Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 3 May 2011

Waswahili wa Holland na Qeen Day!!!!!!!!


































 Waswahili wa Holland wakisherekea Qeen day.Hii ni Siku muhimu kwa watu wa Holland,Waswahili wa huko nao wakaona vyema kujumuika na wenyeji wao.Tunawatakia Maisha mema na Ushirikiano mzuri.
Je wewe msomaji  huko unapoishi,  Unapenda kuungana na wenyeji wako katika siku zao muhimu?Karibuni sana  Waswahili wote popote mlipo,Mnaweza kutuma picha /matukio yenu.

12 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hapo ni Orange kwa kwenda mbele.. mmependeza sana wapendwa.

Yasinta Ngonyani said...

Mija umeniwahi nami nilitaka kusema kama ulivyosema:-) Safi sana kwa kweli kufuata mila na desturi za pale uishipo....

Simon Kitururu said...

Wamependeza!

rabia said...

asante sana dada siwa tunashukuru kwa kutuunga mkono mungu hawe nawe daima kwa kila jambo

Rachel Siwa said...

Da mija umekosa wewe tuu hapo!

@Yasinta asante sana tunasubiri za huko dada!

@kaka Kitururu asante kwa niaba yao!

@Mdogo wa mimi Rabia pamoja siku zote,lakini naomba huyo brother man anetaka kumbusu mwanagu Naomi anipe mkaja wangu kabisa kabla sijatia timu huko!!!!!!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Tena bahati tu nasoma blogu yako, Dada baada ya kumsoma Simon alipozungumzia siku kuu “Kwanza” huko Amerika... siku kuu waliyoanzisha Waswahili huko kwa wakati wa Christmas na Mwaka Mpya kwa kutotaka kuiga ya kigeni na nikajiuliza bila kufikiri: “Kama ni hivyo Amerika, kwanini huko Uholland waswahili wajumuike na Wazungu?”


Papo hapo nikajipatia mwenyewe tena jawabu, kwani huko Amerika Mzungu na Mswahili wote siyo wenyeji; lakini Uhollandi huko Wazungu ni wenyeji kabisa.


Kusema ukweli, ukiwa uPareni lazima ufanye kama Wapare; na ukiwa Soweto ni lazima tu ufanye kama Wasoweto, sio?


Nakweli, kama Simon alivyosema, MNAPENDEZA JAMAANI!


Nje kidogo ya tundu, Dada aisee! Leo ni siku yangu ya kuzaliwa; na nakuomba utembelee (nakujiunga pia na) blogu yangu mpya http://ninaewapenda.blogspot.com/


Humu najaribu kuelewesha watu ukaribu walugha zetu (Kiswahili na Siswati/Isizulu/Isixhosa).

Pia najaribu niwapate wanablogu wenzangu kama wewe hapo tuwape watoto washule mawaidha ya kufaulu shuleni... mtaalam hapa hamna... na kila mmoja wetu anatoa mawazo yake kusudi Afrika isonge mbele!

Nakushukuru!

Mija Shija Sayi said...

Da' Rachel hujakosea kabisa nimekosekana mimi tu, sasa unasemaje nami nikutumie zangu za Oranje?...kusema kweli sijawahi kuona nchi inayothamini rangi yao ya taifa kama Holland!!

@Yasinta, nyie rangi yenu ipi?

emu-three said...

Safi sana, mkikitana namna hiyo mara kwa mara...mmh, kiswahili na uswahili hautasahaulika au sio

Rachel Siwa said...

Asante kaka Manyanya kwa niaba yao,pia ni kweli ukiwa Soweto ufanye kama Wasoweto kaka yangu.

Hongera ya kuzaliwa kaka Manyanya na Munguakuzidishie miaka mingi sana na baraka zisipungue maishani mwako na familiya pia,

Hongera pia kwa kuzaliwa kwa blog mpya kaka nimekaria huko na nipo bamoja daima,Nikweli kuwapa watoto shule nasi pia tunajifunza zaidi kaka PHIRI!!!.

Ubarikiwe sana!.

Rachel Siwa said...

Da Mija unangoja nini sasa jamani wewetuu wangu muvutisha tuu mipicha ya Orange hiyo!!!!!!!
Tunasubiri kwa hamu mamaaaa Msita!!

@kaka emu-three nikweli wangu hapo ni kiswahili kwakwenda mbele tuu!
Asante sana.

rabih said...

wewe njoo tu dada siwa ujekudai mkaja wako kwani ni mwanao huyo naomi mimi nakuachia wewe kibonge mwenzie nakupenda dada yangu daima mungu hakipenda tutaonana

Rachel Siwa said...

Amina da Rabia na asante sana kwa kuniachia kibonge mwenza!Nami nawapenda sana kwa mapenzi ya Mungu tutaonana wangu, daima pamoja!.