu.
Halafu nimewahi kusikia kuwa wengine huwa wanapenda kula mchele wa kuloweka. Yaani kama mimi nina mimba basi rafiki, yangu au wifi atakuwa anakula kweli mchele. Mimba kweli zina vituko...

Unknown said...

Unajua mimba huja na mabadiliko ya homoni hivyo sidhani kama ni kudeka au kujifanya....

sam mbogo said...

katika, hili la mimba,kuna somo nimejifunza.1-utamaduni wa kuikubari.2-ushirikiano katika kuikuza,kuilea kipindi chote mpaka wakati wa kujifungua.3-ushirikishwaji na ushiriki wa mwanaume katika mimba mpaka mtoto,nk. baadhi ya haya matatu hapo juu ni msingi mkuu katika swala zima la mimba, katika jamii zetu hasa wakati huu wa utandawazi.mfano kidogo,unakumbuka kwa maraya yakwanza(dada zangu) ulipojisikia una ujauzito muhusika ulipo mwambia alijibu vipi!!? vivyo hivyo kwa akina baba mara yakwanza mkeo/mchumba/hawala/demu wako, alipokuambia anamzigo/mimba yako ulimjibu nini au ulijisikiaje.nimeuliza hivyo kuna kitu pia nimejifunza katika swalilangu hili. ila maoni yenu majibu yenu nimuhimu ili niweze kutoa hilo somo. kaka s

Mija Shija Sayi said...

Rabia sikuwezi sikuwezi kabisaaaaaaa!! labda unambie ni enzi za Nadia!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mimba simzaha. Lazima tuwahurumie wananamama wajawazito na "vituko" vyao!

Anonymous said...

Hello mswahili?
Pole na majukumu, samahani kutokana na hii hoja ningependa kujua kama wewe ulishawahi kubeba mimba au la ili nijue jinsi gani nianze kurusha mashambulizi.

Au labda iwe hoja hii imewalenga watu ambao hawajawahi kubeba ujauzito! zaidi ya hapo nitakuandikia maneno ya kichokozi hapa mpaka utie akili. Maana naona sasa unaanza kejeri.


Wako mtiifu

Mchokozi(www.mchokozi.co.tz)

Goodman Manyanya Phiri said...

Mchokozi njoo! Utamu kolea!


Jibu lako: "Wala, Manyanya ya Mswahili mwenzio sijawahi hata siku moja kubeba mimba, wala sitarajii kubeba. Lakini mimi nawe tuliwahi kubebwa kimimba. AU MWENZANGU WEWE UMESHASAHAU JINSI ULIVYOKUWA UNAMWENDESHA NA KUMHANGAISHA MAMA YAKO MZAZI?!!!"

Kuhusu majukumu, ASANTE SANA KWA POLE. Tena kama ulijuwa: leo natoka mahakama kuu na mambo ndivyo hivyo tena kisheria: YOU WIN SOME AND YOU LOSE SOME.

Anonymous said...

He he he!!! chizi kapewa rungu. habari yako Mwanaume mzuri, naona umeununua hii debate. Lakini nina wasiwasi debate hii your about to get off at the next exit. Kinachoongelewa hapa ni kubeba mimba sio kubebwa mimba.
Manyanya usilete uchokozi mwingine tafadhali.
Let us stick to the point.
Anyway pole na kazi za mahakamani.

Swali kwa mama mswahili
mama mswahili huyu Manyanya ni lawyer wa hii blog?

Rachel Siwa said...

Kwikwikwikwi kwanza nicheke,nitakuwa mwizi wa shukrani nisiposema ASANTENI!!!kwa niaba yangu na wasomji /waliofaidika kujifunza kupitia ninyi wenyewe.

SWALI;Mswahili ulishawahi kubebaMIMBA?
Mswahili mimi Rachel nimesha beba yaani nina watoto.

Na nikiwa MJAMZITO miezi 3 ya mwanzo nakuwa mgonjwa, siwezi kula natapika sana, Yaani nanyorodoka sana[sipendeziiiiiii]Vyakula; nilipokuwa mdogo sana mama anasema nilikuwa napenda sana UJI WA MAZIWA kama sikupata huo hapakaliki,nilipokuwa najitambua mwenyewe sikuwa napenda sana Uji huo na nilikuwa napenda CHAI kupita maelezo,Hapo nyumbani kulikuwa na CHUPA ZA CHAI, kati ya hizo moja ni ya kwangu mimi tuu.

NILICHANA NA CHAI KWA SABABU YA UJAUZITO[MIMBA] SIKUWA TENA MPENZI WA CHAI,LAKINI SASA HUKU NILIPO IMEBIDI NIRUDIE CHAI LAKINI SI KAMA ZAMANI, HILO NI MOJAWAPO LA TATIZO LILILOSABABIHSWA NA MIMBA.

KUOGA SINA TATIZO,KULA VITU VISIVYOLIKA NA WATU WA HALI YA KAWAIDA HAPANA,KUJIPURA[KUJIREMBA] NI KAWAIDA YANGU SI WAKUJIREMBA SANA.

KWANINI NIMEULIZA HIVYO,KWIKWIKWIKWI!!!!
ni kutaka jua hali za Ujauzito kwa wengine,pia hapa wanatembelea wengi basi kuna mengi ya kujifunza,
Pia kuna wanao Ogopa/Kujishauri kwa hofu ya VITUKO/TABU ZA MIMBA,KWANI WENGINE WANAUME ZAO WANASEMA NI UONGO HAKUNA VIOJA/VITUKO BALI NI KUJIENDEKEZAAAAAAAAAAAAA!!!

Nami sikuwa na jibu la moja kwa moja nikaona nifikishie hapa ili TUELEKEZANE WAPENDWAAAAAAAAAAA!!!!!

Mtiifu Madau MCHOKOZI MWENYE VITUKO NA WENGINE WOTE!!MIMI NILIKUTANA NA HAYO KWENYE MIMBA ZANGU!!!

HAYA THATHATHATHA NANYI ZAMU YENU DA'YASINTA NIMEKUOPATA,@ KAKA YANGU MROPE MUNGU AZIDI KUKUSIMAMIA NA MOYO WAKO HUO@DA'MIJA JE WEWE NAONA RABIA HUMUWEZII KWANI WEWE INAKUWAJE?
@ KAKA YANGU SAMA MASWAHILI YAMMETLIA HAYO NAONA TUKUPE MJI NENDA DAR KAKA!!!!!!

@MANYANYA MWENYEWE MSWAHILI WA BONDENIIIIIII,POLE KWA MAHAKAMANI, VIPI KWANI UMEMPA MIMBA MWANAFUNZI AU UMEINGIA MITINI KWA WAMAMA WA MUJINI UMEACHA MIMBA HUKO ZA VITUKOOO?.

TANGAZO:NAMTAFUTA KAKA YANGU ANAITWA SIMON WA KITURURU AKA MZEE WA DUHHHHH MAWAZONI,MARA YA MWISHO ALIKUWA ANATAFUTA MWENZAAAAA.[JOKE]

HAYA WAPENDWA TWENDE PAMOJA SASA!!!!!