Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 28 October 2011

Mama mkwe Kuvunja Nyumba/Ndoa,ni Mapenzi kwa Mwanawe?Kwani ni Yeye Mama!!

 Wapendwa, hivi kwa nini MAMA MKWE/WAKWE;Hasa  Mama wa MUME.Mara nyingi wanapenda kuiingilia nyumba/Ndoa za watoto wao, Mpaka wengine kufanikiwa kuvunja/kuharibu Mahusiano/Ndoa hizo.Je wanataka mke wanaompenda wao/ kukuchaguli wao au Mapenzi tuu ya Mtoto wake tangu mdogo mpaka Akioa ndiyo yanamfanya aone/waone WIVU?Na JE nini kifanyike ili hali hiyo isitokee?.

Mimi Rachel nasema;Kina mama wakwe watarajiwa na mliokuwa na wakwe tayari,Jamani Taratibu waacheni watoto wajinafasi,Bali pale watakapotaka Ushauri au inapobidi.
Haya nawe Mpenzi Msomaji unalipi la kuongezea au Ushauri,Maoni gani kwa mama Wakwe wa Aina hii?

Karibuni sana Wababa,Wamama,Wanawake na Wanaume,mliokuwa ndani ya ndoa na mliokuwa bado!!!!!!!.

PATA NA BURUDANI YA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAKA; MRISHO MPOTO!.

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Swawli nzuri sana ..kwani nimekuwa pia mara nyingi nikijiuliza hili swali na sijapata jibu maana utakuta mama mkwe wengine wanapoenda kuwatembelea/kumtembelea kijana wake anadiriki hata kutandika kitanda cha kijkana wake ambaye ana mke. Na Nimekuwa nikijiuliza sijui akina baba pia wana kuwa hivyo kwa watoto wa kike?

Yasinta Ngonyani said...

Rachel nimerudi tena nilisahau kusema nimependa mabadiliko uliyofanya ingawa nidhani nimepotea njia.

Rachel Siwa said...

Hahhahaha dada Yasinta wewe hahaha uwezi kupotea kwako dada yangu tumepanda maua tuu.

Mpaka unafikia kutandika kitanda mi naona kama uchokozi tuu maana humu ndani kuna kazi nyingi tu za kuweza kumsaidia MKA MWANA[MKWEO]pengine huko kwake hata shuka hafui,na kuhusu wababa wakwe hata kama wapo ni wachache lakini kina mama tunaongoza nafikiri da'Yasinta,Hivi na wakwe wa kithungu wanayo hayo au ni wa Afrika tuu?

Yasinta Ngonyani said...

Da´Rachel afadhali hata wakiafrika kuliko wa kidhungu. Nina rafiki mmoja haongei kabisa na mama mkwe wake..kisa hakutaka mtoto wake wa kiume afunge ndoa na huyu mdada. Hata akimwomba akae na wajukuu anakataa. Kwa hiyo hawana maelewano kabisa na wamesutana. kaaazi kwelikweli

sam mbogo said...

mama mkwe nimama mkwe tu ,dada Rachel awe mdhungu/mswahili.muhimu, ni kuwa na msimamo katika nyumba yenu.kuwa mwangalifu, maana uzuri haya yote ukisha mjuwa mama mkwe wako ni wa aina gani basi,jaribu kumkwepa ili msije leta kutoelewana ndani ya nyumba yenu. ila nikazi sana usione ukadhani ni afrika tu hata huku ulaya.kaka s.

Rachel Siwa said...

Da'Yasinta Asante kwanza ya kupenda mabadiliko, pia Asanteni Wewe na Kaka Sam kwa kunijuza kumbe hata wathungu ndiyo bab kubwa, mtu anafikia hata kutowapenda wajukuu zake?
@kaka Sam ni kweli kabisa dawa kuwakwepa, jee wakija nyumbani kwako utamfukuza? maana nasikia mama mkwe mwingine haishi miezi mtatu huyu hapa je utafanyaje?naku nuukuu;ni kazi sana..........

Anonymous said...

