Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 15 May 2011

Jikoni Leo ni kwa Mama Kamala!!!!!!!!!


Haya wapendwa leo tupo jikoni kwa MAMA KAMALA.Kama unavyomuona hapo juu anayetwanga.
Hapa chini ametuandalia Chakula ambacho kina mchanganyiko wa Ndizi,Maharage meupe,Nyanya chungu/Ngogo na Samaki wakavu.Mimi sijawahi kula hicho chakula,Je wewe Mwenzangu umewahi kuonja mchanganyiko huo?Je unaweza kutuambia na Jina la hicho chakula na ni chakula cha Asili ya kabila gani?.
                    Karibuni sana Wapendwa kwa maoni/mawazo yenu.9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi sijawahi kula na wala kusikia ...nami nasubiri jibu...

Anonymous said...

Mimi nishawahi kula. nichakula cha watu kutoka mkoa wa kagera(wahaya). Nikitamu kwani mchanganyiko wake nimzuri,samaki,nyanya chungu na maharagr/we meupe yana fanya mkusanyiko huo kuwa na radha unapo kiweka mdomoni.nimekila sikunyingi sana kwenye miaka ya 80. kaka s

emu-three said...

Duh, kinafanana na chakula cha wapare lakini sio lazima maharage meupe, ...kinaitwaje vile mmmmh, `kishumba'

SIMON KITURURU said...

@M3: Umenikumbusha kishumba UPARENI na maparachichi Mkuu! Halafu baada ya msosi ni MASTAFELI!:-(

Swahili na Waswahili said...

@da Yasinta vuta subira tuu!

@kaka S mbona hukurudia tena kula au jinsi ya kukipika hukufanikiwa kujifunza?asante kwa kututamanisha kimezidi kunivutia.
@kaka emu-3 samahani nimechakachua jina kidogo,lakini ni kaka Kitururu ndiyo kaanzisha KISHUMBA kinapikwaje?

@kaka wamimi Kitururu,je KISHUMBA kinachanganywa na hayo maparachici na Mastafeli? Inaelekea kitakuwa kitamu sana je hapo ulipo huwezi kupika?
Nipeni jinsi ya kupika na vitu/vyakula gani vinahitajika katika huo mchanganyiko wa KISHUMBA!!!!!!!.kaka Kitururu unajua jina lingine la maparachichi? nitakuambia siku nyingine!!!!

Asanteni sana na tuendelee mtu anayejua jina la chakula!!!!!!je wewe unakijua?

emu-three said...

Kishumba kinapikwaje..?,mmmmh ngoja nikamuulize mama Nanihii...oh, easy!
Kumbe, kwanza unapika maharage yaive...oh nimesahau;
Vifaa: ni ndizi na maharage, na ....nini vile, magadi, na chumvi, na mafuta na....oh, hivyo ndivyo muhimu.
Unfanyeje vile: kwanza unapika maharage, siunajua tena ubishi wa maharage, haya yanaubishi wa kuiva. Yakishaiva..eehe, hapo, unakuwa umeshamenya ndizi, zikawa tayari, ndizi mshale ndio safi, unakatakata zile ndizi ziwe ndogondogo,unachukua zile ndizi, unachanganya na maharage ambayo yalishaanza kuiva. Nakumbuka mama alikuwa anapunguza maharage, nusu, anaweka ndizi halafu anarudishia yale maharage juu ya ndizi, anafunika kwa majani ya ndizi...
Unasubiri ndizi ziiive zikiwa ndani ya maharage, ndizi hazikawii kuiva, kule migombani wanafunika na majani ya migomba, ili kuharakisha kuiva, ukumbuke kuweka magadi kidogo na chumvi..na mafuta,
Vikishaiva hivyo, kazi ya pili inaanza, kuvichanganya pamoja na mwiko, unapondaponda vile mpaka vinalainika pamoja, utakuta rangi ya maharage inatawala.
Kiasi gani kwa gani...hapo nimesahauu labda nikamuulize mama nanihii tena,kuwa maharage yanakuwa kiasi gani na ndizi kiasi gani...kufanya life easy wewe kadiria tu...
UKIMALIZA KUPONDAPONDA HIVYO VITU, KISHUMBA TAYARI, KAMA HUTAKI KISHUMBA, UNAWEKA MAJI MENGI KINALAINIKA KAMA MTORI...HAPO HUITWA KIOMBO...SAFI SANA!
Kuhusu maparachichi na nini vile, mastafeli, aaah, hayo si matunda tu, unakuja kuyaponda ponda na kishumba baadaye kikishaiva, ni wewe mwenyewe tu ukipenda kulumangia au kuchanganya...kazi kwako...
Mhhh, labda tusubiri sehemu ya pili...lol nimesahauu nikadhani naandika stori...bye

SERENGETI GRILL said...

jamani chakula hiki ni kitamuuuu!!!, niliwahi kula bukoba ni kitamu mno!!! yaani mimi kila nipatapo mahitaji huwa napika jiana silijui ila wakati mwingine mimi badala ya maharage meupe huweka mboga za majani.

EDNA said...

Mmmmh mimi bado lakini ningetamni kuonja.

Swahili na Waswahili said...

Asante Serengeti kwakuhakikishia na karibu sana maana wewe ni mtaalam wa makulaji!!!!!!!

@daEdna namipia!

@kaka emu-three Ubarikiwe sana mpesalamu na Asante mama nanihiii kwa kukufunza nawewe ukanifunza mimi na wengine waliopita hapa nao watafaidika na Mapishi ya KISHUMBA,PIA NIWEKA MAJI MENGI KITALAINIKA KAMA MTORI...LAKINI CHENYEWE KITAKUWA KIOMBO!!!!!!!.
HIKI KIOMBO SIJUI KAKA WA MIMI KITURURU KAMA ANAKIJUA.
TUSUBIRI AKIINGIA HAPA ATASEMA MWENYEWE!!!!!.