Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 25 April 2011

Wazazi wa sasa na Malezi!!!!!!!


Katika pitapita zangu nimekutana na malezi tofauti ya Watoto.Hasa ya kule Nyumbani Afrika/Tanzania na Wanaoishi nje ya Nchi.Watoto wa Nyumbani wengi wao bado wanaheshima kwa wakubwa wote awe mzazi au jilani,kwa Mgeni au Mwenyeji,Akufahamu/kukujua au Asikufahamu/Kukujua.Unyenyekevu na Usikivu. na mengine mengi.
Watoto wa waishio nje ya Afrika/Ng'ambo Wengi wao ni wabinafsi, wanauthubutu wa kukujibu lolote analoweza,anaweza asikusalimie,hawana karibu wala heshima kwa wakubwa,wanamaamuzi zaidi na matakwa yao,Akisema sitaki na hataki,Na  baadhi ya wazazi wao wanawasilkiliza zaidi, Hata  hawana Aibu kwa matendo ya watoto wala Hofu.
Je Msomaji wewe unamawazo gani katika haya,je ni Mazingira,Maendeleo,Malezi ya kisomi au ni nini kwa hawa wa Nje?.
Na jee hawa wa Nyumbani ni Waoga,Hofu,Kutojiamini au Washamba na wanapitwa na wakati?
Karibuni sana  kwa Kuelimishana na Kufundishana .

12 comments:

nyahbingi worrior. said...

This is what i have preaching.

Ugenini....tabia ya maisha ya ugenini hayaendani na maadili ya nyumbani(Afrika).

Nini kifanyike?ukiwaambia warudi hawataki.

Nimependa sana hii..nanukuu

Watoto wa waishio nje ya Afrika/Ng'ambo Wengi wao ni wabinafsi, wanauthubutu wa kukujibu lolote analoweza,anaweza asikusalimie,hawana karibu wala heshima kwa wakubwa,wanamaamuzi zaidi na matakwa yao,Akisema sitaki na hataki,Na baadhi ya wazazi wao wanawasilkiliza zaidi, Hata hawana Aibu kwa matendo ya watoto wala Hofu. mwisho wa nukuu.

Yasinta Ngonyani said...

Mimi naona inategemea na malezi mtu ayapatayo. Yaani hii ipo popote pale si Afrika wala Ulaya,Asia,Amerika kwote ni malezi gani mtu ameyapata tangu kuanzia msingi...ukimöea mtoto ndivyo anavyokuwa. Nimeona mara nyingi sana kwa kweli inatia uchungu sana utakuta mtoto kama alivyosema< da`Rachel anamjibu mtu aliyempita makamo utadhani ni rafiki yake na pia wazazi wanawaogopa watoto wao hata kuwatuma sasa hii sijajua kama ni heshima au?....tuendelee jamani na mada hii nzurii ya mafunzo

Anonymous said...

Malezi ya wazazi nikuweka misingi ya utamaduni ndani ya nyumba,upendo kati ya unaowalea,na kuondoa chuki kumuonesha unaemlea,hapo utafaulu na matunda ya mtoto umleae ata akiwa wakumlea tu si wako,ila alikuwa katika himaya yako ndani ya ulezi wako,

Goodman Manyanya Phiri said...

@Yasinta

Kweli kabisa! Haya mambo hayana mipaka wala bendera la nchi au bara fulani. "Umleaavyo ndivyo akuavyo" (nahisi ndicho Kiswahili chake).

Mimi mtoto wangu sitaki hata kamwe apigwe; lakini siku nikimgundua haonyeshi tabia njema kwa watu wazima hata wakiwa wageni, HAKIKA ITAKUWA VIGUMU KUPATA KIZUIZI CHA KUMPIGA TU!

Naye Dada Rachel akija nyumbani kwangu kuniambia amempiga mwanangu kwa nia ya kumkanya, huyo Rachel hata kumlipa kabisa nitamlipa!

MSINGI: Silei hata kamwe jambazi nyumbani kwangu!

