Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 31 May 2011

Siku kama ya Leo dada Upendo Penza Alizaliwa!!!!!!!!

Dada/Mdogo wetu Upendo[Mwana Penza].Siku kama ya leo alizaliwa na kuongeza idadi ya watoto wa Familia ya Bibi na Bwana J,Penza.Pia idadi ya Wajukuu wa Penza.Upendo ana Upendo na Mtu wa Vichekesho na Utani mwingi sana,Pia ana huruma na niwakujitoa sana kwa kila jambo,Liwe la Familia,Marafiki na Majirani. Kama mwanafamilia ninakuwa na wakati mzuri sana kuwa nae popote,  Hasa kwenye mikusanyiko ya kifamilia,Hata ikiwa ya majonzi basi baada ya muda kidogo  mtacheka tuu.
      Upendo, Tunakutakia kila la kheri na baraka katika maisha yako na uwe na wakati mzuri leo na siku zote.


Je mpenzi msomaji eti jina linaendana na Matendo ya mtu?kama vile ukimpatia mtoto jina la Shida na kweli Shida zitamuandama? au Imani za Waswahili/Watu?.


11 comments:

isaackin said...

bantu queen!
HAPPY BIRTHDAY LOVE

Yasinta Ngonyani said...

Kheri ya siku ya kuzaliwa Upendo. Uwe na siku nzuri na kila utakalofanya liwe jema.

SIMON KITURURU said...

Kheri ya siku ya kuzaliwa Upendo!

Kuhusu kama jina linaendana na MATENDO,...
.... mimi naamini ni imani tu za kiswahili hizi,...
.... ingawa IMANI ni kitu cha ajabu ndio maana yasemekana BABU wa LOLIONDO kwa mwendo wa apatavyo wateja KIIMANI atakuwa miongoni mwa matajiri wa kubwa Tanzania baada ya miaka michache na kwa imani kuna wadaio kupona.


Nikiwa na maana:
Kiimani za KISWAHILI kama tu imani yoyote ile ukiamini inaweza kukutokea kweli kitu kisababishacho ukimuita mtoto SHIDA halafu akapata shida za kawaida tu kama za watu wengine ila yeye akazioanisha na JINA LAKE,...
.... anaweza akashindwa kujikomboa kutoka kwenye shida hizo kisa KAAMINI tu kuwa kuanzia jina lake ni NUKSI.

Kwa hiyo watu wawili wenye jina SHIDA na imani tofauti huweza kuathiriwa tofauti kama tu tatizo MOJA liwezavyo kuwa kwa mwingine ni CHANGAMOTO ya kujaribu zaidi na kwa MWINGINE ni kitu cha kumkatisha tamaa.

emu-three said...

Hongera kwa siku yake ya kuzaliwa, mungu amzidishie maisha ya heri na fanaka~
Ama hizi imani za majina, kama livyo imani, ukiamini unaweza ukanasa katika hiyo imani, lakini kwa ujumla, jina ni jina tu, tabia ni kitu kingine kabisa!

mumyhery said...

Happy birth day Dada Upendo, twkutakia kila la heri baraka furaha na afya tele

EDNA said...

Hongera upendo kwa kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Goodman Manyanya Phiri said...

Wala sio imani tu za Kiswahili! Wewe mtoto utampaje jina la "Shida" badala ya "Mshindi" au jina kama hilo linaokaribiana na shida lakini kwa mantiki ya kudumisha uwezo badala ya udhaifu?


Tukumbuke kila binadamu ni binadamu wawili ndani ya mmoja nikiwa na maana ya CONSCIOUS na SUBCONSCIOUS MINDS pia LEFT na RIGHT HEMISPHERES za ubongo.


Wewe unao ubongo wa kulia (moja) na ubongo wa kushoto (mbili) na kila ubongo unawaza upendavyo ndani ya kichwa chako hicho kimoja!


Akili (CONSCIOUS MIND) yenye utawala, yenye sauti, makelele na shamrashamra zote katika maisha ya kila siku inafurahia kutaja na kutajwa jina ("UPENDO! UPENDO! MTOTO MZURI UPENDO!") lakini nguvu za kuleta upendo au hata urembo akili hiyo haina kabisa!


Akili inaotawaliwa (SUBCONCIOUS MIND) ni mtulivu tu (hata kipofu) lakini pia ni msikilizaji makini, PAMOJA NA KUWA MTEKELEZAJI au MTENDAJI MKUBWA katika maisha yako Upendo (ikiwa jina lako la "Upendo" unalionyesha matunda yake kwa jamii yako wala sio kwako peke yako na kujiona hovyo!


Mimi nawaambieni: Hakika, bila jina la "Upendo", mwanamama huyu asingekuwa na tabasamu yake hiyo INTERNATIONAL, wala mashavu yasingekubali namna hiyo!


KIFUPI: Umependeza sana, Upendo! Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa!

Swahili na Waswahili said...

Kwaniaba ya dada Upendo nasema Asanteni sana kwa maombi/sala zenu.

Nami nasema Asnteni sana kwakujibu Eti jina linaendana na matendo ya mtu!

@Kitururu Asante kwa mchango wako!!
@kaka emu-three nimekupata pia!

@kaka Mkubwa Manyanya Asante kwa uchambuzi wako!

Nimatumaini yangu mimi na wasomaji wengine tumefaidika!.

kama wewe hujatoa wazo/maoni yako unakaribishwa pia BADO HUJACHELEWA Yahkeeeeee!!!!!!!!

Ebou's said...

Ohh that's so sweety jamani mimi sijawahi kutembelea ukumbi huu wa swahili na swahille leo nipo swahilivilla ndani ya swahili na swahili. Ndani ya furaha iliyojee kwa dada 'Upendo Penza' kwa siku yako adhimu ambayo siku ya kusherehekea kwa kuzaliwa kwako M/Mungua akupe afya njeema wewe pamoja na familia yako. HAPPY BIRTHDAY PENDA.

John Mwaipopo said...

kitururu na goodman nawanyooshea mikono katika hoja zenu kinzani.na ziendelee kuwa kinzani hivyohivyo huku nikimpongeza dada upendo kwa kuchana kalenda nyingine huku akitabasamu ki-INTERNATIONAL

Swahili na Waswahili said...

@kaka Ebou's na @kaka Mwaipopo wote Asanteni sana kwa niaba ya Upendo!

@kaka Ebou's karibu sana!.