Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Monday, 26 September 2011

Kaka Joel Atimiza Miaka 5!!!!!!!!

             Mwenyewe kaka Joel.
             Kaka Joel akiwaza juu ya miaka 5.
            Akikata keki na da'Tracey akishuhudia.
            Kaka Vin ndiye aliyetuongozea sala ya Chakula.
           da'Manjula akiwa kwenye Sala.
             Hakukuwa na Shani leo ni juisi.
         Kama kawaida ya da'Damari yupo makini kwa watoto.
            da'Damari akihakikisha kila mmoja hakosi keki.
        Mwenyekiti na msimamizi mkuu wa watoto wa Swahili Fellowship, da'Mija Mwanamke wa Shoka.
   da'Josephine ,Mdhungu Mswahili mwenye vituko alikuwepo.
    Wamama waliwakilishwa na Mke wa Mwenyekiti wa Swahili Felloship da'Edna.


Familia ya Bwana Godfrey[Mzee wa Fellowship] na bibi Mellanie wa Coventry,U.k.
Wanamshuru sana Mungu kwa kumtunza mtoto wao Joel na Mungu azidi kumsimamia katika makuzi yake,
Awe baraka kwao na kwa Jamii pia.
Shukrani za pekee ziwaendee Watoto wote wa Coventry Swahili Fellowship,Mwenyekiti da'Mija na msaidizi wake da'Damari, Bila kuwasahau Wazazi/Walezi na wote waliofanikisha sherehe ya kaka Joel.
Mungu awabariki sana na wanawapenda sana.

Familia ya Isaac na Cuthbert wa Coventry nao wanamtakia kila lililojema kaka Joel na Mungu awenawe daima,Pia wanasema asanteni sana Familia ya Godfrey kwa yoteeeee!!!Mungu awaongezee kila inapoitwa Leo.


Mengineyo; Kaka Joel anapenda sana Magari na kuyajua mnoo,Mpaka ananishinda mimi jamani, kila aonapo Gari  alipendalo atakwenda kumwambia Mjomba Isaac na Wazazi wake, kutwa anatafuta Magari kwenye Computer, kama uonavyo hapo kwenye keki alikosa Gari kapachika ka'Pikipiki.


Swali; je kupenda huku ni kwasababu ni mtoto wa kiume,akikua anaweza kufanya kazi ya Udereva au zinazohusiana na Magari au ni Utoto tuu akikuwa ataacha?.

Wewe mpendwa kunakitu ulikuwa unapenda wakati wa Utoto na mpaka Leo unakipenda/kukifanya?
Karibuni sana!!!


6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kaka Joel kwa kutimiza miaka 5..Hongera pia wazazi kwa kazi kubwa mloifanya...nimependeza na ushirikiano mlionao...Nje ya mada Mija umetoka chicha mdada:-)

SIMON KITURURU said...

Hongera sana Joel!

Anonymous said...

Mungu akujalie maisha marefu, hongera sana Joel

Goodman Manyanya Phiri said...

"HESHIMA KWA WAZAZI, JOEL"(hili ni shairi la Mjomba Manyanya kwako, na anawaomba wajomba wengine wamsahihishe Kiswahili halafu wamtumie manyanyaphiri@gmail.com)
... Kwetu Uswahili unatoka...
....Angani huko pananyota...
Tupatie moja Joel tusisononeke!
Tunakushangilia Mtoto wewee!MIAKA MITANO Joel Hongera!
Unaugusa mlima na kujitangaza!
Mlima wa Uchagani siyo utani!
Milima Himalaya wengi imetwanga!


MIAKA KUMI Joel kweli umekua!
Mara ya pili Mlima unagusa
Maisha ya mlima na vumbi unanusa
Mikono miwili mlima umekumbatiwa!Kilimanjaro ya kale nayo kuitika
Lakwako Joel hapo ni kukiri
Majukumu juu ya maisha nimeshika
Miaka kumi wazazi hawakuninyima!Joel tayari MIAKA KUMI NA TANO!
Jina lako hakika Sibusiso Vilane
Mguu mmoja tayari umenyanyua
Kuupanda kabisa mlima wa maisha


Sasa kweli Mjomba uko tayari?
Utayumbayumba au utashikilia?
Kigugumizi Mjomba wewe cha nini?
Uoga waMusa mie Joel sisingizii!
Mjomba mie simu nipigie
Kuwashughulikia Wazee sisiti
Kwanini mkawie kumpa siri?
Mlima kupanda mtoto ajizatiti!MIAKA ISHIRINI kwa Joel Bingwa
Jogoo huyu kotekote anawika!
Usielijuwa wakuambie lipi?
CHUNGA Juu ya Kilimanjaro umefika..


..Upareni wa milima hawana upara!
Ukipaa juu vichwa-uzee vising'are
Hiyo kwa lugha ya Wazazi niHeshima
Uyaoneje maboga macho juu umegeuza?Angani huko Joel pananyota!
Moja tupatie ndoto tumechoka!
Simabawa tumeyaona..?
...Tunashangilia yanaota!

Goodman Manyanya Phiri said...

Kuhusu magari ya utoto: Tunatoka mbali na magari hayo. Pia tunakwenda mbali. Mimi nikiwa umri wake Joel nilikuwa na magari mawili: moja kubwa la rangi nyekundu kwa ajili ya kubebea mchanga, halafu lapili ndogondogo lakutembelea mimi kama bosi wa kampuni, rangi zambarau... aisee utoto kweli ni ufalme!

Lakini naamini sana magari hayo yalichangia kunipa moyo wa kujifunza mwenyewe kwendesha gari nikiwa na umri 13! Magari yamechangia pia kunipa moyo wakujifunza vyombo vingi nikiwa mtu mzima sasa kiasi kwamba hata matumizi ya kampyuta nilijifunza mwenyewe (1998).

Ukweli ni kwamba napenda kuvitawala vyombo; na kukiri, HATA BINADAMU NAPENDA KUMTAWALA (na nilishangaa majuzi kuona gazeti moja A. Kusini limechapisha habari kwamba mtoto wa umri 16 anaendesha ndege pekee yake! NINI HAPO CHA KUSHANGAZA???)


Malezi ya mtoto hayo!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana kaka Joel kwa kutimiza miaka mitano... Mungu azidi kuwa nawe hata utimize ndoto yako ya kuwa injinia wa mandege...magari kitu gani bwanaaa!!

Hongera sana.

@Yasinta, asante sana na Mungu akubariki, ila si uongo huku kuna ushirikiano sana nadhani kwa sababu kuna watanzania wengi zaidi kuliko nchi nyingine zote za Ulaya.

@Mjomba Manyanya, utenzi nimeuona, unalipa si kidogo kaka.