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zanguni!
Kuchapa mtoto si ndio kumfunza mtoto. Mimi kama mzazi pia naweza kusema sijawahihata siku kuwachapa wanangu na nipo kinyume kabisa na kaka Phir kama mtu atamchapa mwanangu kwa kweli nitazuka mbogo. Kwani kuna njia nyingi sana tu za kumfunza mtoto ila si kumpiga. Naamini kumpiga hakumfanya aache fujo/ujambazi kwani ndo kwanza atakuwa SUGU. Chukua muda wako kaa na mwano na ongea naye kwa utaratibu na wala usionyeshe ukali na pia kaa katika ile saizi aliyo naye yeye. Na kama amemkosea mtu basi kama mimi nitataka yule mtu aje kwangu na tutakaa na kuongea wapi kumetokea tatizo...haya ni malezi yangu na pia ni malezi pia niliyoyapata kwa walezi wangu na nayaendeleza na naanmini nafanya la msingi---Ruksa kuwa tofauti nami...

Simon Kitururu said...

Bado natafakari hoja!:-(

Rachel Siwa said...

kaka Kitururu wewe tafakari,sisi tunasubiri kujifunza tuu!

@kaka Nyahbingi kwikwikwi kurudi hawataki!!si kwamba wote wa nyumbani wametukuka lakini,binadamu tunatakiwa kutawanyika ndiyo maisha.

Nakubaliana na da Yasinta na kaka Manyanya kausemi pia kana ukweli mwana umleavyo ndivyo akuwavyo!Hata kama tutawachapa tuu haisaidii zaidi kutafuta tatizo nini na linasababishwa na nini.

Nyumba ni msingi basi tuanze kuwafundisha na kuwaelimisha wakiwa wadogo sana,maana hatua ya kwanza inaanzia kwa wazazi.

Sasa yakitokea hayo mengine wa kwanza kulaumiwa ni nani?.

tuendelee kujifunza ngoja tusubiri wengine wanamawazo gani,Tuzidi kuelimishana na kusaidiana.Kunipinga huu mtazamo wangu IMO!!!!!!!!.

emu-three said...

Kulea nako ni `elimu'...kulea kunahitaji busara, sio mtulinga!

Anonymous said...

Swala la malezi ya mtoto ni gumu kidogo ukilifananisha namalezi ya watoto wa kiulaya.kwa upande wangu kupiga mtoto si vizuri,lakini kwa wale wazazi inapotokea umempiga mtoto kuna kuwa na sababu.sasa hivi hata hawa wenzetu wa ulaya wana hangaika juu ya kuwalea watoto wao.mimi nafikiri hakuna ubaya na nivizuri na ninapenda jinsi nilivyo lelewa kitanzania, nakubali nilipigwa nk lakini kwa wazazi walio kuwa wanajuwa nini wanakifanya,,hasa kufuatana na mazingira yaliyokuwa yanatuzunguka wakati ule,malezi ya kitanzania mimi ndo yamenifikisha hapa nilipo.kitu kimoja ambacho nimuhimu na ndicho naona katika malezi yetu ya kibongo kinapungua,nimzazi kuwana mahusiano ya karibu na mtoto,kuna umbalisana kati ya baba na mtoto na mtoto na mama,kiasikwamba wazazi unawaona siyo rafiki. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka S! nakuunga mkono hapa uliposema ya kwamba kuna wazazi na watoto ambao wakionana tu wanajiona kama ni maadui. Hakuna hata ule utani kwa jinsi wazazi walivyo wakali hakuna urafiki kabisa. Hii si nzuri kabisa.

Mija Shija Sayi said...

Mimi ninawapenda sana wazazi wanaoweza kuwafunza adabu watoto bila kuwachapa na watoto wakasikia, binafsi mimi siwezi kabisaa, sasa jamani kina Yasinta tunaomba nasisi mtupe hizo skills ili tujifunze..

Lakini pamoja na hayo naomba tukubaliane kwamba kuna watoto wengine ni makusudi sana na bila fimbo mambo huwa hayaendi, hivyo naomna fimbo nayo ina nafasi yake katika kutengeneza adabu. Si mnakumbuka hata wakati wa Nyerere adhabu za fimbo zilikuwapo..wala rushwa walikuwa wakikiona cha moto..

Haya Yasinta na wengine tusaidieni..

.

Rachel Siwa said...

Mija pia tuliosoma shule za ST.Government mwehh tulichapwa haswa!

@kaka S nikweli usemayo urafiki kati ya mtoto na wazazi ni muhimu sana.

asanteni wapendwa na tuendelee kujifunza.
@kaka Kitururu popote ulipo,tunahiji mchango wako, kwani Ahadi ni deni!!!!!