Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 18 October 2011

YUSTA MSOKA, MWANASHERIA ALIYEFANIKIWA KUTIMIZA MOJA YA NDOTO ZAKE.
Advocate Yusta Msoka

Yusta Msoka akiwa amesimama nyuma, mbele ya dirisha la pili upande wa kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wenzake baada ya kula kiapo cha kuwa Advocate (Wakili)

KAPINGAZ Blog inapenda kumpongeza sana Dada Yusta kwa kufanikiwa kufika hapo alipofikia, vile vile inamshauri asiishie hapo aendelee zaidi mpaka aweze kufikia level ambayo ni ya kimataifa.

Kwa kutambua uhaba mkubwa wa Mawakili katika Taifa letu tunapenda kuwapongeza wale wote walioweza kufanikiwa kuwa Mawakili, tunawaomba wakafanye kazi zao kwa uadilifu na kuliletea sifa na mafanikio mazuri taifa letu, hasa hasa kuwa makini katika mikataba mikubwa ambayo taifa letu sasa linaangamia kutokana na mikataba hiyo.
                                                                             Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog
                                                              Hongera da' Yusta.

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Masomo ya sheria ni moja katika fani zinazovutia sana kwa wachapakazi. Mimi binafsi nashangazwa zaidi na mwelekeo wa akili ya mwanasheria (psychological make-up)


Yaani wewe mpe kesi ya kumtetea jambazi ataifanya. Sekundi ya pili mfumbe macho na kumfumbua huyohuyo mwanasheria kwa amri yeye sasa awe ni mwendesha-mashtaka dhidhi ya huyohuyo jambazi NAYE MWANASHERIA HUYOHUYO ATAIFANYA KAZI HIYO TENA KWA BIDII ILEILE!!!!


Nawaheshumu sana wanasheria kwa huo uwepesi (nataka kusema "VERSATILITY") wao katika kubadili mwelekeo au mtazamo wao.


Hongera sana Advocate Yusta Msoka!