Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 25 May 2011

Je Utoto wako Ulipitia huku???.

Kunamambo mengi sana  watu hupitia katika safari ya Maisha ya Utoto mpaka Ukubwani.Kama Udokozi wa mboga,pesa,Sukari.Pia Kujaribu kuvuta Sigara,Bangi.Utoro shuleni,Ugomvi/Ubabe,Matusi na mengi mabaya ambayo hayapendeezi katika jamii.Je wewe ulikuwa katika kundi lipi katika haya na je ulibadilika mwenyewe au kwa msaada wa Wazazi/walezi?. Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana.

8 comments:

Entertainer said...
This comment has been removed by the author.
Yasinta Ngonyani said...

Mimi nilikuwa mshamba wa hivyo vyote. Nangoja wengine watoe yao:-)Ahdsante kwa kuliandika hili wazo Rachel kwani ni muhimu sana kujadili ya kale hata kama mabaya au mazuri.

John Mwaipopo said...

yasinta usione soo sema tu. haiwezekani kukosa katika yote hayo.

mie nimo kwenye mengi hapo likiwamo la kuvuta sigara na kuacha mwenyewe.

Simon Kitururu said...

Mie kibao hayo nimeyapitia kasoro udokozi wa pesa ,ubabe, na bangi ingawa nahisi labda ni kwa kuwa tu haikuwepo katika mitaa nilikokuwa nashinda utotoni, ila majani ya mpapai nilivuta, na gongo ambayo tulikuwa tunaimix na fanta nilikunywa nk.

Na pia nilikuwa napenda kudokoa maziwa yaunga ila sio sukari.

Na nilibadilika mwenyewe kwa kuwa WAZAZI hawakuwahi kustukia hayo!

Mimi wazazi wangu kipimo chao cha mtoto mtulivu ilikuwa ni kama unafaulu darasani na unaenda kanisani! Na nilikuwa naenda kanisani kwa bidii na nafaulu darasani na napenda kujisomea mpaka ilikuwa ni kawaida kwao kuniambia niache kusoma nikalale kwa kuwa nilikuwa namchezo wakupitiliza na waweza kunikuta saa kumi usiku niko macho nimenogewa na kitabu hata kama ni cha WILLY GAMBA kitu ambacho kilifanya mambo mengine kama nikichelewa kurudi nyumbani au tu nikijichanganya mtaani wasishuku sana kuwa na wadau tunaonja gongo.:-(

Rechel mbona lakini hujaongelea wewe nini umepitia?

... ingawa nahisi kwa kujipikilisha utotoni WEWE ulishawahi kwenda nyumbani kudokoa mchele bila kuomba ili ukajipikilishe na na mashoga zako mtaani!.:-)

Tukiachana na hayo:
Umeshawahi kujiuliza ni kwanini WATOTO hufikia kudokoa au kujificha katika mambo ambayo labda wangefanya mbele ya wazazi kama kusingekuwa kuna kitu kifanyacho WATOTO waogope wazazi?

Huhisi labda ni kosa pia la WAZAZI kufanya watoto wafiche wafanyayo kwa wazazi?

emu-three said...

Naona akina dada siku hizi mnakumbukia `enzi hizo...' kwakweli `utoto' una viroja vyake,na ukikumbuka ni `tamithilya nzuri sana'
TUPO PAMOJA...mimi sikuwa mtukutu kihivyo...lol

Rachel Siwa said...

@kaka Kitururu nanukuu:Rachel mbona lakini hujaongelea wewe nini umepitia? Hahahahahah kwikwikwikwi ohhhhhhiiiiiiii yaani hapa kwanza hiyo sentensi yako inanikumbusha mbali hahah yaaani mbona wewe ufanyi unawaambia wenzio tuu?kicheko tena yaani kaka wa mimi kweli wewe ni Kitururu mawazoni!!!!!!leo nimeamini!ok Au wewe ni mrithi wa yule Shekhe aliyekufa juzi?

Kwasababu hayo uliyoandika kuhusu mimi na shoga zangu duh si uongo ni kweli tupu kaka Umenipiga jicho la kiundani sana hahhahahhha yaani leo umeniweza kaka wa mimi,Nikiongeza hapo nilikuwa napenda kuwa mwalimu na dalasa langu lilikuwa linajaa, sasa hicho kipondo mbona walikuwa wanakoma!Mama yangu alikuwa anawaambia nanyi mnamtakia nini huyo mwalimu mwalimu gani anawapiga hivyo?wanaacha leo kesho tukianza tena mchezo wa kishuleshule wanakuja kwa mwalimu Rachel.hahahhaa @ Kaka Kitururu na wengine asanteni sana maana nikianza kuandika ya utoto hapa tutakesha!!!!!!!

@da Yasinta na kaka Mwaipopo na mkuu emu-three Tupo pamoja!

Lkini yote 9 duh kaka Kitururu wewe ulikuwa kiboko!!!!!!!!

chib said...

Watoto hupenda kuiga kwenye mambo wanayoyaona wakubwa wanafanya. Wakigundua ni kitu mbaya, basi hujificha na kukoroga mambo.
Mimi kwa ufahamu wangu naona nilikuwa mtii sana, na nilichoambiwa hapana, nilikuwa nazingatia!

Rachel Siwa said...

Ubarikiwe kaka Chib!