Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 26 June 2011

Jikoni Leo ni Kisamvu!!!!!!

                                         Hapa kipo jikoni.
                                        Hapa kimeshaiva.
                                      Kimepakuliwa.
                                     Ngoja tuongezee na samaki kidogo.
                     Ngoma ndiyo hiyo mwendo wa nguna.


Unapenda Kisamvu na je unapenda kula na nini? Wewe unakipikaje na Karanga,Nazi,Mafuta ya Mawese, Mafuta mengine ya kupikia tuu au Unachemsha/Chukuchuku?
Mimi hupenda kuweka Nazi na Kitunguu tuu,wakati mwingine naongeza pilipili Hoho.Zaidi napenda kula na Ugali.


Eti Kisamvu ni mboga ya Watu wasio na pesa/hali ngumu?
Kunawimbo pia ulikuwa ukiimbwa ;Ukila Kisamvu kaza roho mama Dar-es-salaam Jiji umbea Mwingiiiiii!!!!!


Zao lenye faida nyingi, Majani mboga,Mti wake kuni,Mzizi wake unaweza pata Ugali na Muhogo ukashushia na maji,chai, pia unaweza kupika Uji wa Muhogo.
Karibuni Waungwana!!!!!!!!



11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Rachel mchokozi...ila si mbaya sana ni keshokutwa tu nitakuwa kunyumba na nitakula, nitakula. Haya mie huwa napenda Kuchemsha /chukuchuku na napenda kula na ugali halafu ungejua hicho ni chakula changu nilichokulia....halafu swali la kizushi..unajua kama kula ugali na kisamvu wakati mvua inanyesha ni utamu sana???...mimi nionavyo:-)

Anonymous said...

Asante kwa kisamvu, ni mboga nzuri sana. Ila inatakiwa kuliwa mara moja moja. Ukila mara kwa mara inakinai. Ni nzuri kuweka nazi na kitunguu pia pilipili mbuzi.

Simon Kitururu said...

Mie Udenda umenitoka!

EDNA said...

Umenikumbusha mbali sana,mimi hupenda kisamvu cha nazi tena ukiacha kilale ule kesho yake ndio kinanoga zaidi.

Evarist Chahali said...

Yum yum.Yaani Rachel umesababisha ugomvi kati ya tumbo la ulimi.Tumbo linadai haki yake,ulimi nao unabubujikwa mate kwa tamaa.Asante kwa picha hizi nzuri

emu-three said...

Tumbo limelia ngruuuu! siunajua tena hii ni lunch time, na ukiviona vitu kama hivyo tumbo linadai...TUPO PAMOJA

Goodman Manyanya Phiri said...

Nipe kisamvu kwa namna yoyote ile NITAKULA, kwani sisi wenye miBLADI GRUPU yakiajabu-ajabu, utakuta mboga za majani kwetu ni kama nyama kwa wengine!

Lakini unipe kisamvu chenyewe pamoja na ugali wa mihogo (CASSAVA)wala siyo wa mahindi! Sijawahi kula wala kuona ugali huo TZ, lakini huko Chilumba, Malawi, aiseee....

... Sasa naona njaaa...ngoja niende jikoni!

mumyhery said...

Mwanangu mimi kisamvu hukipika na mawese, karanga, huongezea nyanya mshumaa, nakipenda kula kwa wali, ugari, mhogo wa kuchemssha au viazi vitamu vya kuchemsha

Rachel Siwa said...

Ahsante sana wapendwa kwa maoni yenu,
@da Yasinta kama nakuona huko nyumbani wangu,unapata vitu kamili.
@da Mumyhery nami nitajaribu ili nipate hiyo radha.
@Anony ni kweli kila kitu kwa kiasi.

@kaka Kitururu hahahha pole wangu!
@da Edna umenena je Shemeji umeshampikia Kisamvu?

@kaka Chahali na emu-3 ahahhahaa poleni sana.
@kaka Mnyanya TZ tunakula Ugali wa muhogo.

chib said...

huwa nakwepa sana kuangalia blogu za vyakula, kwani hii ni kutesana tu, kuvila kwa macho :-(

Rachel Siwa said...

hahhaha jamani kaka Chib tunakukumbusha tuu ili usisahau nyumbani!!!