Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 5 July 2011

Mama Lwanji Asema, Shikamoo zikizidi ni ukosefu wa Akili!!!

                                 Mwalimu Lilian Lwanji [mke wa muheshimiwa Lwanji].
                                 Muheshimiwa Lwanji akitoa machache na mama pembeni.
                              Mama Lwanji akiwa na binti yake.
Nanukuu;  Hivi mtoto wako ukikutana nae Sebuleni akakuamkia Shikamoo,Muda mfupi baadae unakutana nae chumba cha stoo akakupa Shikamoo, Tena unakukutana nae chumba cha Kulia chakula anakuamkia Shikamoo,Je hiyo itakuwa ni Heshima au ni ukosefu wa Akili?

Maneno hayo  ya Mwalimu Liliana Lwanji, Jee wazazi/walezi manasemaje kuhusu hizo Shikamoo?

Karibuni sana Waungwana!!!!!!

Habari na Picha,zaidi  zinapatikana;kwa, Mohammed Dewji blog!!!!!!7 comments:

emu-three said...

Huenda yeye ana maana yake nzuri, lakini tukamnukuu kwa hayo maneno machache, na mwisho wa siku tafsiri halisi ya alichokikusudia hapo ikaondoka!

Swahili na Waswahili said...

Nikweli mpendwa emu-3 huenda anamaana yake nzuri, je tukiachana na maana yake yeye, mimi,wewe na wengine tukitupia jicha kuhusu malezi ya watoto na Shikamoo nyingi,labda ni woga au anamatatizo mengine au ni hali ya kawaida/heshima iliyotukuka au.....

Paoja mtu wangu!

SIMON KITURURU said...

SHikamoo zikizidi ni woga huo!

Na shikamoo nikipewa na MDADA mkubwa huwa nahisi kuna kitu anataka kuninyima kwa kujifanya yeye mdogo!:-(

Mashughuli said...

Mimi naona sio sawa Simon, mbona mke anamwamkia mume wake kwa sababu umri wao ni tofauti, na usiku wanalala kitanda kimoja???

SIMON KITURURU said...

@Mashughuli:Kulala kitanda kimoja sio hoja -Ila shikamoo inaweza kuwa inaathiri wanalalaje katika hicho kitanda kimoja!


Mimi naamini katika ndoa kama nikipata lishuga mama langu halafu likitaka nilipe shikamoo nitaathirika kisaikolojia na kuna mambo ntakuwa siyafanyii UTUNDU kitu ambacho naweza kujikuta nafanya na hausigeli ambaye twaheshimiana bila shikamooo kiutuuzima!

Neno shikamoo ambalo kirahisi hutokana na sentensi ´´niko chini ya miguu yako ´´- mie binafsi naamini ni neno linaloathiri sana na laweza kuwa ni moja ya sababu ifanyayo Watanzania na Wakenya hata kiushapu/UTUNDU kunatofauti.

SHikamoo kiaina ni mwanzo wa wakujiwekea mipaka na kudhaifisha baadhi ya MAUTUNDU.

Haki ya nani mwanamke ampaye shikamoo mme wake mie naamini ni rahisi kuonewa na mme huyo huku akivumilia kuliko mwanamke ambaye mmewe kimke na mme wanasahau umri.
Na mwanamke atoaye SHIKAMOO kama hana mume mwenye huruma huyo kichakula cha usiku kamwe hawezi kugewa akashiba.

Na inasemekana(sijafanyaia utafiti) kuwa wanawake wampao mme shikamoo ndio rahisi kwa mme wao kutofanya mambo fulani kistaili ya kuchochea unyumba -na kwa mwanamke huyo vilevile yasemekana ni fulu heshima mpaka kwenye unyumba kitu kifanyacho -hasa wanaume- kwenye mahusiano ya aina hiyo kuwa na kimada ambaye ndio maswala kinaeleweka 100% kisa kwenye nyumba maswala ni kabla ya tendo hata la asubuhi kabla ya kwenda kazini huanza na bonge la shikamoo kitu kiwezachofanya lidume zee kukumbushwa kweli ni zee kitu ambacho huondoa nguvu ya machojo!

Ni mtazamo tu!

Anonymous said...

Mimi niko nje ya mada jamani.....yaani kunawatu wanajua kufanana....huyo dada na mtufudenge ninae sali nae kama mapacha vile....Kwakweli nami naungana na mama kbs shikamoo nyingi ni ni nidhamu ya woga....


Mpendwa....

Anonymous said...

Hahahahahaha aminia kaka Simon....toa darasa.....hakuna mambo ya shikamoo kwa mume wako...salamu ya kawaida na kiss ya kumuaga aendapo kazini inatosha sanaaaaaaaaaaa.....tufungue macho kaka.
Mpendwa...