Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 7 May 2011

Watoto na Urembo!!!!!!

Mzazi/Mlezi na Mwana familia.Unamawazogani kwa watoto wadogo na  kujiremba?.
Hasa kwa mtoto wakike wa Leo/Sasa, Unafikiri ni umri gani kwake unafaa kwa kuanza kupaka,Shedo,Wanja,Rangi za mdomo,Kunyoa nyusi, kupaka Poda na mapambo mengine yanauotumiwa na Wanawake /kina Mama.Na si kila Mama/Mwanamke anayependa kujiremba pia.
Karibuni sana kwa Kuelimishana na Kusaidiana katika Malezi ya Watoto wetu.

12 comments:

emu-three said...

Kila jambo lina muda wake, sio vyema watoto wadogo kuanza kutumia mapodozi, na yanaweza kumkomoza...siunajua tena, mio ndio maoni yangu

EDNA said...

Mmmmh wengi wao huwa wanaanza wakishabalehe,maana hiki ni kipindi ambacho usichana unakuwa umeingia....hivyo basi katajipodoa hadi basi, hapo mzazi hata upige kelele za namna gani hata kusikia kamwe.Ni kipindi ambacho kanakuwa kanatafuta attention ya wavulana.

Goodman Manyanya Phiri said...

Ukiwa rafiki kwa mwanao KIWANGO KINACHOKUBALIKA, hasa nyie akinamama, utaelewa kwanini vipodozi vitakuwa mhimu kwa siku fulani kwa mwanao WAKIKE.

Mimi kama baba-mtoto sioni kosa la kujipodoa kwake ili mradi inategemea na hali au mategemeo ya siku fulani...

...LAKINI SI KWA KILA SIKU!!! LAHASHA VIPODOZI DARASANI!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Hili swala kwa mimi kwa kweli sioni umaana wake. Kwanini kujipodoa? kwanini mtu usiwe tu kama ulivyo? najaribu kumuelimisha binti yangu na najua si rahisi kwa vile ana marafiki ila najua nitaweza tu.

Rachel Siwa said...

Nikweli kaka @emu-three,kila kitu kina muda wake, wewe unafikiri labda wakifikia umri gani?

@da Edna mbona umeanza na kuguna kwikwiw!attention ya wavulana!sasa tufanyeje?Mungu atubariki.

@kaka Manyanya asante sana kwa mawazo yako!.

Da Yasinta hapo kwa marafiki,lakini nimefurahi kuona hukati tamaa dada.

Duuhh mimi sijui niseme nini,maana kama mimi sipendi yeye anapenda, zaidi ni kumuelimisha wewe bado hayo mambo, wewe ni mtoto bado na vipodozi vingi vinamadhala kwa ngozi yako, hapo baadae ngozi yako haitakuwa njema tena,na ukijizoesha ukiwa mdogo hata kuacha baadae itakuwa ngumu.Pia kama alivyosema kaka EMU vinakomaza sana.

tuzidi kuelimishana wapendwa!!

WEE JE UNAMAWAZO GANI?

Simon Kitururu said...

Mimi nafikiri kwa mtoto vipodozi sio vya lazima kama tu kwa wakubwa. Na siku hizi vipodozi na mavazi ya kikubwa kwa watoto ukizingati na watoto wakuavyo kama kuku wa kizungu siku hizi huweza kuchangia mpaka watoto kubakwa au hata kufanywa vibaya na vizee kwa kuwa kwanza vipodozi na nguo kama viruka njia hufanya vidume wengine wakimuona mtoto waanze kumfikiria kikubwa .

Nafikiri mara moja moja mtoto kumuigilizia mama sio mbaya ndio mazoezi yenyewe!

Na haya mambo ya vipodozi kwa watoto yapo hata kitamaduni tokea zamani ingawa ya siku hizi ya watoto wadogo na wamama wakubwa kujiremba sawa virembeo vilevile nahisi ni jambo jipya!

Nafikiri ni muhimu watoto wabakie watoto kwani muda utafika tu kwani haraka ya nini?

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli usemavyo Simon, ila kwa nini kujipodoa? kwa nini mtu usiwe kama ulivyo? Ni ruksa kubisha ila mimi sioni sababu ...

Rachel Siwa said...

Wapendwa @kaka Kitururu si uongo kwani wanajipodoa na mavazi yenyewe duuhh. Hajulikani mtoto nani mkubwa nani.

@da Yasinta kwikwiwkwi dada yangu wanaongetha Urembo!Nami naungana nawe usipojipoda sithani kama utapungukiwa kitu,kama unapendwa utapendwa tuu.Ngoja tusubiri na wengine watajibu nini katika Swali lako Zuri na lenye maana na kutaka kujifunza sote!
Asanteni sana kwa kuendeleza mada hii ilitusaidiane!!!

Anonymous said...

mimi naona watoto wengine inategemea sana mama, kwa mfano siku hizi unakuta kibinti kidogo labda miaka mitatu, mama anamnunulia handbag, humo ndani anamuwekea vitu mbalimbali vya kujiremba, lipstick, kajikioo n.k, kila wakati unakuta mtoto kafungua bag yake, mara ajiangalie kwenye kioo, mara aweke lipstick basi tu ilimradi anakuwa busy, kwa wale ambao hawapati nafasi ya kuwekewa hivyo vitu na mama, hao sasa wakifikia usichana wenyewe wanaanza taratibu kuona umuhimu wa kujipodoa, hayo ndiyo maoni yangu, itabidi nichunguze hao binti zetu hapo kama wanatumia au la.

emu-three said...

``Nikweli kaka @emu-three,kila kitu kina muda wake, wewe unafikiri labda wakifikia umri gani?''
Nikuulize mpendwa kwanini mtu anajipodoa, ? kwangu mimi ni kwasababau anataka kuongeza uzuri, muonekano nk. Kwa mtoto , yeye bado ana ngozi ya asili, nyororo, nzuri...kwanini ajipodoe?
Nafikiri ni pale msichana anapojifahamu? na labda tuseme kiumri, kama ni lazima anaweza kuanzia miaka 18, lakini huenda huyu bintii bado yupo shule, sio lazima kujikwatua saaana, ...siunajua tena ...bado mawazo yanatakiwa kuwa shule...mmmh, ni hayo tu

Rachel Siwa said...

@Mdau usiyeweka jina asante sana kwa mchango wako!kijioo chanke na kuanza kujipodoa hahahahaha kweli kazi ipo,Karibu sana uwachunguze hivi vibinti mtu wangu kwikwikwikwikwi na unajua na vihandbag vyao kutwaaaaaa!!!!.

@ kaka emu-three nimekupata wangu,kwaniniajipodoe??
Vipi jibu la dada Edna yeye amekwenda na sababu aionayo.

Haya tuendelee kujifunza kwanini wanajipodoa?

chib said...

Watoto wengine hupenda kuigiliza tu waonavyo mama yao akijiremba, au hata mabinti wakubwa, lakini kiujumla hawajui wanachokifanya.
Wanaojiremba wakiwapa somo watoto wadogo ya kuwa shughuli hizo ni za wakubwa, watoto wanaweza kuwa wasikivu.
Ni sawa na "wanywaji", ikitokea wanajichana ulabu nyumbani, huwaeleza watoto kuwa hicho kinywaji si kizuri kwa watoto, na kutoa sababu kadhaa kuwakatisha tamaa kuomba kuonja, mara nyingi hufanikiwa, iwapo mtoa somo yupo makini na anajiheshimu kiasi cha kuweza ku-win imani ya mtoto