Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 17 September 2011

Ukatili Mbeya!!!!!!!!

VITENDO HIVI VYA KIKATILI VYA WATU KUPIGWA NONDO VITAISHA LINI MBEYA?

Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.

Bwana Zefania Mwangwale mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Uyole akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya baada ya kupigwa nondo pia.

Vitendo vya watu kupigwa nondo kwa Jiji la Mbeya vimekua kama ni vitendo vya kawaida, ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu kila mwaka lazima hivi vitendo vitokee na kupelekea watu wengi wa jiji la Mbeya kuishi katika maisha ya wasi wasi sana.
KAPINGAZ Blog inapenda kuviomba vyombo vyote vya usalama Jijini Mbeya kuona kama hivi vitendo kama ni janga kubwa kwa watu wa Mbeya.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

haki inasikitisha sana na jambo hili linabidi lishughulikiwa haraka sana...Huwezi kuamini kuwa ni kweli ni hiii Tanzania yetu isemekanayo ni yenye AMANI.

Swahili na Waswahili said...

da'Yasinta kweli inasikitisha sana, Tanzania yenye Amani.