Heh heh heh!!!! Mchokozi nimerudi
Kwanza nianze na salam kwako mswahili sijui leo umeamkaje? mchokozi naongezea ulichoanza kusema ni kwamba kuna baadhi ya tabia/sifa ambazo asilimia kubwa ya akina mama wakwe wanazo.

Wao hufikiri wanajua mengi zaidi ya wakamwana wao. Matokeo yake hutoa mashauri mengi hata yasiyohitajika, Hawaheshimu taratibu za wakamwana mahali popote, hivyo hutoa amri(ambao wao hujifanya kama ushauri) haijarishi uko kwako kwao au hata kwenye mikusanyiko ya kifamilia. Yaani kwa kifupi wao hudhani huwa wanasaidia. Lakini huwa hakuna zaidi ya kutaka KU-CONTROL.

Sasa hapo mama mswahili hakuna cha kujiuliza nini kifanyike. Hawa dawa yao pale unapoona hali hii inakuja ni kuonyesha wazi YOU DONT NEED THEIR SOLID ADVICE.

Hakuna haja ya kujiuliza mara mbili kila mtu anawajibika keupelekea maisha yake yawe happy au miserable sso if somebody try to show you unwanted attention you have ability to stop it. WAKE UP PEOPLE HAVE CONTROL OVER YOUR LIFE.

Ni hayo tu.

Wako mtiifu
MCHOKOZI

Simon Kitururu said...

Mmmmh!Langu sikio!

Ila yasemekana WANANAUME wengi ukimchukua mtoto wao wa kike kiaina ni kama umemchukua demu wao kisaikolojia na ndio maana sie wamendeaji chamoto tunakiona kutoka kwa MABABA za nyie MABINTI na WAMAMA ukimchukua mtoto wake wa kike kiaina za kisaikolojia ni kama umemchukulia kidume kitu kifanyacho yaweza kuwa MKE na MAMA MKWE mfanyacho ni kushindania KIDUME anampenda nani zaidi katika WANAWAKE hao WAWILI.

Kwa ujumla BINADAMu ni kiumbe FULU MAMBO MENGI na majibu rahisi ya mpaka ni kwanini MDADA na MMAMA wa toto tundu lililodaka MKE wanagombania atenshenni ya KIDUME si kitu rahisi kuhitimisha kama tu ilivyo kuwa si rahisi kuhitimisha kwanini kuna MIDADA inabwengwa na midume yao lakini imeng'ang'ania KIDUME tu utafikiria tamu kubwengwa!:-(

Goodman Manyanya Phiri said...

@Sam Mbogo

Barabara, kabisa, Mkuu Mbogo! Yataka moyo wa kujaribu kumuelewa mama-mkwe!!!!


Lakusema lakini watoto waachiwe walivyo na penzi lao, ni ndoto tu ya mwendawazimu kwa kuwa penzi lazima litawahusisha ndugu wa karibu kwa wale wapendanao kama vile mama- na baba-mzazi wa kila mmoja wa wahusika, tukipenda tusipopenda!

Rachel Siwa said...

Kwakweli sijui nianzie wapi Wapendwa mliochangia hii mada!!!!Naomba niwashukuru kupita maelezoooooo,yaani kila mtu aliyesoma hapa ninamatumaini ameondoka na kitu/kujifunza mengi sana,Mungu awabariki sana kwa kutoa muda wenu ilikufanikisha/kufikisha ujumbe kwa walengwa,Nimepokea simu kadha wa kadha kwamba kunawatu wameguswa na maoni yenu.

@Mtiifu Mdau Mchkozi nimefurahi kukuona tena, ubarikiwe!!
@kaka wa mimi Kitururu kwikwikwi asante kaka!!!

@Kaka yangu Manyanya hahaha yataka Moyo!!asante sana.

Nakama kuna mtu yeyote anayesoma hapa,Analake linalomtatiza na kutaka wengine wamsaidie kwa mawazo, Karibuni sana, tuma kupitia email hapo pembeni kwenye blog, Nawe kama bado ujatoa lako Rukhsa bado Hujachelewaaaa!!