Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 30 September 2011

Ubatizo wa da'Arianna,Uliofanyika Tanzania!!!!!!

                             Da'Arianna na mapozzzz.
                    Siku zote uwe Nuruni.
        Shangazi akiwa sambamba na mtoto wake,Hatimaye Arianna anabatizwa.
                          Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina!!
                    Mama Arianna kama anaota vile.
                         Familia pande zote 2, walikuwepo.
                       Familia sambamba na Mpendwa wao.


                 Mashangazi wa Arianna, wapo Makini.
                           Mjomba na Shangazi wakifurahi.
              Nakuaminia  MAHOZA hapo huhitaji msaada.
                 Kula mama mimi penda sana wewe Rafiki yangu.
                      Kula kwa niaba ya baba, mimi penda sana wewe ba'Mdogo.


             Asante sana mama kwa kunisababishia haya , baba yako inakuja hukohuko.
             Arianna mwanangu tumemaliza ehh, Ndiyo mama, yaani nilikuwa naogopa.


Arianna;  Ali BATIZWA katika kanisa la KIANGLIKANI  MAGOMENI,DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.
Baadae walielekea kwenye Sherehe ya kumpongeza kwa UBATIZO na Kufika kwake TZ.


Ujumbe kutoka kwa Wazazi wa Arianna;Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jambo hili na mengi mema aliyotutendea.Pia Tunawashukuru sana Wazazi wetu,Ndugu,Jamaa na Marafiki wote,kwa yote.
Mungu awabariki sana sana.


   :Swahili na Waswahili inakutakia maisha mema da'Arianna na Hongera sana,
    na pole sana huku kucheza kama Bongo sahau, lakini Mchanga unauzwa hata Tesco mwanangu.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kwa siku ya ubatizo wako Arianna sasa umekuwa mkristo kamili!!

Anonymous said...

THANKS DADA RACHEL

Goodman Manyanya Phiri said...

Arianna, Hongera sana, Mwanangu! Sasa ubatizo umepata; ni kama silaha na ngao dhidhi ya mengi magumu ya dunia ili moyo wako upone milele na milele vitani vya roho. Tunawapongeza wazazi wako kwa kukupitisha katika mto huo mtakatifu wa ubatizo!

Anonymous said...

Naakue katika imani ambayo wazazi wamesha mwazilishia....Mungu nimwema na atampigania katika mambo yake yote....Amen

SIMON KITURURU said...

Hongera Da'Arianna !

Mija Shija Sayi said...

Yaani Tina likizo umeitumia vizuri sana....

Hongera Sana Arianna.