Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 18 October 2011

AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!!




Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang'hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.
                                                            
                                                                          Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog
                                                             Asante sana kaka Kapinga.

2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

KapingaZ Blog hawatutendei sisi wasomaji wa makala yao haki. Nasema: si vema mwandishi kudai eti watu wamewatuma wengine kufanya uhalifu lakini hatupewi hata fununu na mwandishi huyo NI NANI ALIEMTUMA MHALIFU. Hata kama mhalifu katumwa, kwanini KapingaZ Blog YAPINGA kukamatwa kwa wahalifu ili wawataje wale waliyowatuma?


Acha, Mdogo Wangu Rachel, ninukuu pale ninapoachika kwenye mataa na mandhari yake KapingaZ Blog:



“...sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!”

emuthree said...

Ndugu yangu tupo pamoja, nimewahi ili nipitie pitie kwa wenzangu, looh, ,mtandao nao unagoma...