Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 5 June 2011

Mtoto Wetu Leo ni Frank- Jayden!!!!!!!!!!!!!!!!

 Hapa anawaza leo nianze na  Mchezo upi au nikacheze wapi Sijui?
 Nimekuja kunywa maji tuu,Wao wameshanibana nisiende tena kucheza je hii ni haki jamani?
 Nimeshindwa kutoka tena,ahhh ngoja nioge zangu tuu!!!!!
 Sasa watajuta kunifungia ndani ,mimi naungana na huyu ni kelele tuu mpaka kieleweke!!!!!!
 Wakaona wanitoe kidogo hata kwa Mangi nipate walau Soda!!!!!!!
 Hapa sasa mambo poa watu wangu, Asanteni kwa Ofa baba na mama!!!!!!!!
Ngoja nikatafute Elimu , Eti yule babu wanaemuita sijui NYERERE [R.I.P] Nimeambiwa alisema Elimu ni Uti wa Mgongo,Sasa sijui kama nikweli au maneno tuu.

Waungwana kila Mtoto anavituko vyake,Hata wewe kwenye Utoto wako ulipitia mambo mengi  sana mpaka kufikia hapo ulipo.Katika hayo ya Mtoto wetu Frank-Jayden, Umeguswa/kumbushwa na  nini katika Maisha ya Utoto?. Karibuni sana kwa Ushauri na kuelimishana katika malezi ya Watoto wetu!!!!!!!

3 comments:

emu-three said...

Kweli mtoto wetu, elimu ndio msingi wa maendeleo soma sana. Mpendwa tupo pamoja!

Yasinta Ngonyani said...

Watoto watoto... ni viumbe vyenye kupenda kujifunza ni rahisi sana kwao kujifunza hawana aibu kama watu wazima... Frank umeamua la muhimu sana katika maisha yaani kwenda shule......Rachel Nimependa hilo badiliko hapo juu...ila nitamiss ile picha ya kwanza hazi zile ndizi..LOL

Rachel Siwa said...

Asanteni wapendwa kwa niaba ya Frank!

Asante da Yasinta nimedilisha kidogo muonekano,kuhusu ndizi dada usijali njoo huku ili ule vizuri bwana!