Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 20 September 2011

kweli kulea Kazi!!!!!!!

Hata sijui nini anatafuta huko jamani, Mmmmhhh Tumetoka mbali sana.
Mpendwa unayakumbuka makabati ya vyombo ya Zamani yenye wavu kama wa dirisha?
mama yangu aliweka Ufuta huko,umetengenezwa kama vigorori hivi,mimi na kaka yangu tulikuwa tunautaka,
mama akasema tutapewa tukimaliza kula chakula,tumemaliza chakula mama kaondoka,lakini tunajua ulipo,mwenzangu  mimi nikaambiwa niupandie, hahahahaha kama wewe BINGWA panda,Sifa zikaniponza, nikaupandia weee nikala mweleka wa nguvu na kabati juu yangu, wenzangu wakatimua mbio,badala ya kuniokoa, Sasa na huyu naye yange mkuta yaliyonikuta jee? Kweli Kulea Kazi jamani, Wazazi /Walezi tuwe makini sana na Watoto.

Mpendwa huna kisanga kilichokukuta unachokumbuka?
Hujapitia mambo yakutaka  kuwa Bingwa/Mshindi?.

Karibuni sana.











10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ha ha ha haumenivunja mbavu..nakumbuka siku moja nilimkuta kijana wangu amestarehe kwenye jokofu ...nilistuka hakika watoto/utoto una vituko...Binafsi sikumbuki kama nilikuwaa mtundu hivyo nikikumbuka ntarudi...:-)

Rachel Siwa said...

hahahaaa @da'Yasinta Erik alikuwa anaona jotooo.

sam mbogo said...

dada yangu hata mimi umenikumbusha,kijana wangu yeye ndo ilikuwa kazi yake kubembea kwenye mlango wa friji,na pia kuingia nakutakuufunga mlango.sasa baba mie wa kibongo weeeee!! acha tu,nataka kumfua lakini, ulaya mama utajikuta ndege inayo fuata kesho uko bongo,unabaki kumwangalia nakulia!! tu asante dada wa swahili na waswahili.kaka S

Simon Kitururu said...

Kutaka sifa za ubingwa zilikuwa inaniponza utotoni!

Basi nilishakula sana pilipili kichaa kwa kutaka kuonekana dume halafu navyowashwa nikitaka kulia wanadai kama ntalia sio dume !Basi kwa kutaka sifa nakula pilipili huku chozi linanitoka na kujaribu kutolia kwa sauti kwa kutaka kuonekana dume!

Utoto wee acha tu!

Anonymous said...

Ha ha haa, umenichekesha kweli umenikumbusha mtot mmoja wa mpangaji mwenzangu mabibo, yeye alikuwa anampenda sana mume wangu, basi akija kwetu mamaake akimfata anaingia kwenye kabati kimya, tena sijui huwa anajuaje mamaake anakuja yaani unaongea nae ukigeuka humuoni, mamaake akija Billy yuko huku tunamwambia alikua hapa sasa hivi, mamaake akiondoka tu anatoka kabatini hana mbavu....lol

chib said...

He he heee Kitururu!

Stephano said...

Utoto raha na karaha, lakini ndio maisha!

Utundu wa utotoni. Nakumbuka baba yangu alikuwa na cherehani. Basi siku moja katika kuwaonyesha wezangu kwamba najua, nikachukua kipande cha kitambaa na kuanza kushona. Mikono ikajichanganya kwenye kupitisha kitambaa pale kwenye sindano, ikaingia kwenye ukucha wa kidole gumba! nilipiga ngolo (yowe!), wezangu wote wakasambaratika, nikabaki kama 'panya aliyenasa mtegoni!'

Rachel Siwa said...

Jamani kweli kulea kazi, kakaS, hahahaha unapandihswa pipa!!!!

kaka Kitururu hahhahhaahahahhaa!!

Anonymous;Billy alikuwa na machale mambo ya kuwa mtoto wa mama hakutaka,

Mwagito[stephano] hahhahaha jamani kama uliniona yalinikuta yakushona kucha hahhahaah,

Kaka chib huyo ndiyo Simon!!!!!

Unknown said...

Nyie bwana acheni. Mimi ninavisa vingi sana nilivyowahifanya.

Kwanza nilikuwa tiba sana kwa mama na familia kwaa ujumla maana nilikuwa ninavichekesho sana hadi kuku walikuwa wanacheka, kila nilipokuwa nikifanya jambo au kuzungumza watu ni kucheka mpaka kuku nao wanapiga kelele mithili ya kucheka vile.

Kuna matukio niliyoyaboresha nilipojifunza sarakasi na kuweza. Mimi kwangu ilikuwa ni hali ya kawaida lakini waliokuwa wananitizama mpaka leo huwa naulizwa: Hivi ulishaacha utundu??

Rachel Siwa said...

Hahahaha kaka Mcharia umeacha Utundu?