Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 31 May 2011

Siku kama ya Leo dada Upendo Penza Alizaliwa!!!!!!!!

Dada/Mdogo wetu Upendo[Mwana Penza].Siku kama ya leo alizaliwa na kuongeza idadi ya watoto wa Familia ya Bibi na Bwana J,Penza.Pia idadi ya Wajukuu wa Penza.Upendo ana Upendo na Mtu wa Vichekesho na Utani mwingi sana,Pia ana huruma na niwakujitoa sana kwa kila jambo,Liwe la Familia,Marafiki na Majirani. Kama mwanafamilia ninakuwa na wakati mzuri sana kuwa nae popote,  Hasa kwenye mikusanyiko ya kifamilia,Hata ikiwa ya majonzi basi baada ya muda kidogo  mtacheka tuu.
      Upendo, Tunakutakia kila la kheri na baraka katika maisha yako na uwe na wakati mzuri leo na siku zote.


Je mpenzi msomaji eti jina linaendana na Matendo ya mtu?kama vile ukimpatia mtoto jina la Shida na kweli Shida zitamuandama? au Imani za Waswahili/Watu?.


Saturday 28 May 2011

Usingizi Unaraha yake!!!!!!!!

Kuna asiyependa kulala?Usingizi nao ni Starehe jamani au mnasemaje?Nawatakia mwisho wa wiki mwema.

Wednesday 25 May 2011

Je Utoto wako Ulipitia huku???.

Kunamambo mengi sana  watu hupitia katika safari ya Maisha ya Utoto mpaka Ukubwani.Kama Udokozi wa mboga,pesa,Sukari.Pia Kujaribu kuvuta Sigara,Bangi.Utoro shuleni,Ugomvi/Ubabe,Matusi na mengi mabaya ambayo hayapendeezi katika jamii.Je wewe ulikuwa katika kundi lipi katika haya na je ulibadilika mwenyewe au kwa msaada wa Wazazi/walezi?. Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana.

Monday 23 May 2011

Tracey atimiza miaka 10!!!!!!!!!!!!!

 Tracey-Sarah, Ametizimiza miaka 10,hapo amepozi akitafakali duhh nimekuwa dada sasa.

 Yaani mimi ndiyo nimefika maika hii?



 Kikosi kamili cha Watoto wa Coventry Christian Swahili Fellowship,Kikiongozwa na dada mkuu dada Damari Kihauka chini ya Mwenyekiti da Mija. Nitakueleza Siku nyingine mambo mengi kuhusu kikosi hiki!!!!!!

 Tracey na dada Damari wakitayarisha Keki ili kila mmoja apate.



                                       


                      Tracey akipokea zawadi maalum kutoka kwa kaka Joel.
 Wamama nao hawakuwa nyuma,kwaniaba ya Wazazi wote wa Swahili Felloship.

                                   dada Tracey-Sarah anasema Asanteni sana na Mungu awabariki!!!!!!!

Friday 13 May 2011

Kutokana na Tatizo la kublog, Sabrina atafuta Njia!!!!

Tangu jana kulikuwa na tatizo la kublog,,Mtoto Sabrina akaona ngoja ajaribu kutengeneza!!!!!Alifikiri Tatizo lipo kwa Shangazi yake tuu.Wapenzi wa SwahilinaWaswahili poleni kwa Usumbufu wowote uliojitokeza sasa tunaendelea kama kawaida.

Saturday 7 May 2011

Watoto na Urembo!!!!!!

Mzazi/Mlezi na Mwana familia.Unamawazogani kwa watoto wadogo na  kujiremba?.
Hasa kwa mtoto wakike wa Leo/Sasa, Unafikiri ni umri gani kwake unafaa kwa kuanza kupaka,Shedo,Wanja,Rangi za mdomo,Kunyoa nyusi, kupaka Poda na mapambo mengine yanauotumiwa na Wanawake /kina Mama.Na si kila Mama/Mwanamke anayependa kujiremba pia.
Karibuni sana kwa Kuelimishana na Kusaidiana katika Malezi ya Watoto wetu.

Tuesday 3 May 2011

Waswahili wa Holland na Qeen Day!!!!!!!!


































 Waswahili wa Holland wakisherekea Qeen day.Hii ni Siku muhimu kwa watu wa Holland,Waswahili wa huko nao wakaona vyema kujumuika na wenyeji wao.Tunawatakia Maisha mema na Ushirikiano mzuri.
Je wewe msomaji  huko unapoishi,  Unapenda kuungana na wenyeji wako katika siku zao muhimu?Karibuni sana  Waswahili wote popote mlipo,Mnaweza kutuma picha /matukio yenu.