Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Thursday, 27 October 2011

ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI.


KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.
MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.

HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.

WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.
  
  Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog

Asante sana.

12 comments:

Tayanna said...

Asante sana dada Raheli.....hii unayosema nikweli kabisa maana kama miezi minne hivi kaka yangu alinipigia simu kutaka kujua kama nilicheza bahati nasibu kwa kupitia namba yake ya simu na alikua ameshinda pound elf moja kwa campuni ya nokia...Nikamwambia asitoe details zozote maana mimi sikucheza bahati nasibu mhh na watu wanalizwa sana sana...Thanx again kwa tahadhali

Swahili na Waswahili said...

Pole da'Tayanna, lakini Mungu yu mwema mmewagundua, Duuhhh chanaga la macho hilo!.

SIMON KITURURU said...

Na ulalahoi unatuponza, MTU ukisikia tu umewini unaingia kichwakichwa hata kwenye changa la macho!:-(

Swahili na Waswahili said...

haahhaaahha tena mwingine angetoa na details kabisa, kuna chabure kweli@Kaka Kitururu?.

SIMON KITURURU said...

Hakuna cha bure ila kwa bahati mbaya wengi wetu tunapenda vya bure kitu kifanyacho nasikia ndio kisa kuna baadhi huchukia malaya wauzao kwa kuwa yajulikana sio bure ingawa chuna buzi achunaye zaidi kwa kujidai yake bure halalamikiwi!:-(


Yani Da Rachel we acha tu!
Si umestukia watu bongo tunapigia kura hata tusiowapenda kisa WALI TU wa bure?@Da Rachel

Swahili na Waswahili said...

Nimekupata kaka wa mimi Kituru,tena bora wale wanaopangia bei kabisa kuliko kuchunwa buziii maana wanakuwa na shoga zao wakuchune weee, na buzi ili lionekane linamanyoa shartii lijitutumue huku linaumia,Hapo ndipo ninapo taka kaka zangu Waoe akiwepo na SIMON. Mpaka Wali unaingiza madarakani watu tusiowapenda, kweli Changa la Macho hatusababishiwi na Wapopo tuu Eti ule Usemi unaosema KIKULACHO NI KINGUONI MWAKO NAO UNATAMBA HAPO!!.

SIMON KITURURU said...

@Da Rachel: Si nasikia kuoa au KUOLEWA ni noma kama bado KIDUME au MDADA ananogewa na vitumbua siku nyingine, viazi vitamu siku nyingine , mikate ya Arusha siku nyingine, na bila kusahau VITUMBUA!:-(

Swahili na Waswahili said...

Hahahhaha hapana kaka utakula vivyochaha au kuoza kaka yanguuuu,miokate ya siha,grolia na vyote havina maana@kaka Kitururu chako ni chako,UTAMALIZA BUCHA ......AU?

SIMON KITURURU said...

@Da Rachel: Aku Babu! Nasikia kumalizia vya bucha utakula mpaka damudamu na nyama zisizotakiwa na wengine na kirahisi yasiyolika yatakua yako KINYONGO,.. na na NYONGo eti ni SUMU !:-(

Tatizo mali bon´mba kwa kawaida huwa zishadakwa na wajanja. Si umeona ya Da Rachel , Da Mija, Da Yasinta Ngonyani au tu Mke wa Kikwete kama si DA MIGIRO?:-(

Swahili na Waswahili said...

hhahhahh umeniuwa Aku babu,mali bon' mba mbona bado zipo tuu @kaka Kitururu; Hao umeshachelewa wangu pole, lakini wana wadogo,ndugu,jamaa,jilani na marafiki, tena vyema umshirikishe mama Simon maana asianze oohhh huyu mbona kimini au ooooh Mbona Simon unapika sana, Achana na kuokoteza kaka yangu!!!

SIMON KITURURU said...

@Da Rachel: Yani kuokoteza taabu!Umegusa kabisa eneo. Na sasa ukiwa tu na kishughuli na WADOGOO unadai wapo mie nitakuwa fulu kujipendekeza !
Ila sijui hiyo itamaanisha najipendekeza KIUDOEZI wa DOGODOGO saizi yangu au vipi tena! Ngojea niwaze!:-(.....:-)

Swahili na Waswahili said...

Hahahhahaa hapana sikujipendekeza KIUDOEZI@kaka Kitururu mawazoni saa zote utapata vidonda vya tumbu@